Jamani nani kaniroga?

Jamani nani kaniroga?

Tatizo lako una'pretend' kaka watu wanakuona una pesa nyingi tofauti na kipato chako. Ishi maisha ya kawaida usijionyeshe kabisa kama una pesa hata kama unazo,na siku moja moja wakope na wao,utaona kama watakufatafuata
 
Nimekuwa na maisha magumu kwa huruma . Nafanya kazi ila mshahara wangu wanaishia kufaidi ndugu zangu na watu wengine.

Ndugu zangu wamekuwa kila wakati watu wa kunililia shida tu na zote zinaishia kuhitaji hela na shida huongezeka zikikaribia tarehe za mwisho wa mwezi nami nimeshindwa namna ya kuachana nao japo mshahara wangu ni mdogo

Nilijaribu kubadili namba ya simu nikajikuta nakuwa mpweke sipati msg wala mtu wa kunibeep nikajikuta narudisha line ya zamani.

Kibaya zaidi mimi nikikutana na mtu hata nisie mfahamu akinililia shida hata kama sina kitu mfukoni najikuta nimeenda hata kukopa ili kutatua tatizo lake nabaki kulipa madeni

Huwezi amini kuna siku naishiwa hela kiasi cha kuishi kwa mlo mmoja hata wakati mwingine kukoswa nauli ya kazini naamua kukatiza kwa mguu kariakoo kimara ila kesho yake nikipata hela mtindo ni huo huo

Jamani basi alieniroga aniache imetosha basi maana hii si huruma tena aniachie walau nifanye kitu cha maendeleo kunisaidia la kesho. Ushauri wenu wana jf
mshukuru Mungu kwa kila jambo
 
Usikionee huruma kiumbbe uschokizaa......... Siku ukifa masikin watakuwa wa kwanza kusema ulikuwa unapenda starehe ndio maana huna maendeleo kaz kwako
 
pole, fadhile mpe mbuzi utakula mchuzi kuliko binadam atakuudhi.
 
Mkuu nahisi una blood group 0+ (born to help) hujarogwa hayo ndo maisha yako na hutabadilika jaribu tu kukubaliana na hali hiyo
 
Polee

Tatizo ni wewe mwenyewe umewazoesha... huna budjet?
 
Kitabu kinasema usisumbukie ya dunia kwa maana yanapita tu!!!!!!!!!!!!!!!!1. Endelea na moyo huohuo ndugu yangu maana akiba yako mbinguni inaongezeka. Tukifika mbingu we unaweza jikuta ndio tajiri kuliko wooote. Ameeeni
 
Hujarogwa ndo maana unatambua hilo cha msingi ni kuchua maamuzi magumu kwa kupunguza misaada
 
Back
Top Bottom