Jamani nani anaushahidi kuhusu promotion za voda?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,444
8,239
Mimi aingii akilini kama hizi promotion ni zaukweli au magumashi nani mwenye rafiki au jamaa aliyeshinda Hyunda 100e,??mimi sijasikia kama kuna mtu aliyepata gari hizo zilizokuwa 100!je kweli kati ya hizo hakuna mwenye jamaa yake?Na hizi Tv za samsung?100Nani unamjua kapata?Mimi nawasiwasi kama kweli wanaendesha mashindano ya ukweli kama awaibii watu!!
 

OMGHAKA

Member
Aug 15, 2011
97
23
Ila kuanzia leo airtel bei juu kwa zaidi ya 50%, kuthibitisha check mara utapopiga sim
 

OMGHAKA

Member
Aug 15, 2011
97
23
Ongezeko la leo linafanya airtel kuwa ndio mtandao wenye ghalama kubwa kuliko wowote tanzania.
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,444
8,239
Hii mitandao yote niwezi wakubwa sana mfano ni hii ukipiga unalipa ushuru,ukiweka airtime unalipa ushuru!kwamaana ukinunua voucher unalipia usshuru na ukiitumia ile voucherkupiga napenyewe unalipa!!
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,566
2,815
millioni kumi na moja za voda ni wizi mtupu....last week walimtangaza same person for like five concecutive days kuwa ndiye mshindi katika capital tv....two weeks back walimtangaza Gadna G Habash kuwa ndo mshindi......fu*k voda!...na mia tano hamsini zetu.
 

kinyoba

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
1,269
715
bora hao airtel wapandishe gharama kwa hiyo 50% waziwazi na watumiaji wanaelewa kuliko TIGO wanaodanganya watu eti shilingi moja kwa dakika wakati ni uongo tu. Ukiweka 500 tigo haizidi dakika 3 pesa imeisha. Tigo wahuni sana na wezi kuliko kitandao yote ya simu nchini
 

Jeji

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,975
367
hizi promotion za mitandao ya simu me huwa nawaona wazushi tu hawana lolote.
 

Michael Scofield

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
1,225
470
hizi promotion za mitandao ya simu me huwa nawaona wazushi tu hawana lolote.
Hawa voda mpaka leo mie siwaelewi, malipo yote yakatwa kwa sekunde lakini ukijiunga CHEKA TIME zao wanakukata kwa dakika, nashindwa kuwaelewa? sijui hawa wahusika wamelala au ndio nchi hii tunapelekwapelekwa tu watu hawakemewi.

Na hii tabia ya kupigiwa simu ili kusikiliza matangazo yao nayo inauzi kweli, pamoja na sms zao kila wakati kama una mitandao yote ndo presha kila wakati unajua kuna sms ya maana kumbe tigo au airtel au... usumbufu mtupu.
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,358
2,332
Mimi nadhani kuna kamchezo huwa kanafanyika na hao akina Gardiner walioshinda,inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliyewahi kunieleza kuwa alibebeshwa Dummy Cheque ya WESTERN UNION na kupigwa picha za magazetina TV kuwa ameshinda shindano lao na kuzawadiwa 5,000,000/= wakati kiukweli walimpa 1.5 M tu.ilimpa tabu kwa mkewe aliyeamini amechikichia fedha nyingine!..janja ya Nyani kwisa jua
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
mi nina ushahidi wa za tigo, rafiki zangu walipewa ushindi wa magumashi. walipewa millioni moja kila mtu ila walitakiwa warudishe laki tisa.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom