Jamani nimefurahi sana

Karibu sana nafasi bado zipo nyingi sana!, lakini kua makini make hapa ni zaidi ya bungeni!
 
Angalizo- humu jamvini kuna makundi mbalimbali.
1.Wanaojifanya kujua kila kitu. Siasa wao,uchumi wao,utamaduni wao uwe makini.
2.Wapo waliopo mahsusi kutetea ujinga hata kama uko wazi-kua makini nao
3.Wapo wale ambao hawathamini mitazamo ya wengine kwa lolote lile-kua makini nao
KWA MUDA MFUPI TU UTAWAFAHAMU.

angalizo jingine awe mvumilivu na mchache wa jazba lasivyo jamvi litamshinda.
 
Jamani leo nimefurahi sana yaani nilikuwa naangaika kujiunga na Jamii forum na hatimaye leo nimeweza ila tangu saa tisa natafuta sehemu ya kuingizia bila mafanikio mpaka saa hizi ni saa 12 jioni ndio nimepaona. Jamani mnipokee mi ndio wa kwanza kijijini kujiunga.
umeshapata sehemu ya kuingiza?angalia usikosee ukaenda kinyume na .............
then tuambie una umri gani?
 
Jamani wengine nimeshindwa kuwajibu kwa sababu nilijihimu shambani tangu saa 11 alfajiri na saa hizi ndio nimekaa hapa kwenye kitindi cha ulanzi huku nikiendelea kupata nyamtutu baridi na kuburudika na jamii forum. Kweli jamii forum raha sana asikwambie mtu.
 
Jamani leo nimefurahi sana yaani nilikuwa naangaika kujiunga na Jamii forum na hatimaye leo nimeweza ila tangu saa tisa natafuta sehemu ya kuingizia bila mafanikio mpaka saa hizi ni saa 12 jioni ndio nimepaona. Jamani mnipokee mi ndio wa kwanza kijijini kujiunga.

Karibu Mwayego
 
Karibu sana kiongozi! Tahadhari kuchangia mada za vyama vya siasa; utapata matusi usiyotegemea!
 
Hongera mwenzangu na mim mi bado kabisa sijaelewa chochote nikitaka kumtumia mtu text inakataa pia kuedit profile yangu yana asilimia 90 ya mambo yote sifaham naomba mnieleweshe pia

Lulu ni ww yule wa Foolish age ama Mwingine..
 
Back
Top Bottom