Tougher
JF-Expert Member
- Jul 9, 2013
- 245
- 65
Ndugu zangu,
Mimi ni mkulima mdogo wa korosho katika mkoa wa pwani. Mazao shambani mwaka huu hayakuwa haba licha ya kuibiwa kidogo (huu ni uzembe wangu niliajiri mtu asiye muaminifu licha ya kumpa ujira mzuri), nilifanikiwa kupata jumla ya kilo 1500 za korosho.
Malengo yangu ya mwaka huu hayapo kabisa katika kuuza korosho hizi katika chama cha ushirika kwa sababu bei za kule ni ndogo kulingana na alternative ya kubangua mwenyewe. Hivyo dhamira yangu ni kubangua na kuuza korosho iliyobanguliwa. Katika hili la kubangua nakumbana na tatizo moja, siruhusiwi kuondoka na korosho yangu toka katika kijiji ninacholimia ninaambiwa ni amri ya mkuu wa wilaya. Amri ni kuwa natakiwa kuuza korosho yangu katika chama cha ushirika, nami sitaki kwa sababu nilizozitaja hapo juu. Ninachofanya kwa sasa ni kutorosha kidogo kidogo na kuzibangua kabla sijawauzia wateja wangu kwa bei ya shilingi 14,000 kwa kilo moja (bei ambayo hakuna chama cha ushirika wanaweza kunipa bei hii).
Kinachoniuma na kunifanya niwaombe ushauri wa namna gani nifanye ili niweze kuhamisha korosho yangu bila mikwara mingi kama hii? INANIUMA SANA KWAMBA INANIBIDI NIHAMISHE KWA USIRI KOROSHO NILYOZALISHA KWA GHARAMA ZANGU KWENYE SHAMBA LANGU MWENYEWE KAMA MWIZI.