Jamani nathubutu kusema kwa dhati kuwa kwa wale wenye majini, dawa ni hii hapa! Sidanganyi..

Status
Not open for further replies.

Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
0
Nilikuwa na jini Maimuna ananisumbua muda mrefu hadi nilikondeana sana. Huyu jini alinitia magonjwa ya ajabu na upele mwili mzima. Nilikwenda hospitali na kumeza dawa lakini wapi! Nikapata msaada wa Sheikh lakini wala sikupata unafuu wowote. Mgongoni mwangu nilijisikia kama nimebeba mzigo mzito sana mithili ya gunia la mchanga kilo 50. Ilikuwa vigumu kwangu kupata usingizi wakati wa usiku.

Wakati mwingine huyu jini alinilazimisha nimpe mapenzi ya ovyo ovyo kila wakati kiasi kwamba sikuwa na uwezo tena wa kumridhisha mke wangu kimapenzi. Sikujua nifanye nini hadi pale nilipomtembelea rafiki yangu mmoja (sitaki kumtaja hapa) na kumkuta anakula ugali kwa kiti moto. Alinikaribisha chakula. Nilisita lakini kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaamua kula walau kidogo.

Nilipoonja tu nyama ile niliipenda na ilikuwa tamu sana. Ghafla nilijisikia mwilini mwangu kama vile nimepigwa shoti ya umeme na kisha kumwagiwa maji ya baridi mwili mzima. Ni kana kwamba ule mzigo mzito niliokuwa nao mgongoni mwangu ulikuwa umeshushwa na nilijisikia mwepesi sana. Sikumwambia chochote rafiki yangu. Baada ya chakula na maongezi tuliagana. Siku iliyofuata niliamua kwenda kuinunua ile nyama na kuitumia. Nilisikia mizigo mingine ikiendelea kuporomoka kutoka mwilini mwangu.

Hadithi ni ndefu wandugu lakini kwa kifupi ni kwamba napata usingizi vizuri sana kwa sasa na mke wangu namfurahia sana kimapenzi hadi kila wakati ananiuliza kulikoni! Hakika hiki kitoweo ndicho chenyewe. Huyo jini amekimbia bila kuaga. Kila mwezi nakamata kitimoto hadi nina kitambi, kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa vile mwili wangu ulikuwa kimbaombao na afya ya mgogoro. Siwezi kuthibitisha kwa 100% kuwa hii ni dawa kwa kila mtu, lakini kwa wale mlio na shida kama niliyokuwa nayo, hebu jaribuni! Najua wengine watanipinga na kunitukana lakini habari ndo hiyo!


 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,080
2,000
@gani salum Tatizo hulikuwa hutaki Lupita papuchi ya jijini....
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,080
2,000
Hajisalum Tatizo hulikuwa hutaki Lupita papuchi ya jijini....
 
Last edited by a moderator:

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
13,159
2,000
Pole sana. Ukweli majini na kitimoto ni maadui wakubwa na ndiyo maana wachawi na waganga wanaotumia majini au wadudu katika kuponya hawakai jirani na wafungaji wa huyu mbuzi. Kama unaweza chukua pia mfupa wa nguruwe chimbia kona za kuta za fence yako. Binadamu wengine ni wabaya na wazandiki bora kujikinga.
 

andate

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
2,653
2,000
hahahaha...
Kuna mmoja aliambiwa atumie nyama ya nguruwe ili majini yaache kumsumbua. basi majini yakawa yanakuja na nguruwe wao yanamla mbele yake yakishammaliza yanaanza kumtenda vilevile.
 

