Jamani nimetapeliwa nichukue hatua gani?

Chizbot

Member
Dec 8, 2019
7
8
Habarini wakuu,

Wakuu nimetapeliwa au niseme kwa lugha nyingine nimedhulumiwa na jamaa yangu, iko hivi awali huyu jamaa alikuja kwangu akidai nimwazimishe computer yangu akadai kuna kazi anaenda kuifanya nikampa two days later akaja kwangu tena akadai vibaka wamemkaba wamemnyang'anya pesa yote aliokuwa nayo akaomba nimkopeshe laki 3.

Baada ya siku 4 angenirudishia kwa vile ni jamaa yangu tumetoka mbali na tumepitia misoto mingi wote nikaamua kumpa kiasi hicho, sasa juzi nimefatilia computer yangu na hela yangu kwake naambiwa ametokomea kusiko julikana na nikijaribu kupiga simu yake haipatikani kabisa asee yaani hapa nilipo nasikia kichwa kinauma balaa tafadhali nipeni mawazo hatua gani nichukue dhidi ya huyu jamaa.

Shukrani
 
Nenda kwa mganga wa kienyeji!

Anyway

1. Karipoti polisi juu ya upotevu, wizi na mwizi mwenyewe. Hii itakusaidia wewe pale ambapo kompyuta yako itakapotumika kutenda uhalifu itajulikana kuwa wewe hauhusiki. Pia utapata RP ya polisi.

2. Mtafute jamaa bila jasho mdogomdogo utampata tu na jinai haiexpai ukimnasa tu, polisi. Atatema kila kitu na gharama juu.

3. Kama ana kwake au unajua kuwa ana mali yoyote popote kachukue mali yoyote yenye thamani sawa au pungufu ya thamani ya mali alizotokomea nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PM mshana jr ndo kiboko yao. Mwombe amuwehushe aokote makopo ili watu wakuogope. Kinyume cha hapo huwezi kwenda polisi kwa kuwa hujasema ka mliandikiana. Hata hiyo comp huna uwezo wa kumkamata nayo kwa sababu hata pass word yake ulimpa.
Mloge tu yaishe
 
Hahaha Mshana Jr kuna kazi huku
 
PM mshana jr ndo kiboko yao. Mwombe amuwehushe aokote makopo ili watu wakuogope. Kinyume cha hapo huwezi kwenda polisi kwa kuwa hujasema ka mliandikiana. Hata hiyo comp huna uwezo wa kumkamata nayo kwa sababu hata pass word yake ulimpa.
Mloge tu yaishe
Asee unanitisha kaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom