Jamani ni mshauri nini huyu?

Jamani ni mshauri nini huyu?

Home First

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2013
Posts
609
Reaction score
248
Ninajamaa yangu kanifuata na kunieleza haya:
Mimi kipindi niko shuleni niliwahi kuzaa watoto wa 3 ingawa kila mtoto ana mama yake napia nasikia eti nina mtoto mwingine wa 4.
Baada yakumaliza masomo nilipata kazi, pindi nipo kazini nilikutana na dada mm1 ambae nilimpenda sana toka moyoni sikusita kumueleza ya moyoni mwangu nae bila ajizi alinieleza kila kitu kuwa aliwahi kuolewa nakuzaa watoto wa 2,
ila walikorofishana na mwanaume wake na akaolewa na mwanaume wa 2 ila hakuzaa nae, baadae wakaachana kwa kuwa huyo mwanaume wa 2 alikuwa hataki watoto wa mwanamke.
Sasa kama utakuwa tayari kulea watoto zangu hakuna shida nimekubali nakama hauko tayari kwa watoto zangu siko tayari.
Kwakua nilimpenda nilikubaliana nae nakweli tuliishi pamoja, aliwahi kushika mimba ikatoka hadi hivi ninavyo kueleza sijawahi zaanae,tatizo kubwa lililonileta hapa nikwamba kabla sijafunga nae ndoa alikuwa akinihudumia vizuri sana kama: maji ya kuoga,chakula na mapenzi, ila baada ya kufunga ndoa huduma zimepungua imebaki moja ya mapenzi.
Ilikuepusha shari huwa najichemshia maji naoga baada yakuoga naenda Hotelini kunywa chai huku yeye mke wangu bado kalala,nikirudi huwa ananiuliza utakunywa chai nami namueleza hapana nimekwisha kunywa basi ataanza kunitukana hapo hadi nashindwa kuvumilia nami naanza kumjibu: (ALIPO FIKIA HAPO NIKAMUULIZA HUWA HUUMPIGI?) (HAPANA SIJAZOEA KUPIGANA NA WALA SIJUI KUPIGANA).

Sasa nikianza kumjibu2 anaanza kulia hadi abembelezwe,sasa nimechoka nimemueleza kuwa nitaoa mwanamke mwingine nae kusikia hivyo akakusanya mizigo yake eti mimi na yeye viishe, sasa nifanyeje?
NDUGU ZANGU WANA JF HILI NDILO SWALI NIMEPEWA NAOMBA TUMSHAURI LAKUFANYA JAMAA YETE.

NAWASILISHA KWENU.
 
sasa wewe kaachwa na wanaume wawili yeye ndio akajiona kidume sana kwamba atammudu. huyo sio mwanamke bwana....yeye amuache asepe zake ndio kashazoea maisha hayo
 
Kapimeni HIV naona huo mzunguko siyo bure lazima kuna mambo hapo. Hiyo kutupa mimba n ahasira zisizo na kichwa wala miguu ni ubongo umeanza kuota mbawa. Jichunguzeni afya zenu khalafu mengineyo nitawajuza wakati mwafaka.
 
Walw watoto wake wa3 wako wapi?
 
Sasa yeye anachotaka ni nini kama ameshamuleza mwamke kuwa anataka kuoa mwanamke mwingine na yeye mwanamke akafungasga? Au alikua anatikisa kiberiti. Inaonekana huyo mwanamke ana matatizo.

Kama nichai ajiri beki tatu
 
maneno tu ndo yamfanye abebe virago vyake?labda kama kuna sbb nyingine....hayo yote yalikuwa ni ya kuzungumzika na kutafutiwa suluhisho.....lkn kama mke ameamua kusepa mume atulie tu,hana haja ya kubembeleza.
 
jamaa anataka kufa watoto wake wawe machokoraa.....huyo mwananke hamfai atulize ball....
 
Kapimeni HIV naona huo mzunguko siyo bure lazima kuna mambo hapo. Hiyo kutupa mimba n ahasira zisizo na kichwa wala miguu ni ubongo umeanza kuota mbawa. Jichunguzeni afya zenu khalafu mengineyo nitawajuza wakati mwafaka.

ukimwi hawana wako fiti labda ndio maana kila mm1 anajidai!
huyu:nitaoa, yule: naondoka.
 
wako kwa mama zao.

Basi ye ndiye mwenye matatizo, wala asimlaumu huyu mdada... wanawake watatu wote azae nao halafu hakuna hata mmoja aliye tayari kuishi naye!!!
Na bado anayeishi naye sasa naye keshakusanya vitu vyake?!!! Mwambie huyo jamaa yako anahitaji marekebisho makubwa sana kwenye tabia zake...
 
maneno tu ndo yamfanye abebe virago vyake?labda kama kuna sbb nyingine....hayo yote yalikuwa ni ya kuzungumzika na kutafutiwa suluhisho.....lkn kama mke ameamua kusepa mume atulie tu,hana haja ya kubembeleza.

Ok!nitalifikisha.
 
Hao wamekutana...waache tu hivyo hivyo, watajinyoosha wenyewe,
 
mwambie atafute wazee wenye busara zao wakae waongelee hilo swala mkewe akiwepo kila mmoja awe muwazi aeleze shida zake then nadhani mtapata solution.
 
kama mwanzo alimuhudumia vizuri
kuna jambo katikati,akae nae amuulize
nini tatizo na ajirekebishe akishajua tatizo!
na ajue kua huyo dada hajiamini kutokana na kuachwa kila mara!
yeye ndio amfanye mwenzie ajione wa thamani na ajiamini
kama zamani!asimtende kivyovyote!atumie nyama ya ulimi kurekebisha!

Huyu jamaa ndondocha nini.. yani analea watoto wa wanaume wengine wakwake anawaacha... Embu aachane nae alee watoto wake...
 
kabla hajachukua hatua azingatie historia. siku hizi historia ni mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo. pia asisahau kuwa historia ina kawaida ya kujirudia.
 
ukimwi hawana wako fiti labda ndio maana kila mm1 anajidai!
huyu:nitaoa, yule: naondoka.

kama kuna mmoja hatakio basi asikilizwe, period. Hiari ndiyo msingi wa yote kwenye mahusiano.
 
Back
Top Bottom