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,373
2,000
afazali umesema kweli maana wengine wanakula alafu wanakuja kumkashifu mnyama huku JF sasa uwe unashushia na castle ya baridiii...
 

uwoya

Senior Member
Oct 18, 2012
166
195
nilikuwa na jini maimuna ananisumbua muda mrefu hadi nilikondeana sana. Huyu jini alinitia magonjwa ya ajabu na upele mwili mzima. Nilikwenda hospitali na kumeza dawa lakini wapi! Nikapata msaada wa sheikh lakini wala sikupata unafuu wowote. Mgongoni mwangu nilijisikia kama nimebeba mzigo mzito sana mithili ya gunia la mchanga kilo 50. Ilikuwa vigumu kwngu kupata usingizi wakati wa usiku.

Wakati mwingine huyu jini alinilazimisha nimpe mapenzi ya ovyo ovyo kila wakati kiasi kwamba sikuwa na uwezo tena wa kumridhisha mke wangu kimapenzi. Sikujua nifanye nini hadi pale nilipomtembele rafiki yangu mmoja (sitaki kumtaja hapa) na kumkuta anakula ugali kwa kiti moto. Alinikaribisha chakula. Nilisita lakini kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaamua kula walau kidogo.

Nilipoonja tu nyama ile niliipenda na ilikuwa tamu sana. Ghafla nilijisikia mwilini mwangu kama vile nimepigwa shoti ya umeme na kisha kumwagiwa maji ya baridi mwili mzima. Ni kana kwamba ule mzigo mzito niliokuwa nao mgongoni mwangu ulikuwa umeshushwa na nilijisikia mwepesi sana. Sikumwambia chochote rafiki yangu... Baada ya chakula na maongezi tuliagana. Siku iliyofuata niliamua kwenda kuinunua ile nyama na kuitumia. Nilisikia mizigo mingine ikiendelea kuporomoka kutoka mwilini mwangu.

Hadithi ni ndefu wandugu lakini kwa kifupi ni kwamba napata usingizi vizuri sana kwa sasa na mke wangu namfurahia sana kimapenzi hadi kila wakati ananiuliza kulikoni! Hakika hiki kitoweo ndicho chenyewe. Huyo jini amekimbia bila kuaga. Kila mwezi nakamata kitimoto hadi nina kitambi, kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa vile mwili wangu ulikuwa kimbaombao na afya ya mgogoro. Siwezi kuthibitisha kwa 100% kuwa hii ni dawa kwa kila mtu, lakini kwa wale mlio na shida kama niliyokuwa nayo, hebu jaribuni! Najua wengine watanipinga na kunitukana lakini habari ndo hiyo!

kitimoto kiasaidia kwa masaa. Baadaye atarudi. Dawa ni jina la yesu-tina hakuna gharama
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,712
1,225
Akuna kitu sipendi kama Mashetani!
Sema sina uhakika kama kweli kiti moto inatibu!
 

kajirita

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
1,575
1,225
Yaani wewe ndo umegundua leo?

Hata kama umehamia kwenye nyumba ya kupanga ambayo unahofu ya uwepo wa majini,ukichukua mfupa wa kitimoto tu ukauweka ndani ya nyumba majini yote yanakimbia!

Ila angalia usiwe unaishi na mwenye nyumba ' mfugaji' wa majini kwenye nyumba moja ,maana kesho yake utapewa notisi kwa kumfukuzia mifugo yake!

Huo ni ukweli hiyo ni dawa tosha!!
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,516
2,000
Tupeleke kitimoto bungeni tuondoe majini yaliyoikalia ccm mgomgoni na spika Anna yawaachie wawe wasikivu na kuondoa Tabaka LA ubaguzi na kutetea wafilisi nchi.
 

Daata

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
4,516
2,000
Dawa nzuri imetangazwa kwa wale wenye majini.....kitimoto ndio dawa
 

Chen Hu Xiansheng

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
3,050
2,000
Kuna jamaa alikuwa na majini na yeye akaambiwa ale kitimoto, cha ajabu baada ya kula chair fire, yale majini yakasema yanamshukuru sana kwa msaada na kama hatojali, yanaomba ayaongezee na banana baridi. Alichokah!
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom