Jamani nimeota ndoto mbili zenye mfanano, hebu tufafanuwe

mwakyambikig

Member
Mar 21, 2011
85
125
Habari ndugu jamaa na marafiki, kama kichwa cha habari kinavyo jionyesha,Mimi ninamuamini sana Mungu na ninaamini kila jambo linalo tokea huwa linamaana Fulani! Majuzi kati hapo nimeota nawafukuza nyoka watatu, wenye rangi,tofauti, nyoka,hao walikuwa wakitokea maaneo ya nyumbani kwangu""! Juzi tena nikaota kuna mvamizi alikuja kunivamia nyumbani kwangu, alikuja na bunduki, naye nikawa ninamfukuza, na akawa anakimbia, Mimi sikuwa na silaha lakini namfukuza Mtu mwenye silaha, basi, ndio hayo wapendwa, labda kuna mtu aliwai ota ndoto kama, hizi, karibuni kwa ufafanuzi*""
 
jerry joshy

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
403
500

ndoto zitabaki kuwaaa ndoto ingekuwaa ndoto zinaa maana basi mimi ninavyootaga nimeokotaa magunia ya ela ningekuwaa bilioneaaa
kwanzaaa we ni shujaaa umekimbizaa majokaa bilaa silaa then ukaja kuwakimbizaa majambazi wenye mabunduki hujioninkama wewe ni champion ??maana yake ww ni shujaaaa
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Habari ndugu jamaa na marafiki, kama kichwa cha habari kinavyo jionyesha,Mimi ninamuamini sana Mungu na ninaamini kila jambo linalo tokea huwa linamaana Fulani! Majuzi kati hapo nimeota nawafukuza nyoka watatu, wenye rangi,tofauti, nyoka,hao walikuwa wakitokea maaneo ya nyumbani kwangu""! Juzi tena nikaota kuna mvamizi alikuja kunivamia nyumbani kwangu, alikuja na bunduki, naye nikawa ninamfukuza, na akawa anakimbia, Mimi sikuwa na silaha lakini namfukuza Mtu mwenye silaha, basi, ndio hayo wapendwa, labda kuna mtu aliwai ota ndoto kama, hizi, karibuni kwa ufafanuzi*""
Haya ni mambo ya vyeti feki na utumbuaji. Kesi yako utashinda na utaendelea na ajira yako
 
molwe

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
260
250
Pole, ngoja waje wajuaji! Hiyo ya bunduki nafahamu tafsiri yake, kwanza kama kaipiga ni kwamba kuna watu wamekutengenezea mtego wa kifo, kama haijapigwa kuna watu wanamipango ya kutaka kutoa uhai wako kichawi! Ya nyoka na wengine wakusaidie.
 
Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Majuzi kati hapo nimeota nawafukuza nyoka watatu, wenye rangi,tofauti, nyoka,hao walikuwa wakitokea maaneo ya nyumbani kwangu""! Juzi tena nikaota kuna mvamizi alikuja kunivamia nyumbani kwangu, alikuja na bunduki, naye nikawa ninamfukuza, na akawa anakimbia, Mimi sikuwa na silaha lakini namfukuza Mtu mwenye silaha, basi, ndio hayo wapend
Bwana Yesu asifiwe mtumishi. Ndoto yako inakupa taarifa juu ya mtu kutafuta au kuiba mawasiliano yako rohoni ili usifanikiwe pasipo Mungu. Hivyo ongeza juhudi katika kumtafuta Mungu maana muda si mrefu kiroho chako kitakufa na maisha yako yatabadilikia hivyo omba ulinzi kwa Mungu. Ndoto ya kwanza, ya pili ikija ya tatu hiyo itatokea. Upesi naam hakika itatokea hivyo rudisha uwepo wa roho mtakatifu nyumbani kwako ili shetani asipate nafasi ya kukushitaki.
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
14,645
2,000
Mkuu kwani unaishi kibiti?...
Tukirudi kwenye hoja, kama unamwamini Mungu, hata kama ndoto haujaielewa vizuri, cha msingi ni kuomba tu akulinde na awe ngao yako. Akili zetu zina ukomo, maarifa yetu hali kadhalika hayawezi kuelewa kila jambo.

Jiweke chini ya mkono wa Bwana, atakulinda na hali zote! Usijaribu kwenda kwa waganga tu!
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,696
2,000
Kama upo Kibiti utafanikiwa kuwaangamiza majambazi, jitahidi kuwatafuta popote unapowasikia.
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
958
1,000
Nyoka ni umbo au ishara ya shetani,na hiyo ndoto INA maana kwamba Mungu anakuonyesha kuwa kuna kitu shetani anawinda kwako. kitendo cha nyoka kukujia au kuingia kwako ni ishara kwamba kuna mlango uko wazi.chakufanya kwanza Ombo toba kwa Mungu halafu omba kwa kunyunyiza damu ya Yesu katika lile eneo unapowaona maana Damu ya Yesu ndio ukombozi wetu na inanema mema kwa ajili yetu. Kumbuka pia ndoto ni lango ktk ulimwengu wa roho na linaweza kutumiwa na Mungu au shetani.rejea maandiko mh10:8,mwanzo3:15 kutoka12:17,22,23.
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,900
2,000
nyoka ni adui , sasa kuna maadui wanakuvizia ila inaonekana utashinda zidisha sala mkuu
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
958
1,000
Kuhusu mtu mwenye bunduki hiyo pia ni ishara ya shetani ambae haji ila kuiba, kuchinja na kuharibu,cha kufanya same as hapo juu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom