Jamani nakosea wapi?

Jamani nakosea wapi?

Ndugu WhatsApp namba ni ya kwake, ww uangalie na kusoma inakuhusu nini mpaka unaanza kufungua Internet.

Sasa nenda kaomba msamaah lakini tambua unaibiwa hapo.

Mapenzi ni hatari sana
Mimi niliwasha data kwa matumizi yangu mengne ya mtandao hayo ya whatsapp yamekuja tu baadae
 
Nimekuwa na huyu binti kwenye mahusiano takribani miezi sita siku zote amejionyesha kwangu ni mtu makini anayeheshimu misingi ya dini yake
Mwezi mmoja nyuma nilitembelea maeneo anayoishi huyu binti bila kumpa taarifa (yeye ni mwalimu hivyo anaishi nyumba za shuleni kwao) nilimkuta nje wapo na jamaa mmoja wanapiga story, nilivyofka kama alishtuka kidogo then akanikaribisha walipoketi kwa tabasamu huku akinitambulisha kwa jamaa kama kaka ake na amekuja kumtembelea, mm nilitambulishwa kama rafk tu na alimwambia ni jirani yetu so sikuona tatzo coz ni kweli hata kwao sijulikani, baada ya story kidogo mm nikawaacha
But last week niliibiwa simu pamoja na wallet yangu yenye vitambulisho so kutokana na kukosa vitambulisho zoezi la kurenew lilikuwa gumu kiasi ikabidi niazime simu yake kwa muda niendelee kutumia katika shughuli zangu
Nilipowasha data mida ya usiku message za whatsapp ziliingia kwa wingi na baadh niliweza kuzisoma kupitia notification bar ndipo nikaona message ya mapenzi toka kwa yule jamaa aliyemtambulisha ni kaka ake na kuangalia chat zao zaidi nikajiridhisha ni wapenz wa muda mrefu kabla hata ya mimi
Leo nimemtumia ujumbe nikamwambia "naona hukujiandaa au ulishindwa kujiandaa kabla ya kunipa simu" akashtuka akapiga nikamueleza hali ilivyo na niliyoyasoma kwenye chat zao
Cha ajabu mwenzangu amepanick na ameanza kutuma txt kuwa mimi sina shukrani kwa msaada wake pia nilikuwa namtafutia sababu ya kumwacha
Jamani wana Jf wenzangu naomba mnipe ushauri kama nimekosea maana sijafanya maamuzi yoyote zaidi ya kumwambia lakini tayari anaweweseka analia mara mm simu siitaki tena wakati mwanzoni alikuwa nimpe baada ya kurenew
Sema na moyo wako my friend
 
Pole mkuu

Chukua maamuzi mwenyewe sisi hatuwezi kukushauri chochote siku zote maamuzi yana wewe mwenyewe
 
Simu kasema haitaki tena...!! Uza mkuu ukanywe bia upoze machungu yakuchapiwa
 
Back
Top Bottom