Haji Salum
JF-Expert Member
- Nov 27, 2013
- 1,022
- 394
Nilikuwa na jini Maimuna ananisumbua muda mrefu hadi nilikondeana sana. Huyu jini alinitia magonjwa ya ajabu na upele mwili mzima. Nilikwenda hospitali na kumeza dawa lakini wapi! Nikapata msaada wa Sheikh lakini wala sikupata unafuu wowote. Mgongoni mwangu nilijisikia kama nimebeba mzigo mzito sana mithili ya gunia la mchanga kilo 50. Ilikuwa vigumu kwangu kupata usingizi wakati wa usiku.
Wakati mwingine huyu jini alinilazimisha nimpe mapenzi ya ovyo ovyo kila wakati kiasi kwamba sikuwa na uwezo tena wa kumridhisha mke wangu kimapenzi. Sikujua nifanye nini hadi pale nilipomtembelea rafiki yangu mmoja (sitaki kumtaja hapa) na kumkuta anakula ugali kwa kiti moto. Alinikaribisha chakula. Nilisita lakini kwa kuwa nilikuwa na njaa nikaamua kula walau kidogo.
Nilipoonja tu nyama ile niliipenda na ilikuwa tamu sana. Ghafla nilijisikia mwilini mwangu kama vile nimepigwa shoti ya umeme na kisha kumwagiwa maji ya baridi mwili mzima. Ni kana kwamba ule mzigo mzito niliokuwa nao mgongoni mwangu ulikuwa umeshushwa na nilijisikia mwepesi sana. Sikumwambia chochote rafiki yangu. Baada ya chakula na maongezi tuliagana. Siku iliyofuata niliamua kwenda kuinunua ile nyama na kuitumia. Nilisikia mizigo mingine ikiendelea kuporomoka kutoka mwilini mwangu.
Hadithi ni ndefu wandugu lakini kwa kifupi ni kwamba napata usingizi vizuri sana kwa sasa na mke wangu namfurahia sana kimapenzi hadi kila wakati ananiuliza kulikoni! Hakika hiki kitoweo ndicho chenyewe. Huyo jini amekimbia bila kuaga. Kila mwezi nakamata kitimoto hadi nina kitambi, kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwa vile mwili wangu ulikuwa kimbaombao na afya ya mgogoro. Siwezi kuthibitisha kwa 100% kuwa hii ni dawa kwa kila mtu, lakini kwa wale mlio na shida kama niliyokuwa nayo, hebu jaribuni! Najua wengine watanipinga na kunitukana lakini habari ndo hiyo!