Hay! waungwana marafiki zangu
Namshukuru Mungu kuniweka hata siku hii ya leo niko mzima buheri
wa afya njema, wengine hatunao leo hii kwanini mm ni nani mpaka
nikawepo, jamani? hiviyo sina budi kumshukuru Mungu hata wewe
rafiki yangu mpenzi wangu huna budi kumshukuru Mungu kila uionapo
leo.
Wapendwa wangu wa moyoni leo tena nimekuja na jambo hili ambalo
nimeonelea niliseme hapa kwenu ili tujadili na kupata ufumbuzi wa kina.
labda nianze kwa kuuliza swali hili hapa: samahani kama mtaboreka
wanaume wa humu mjengoni? ni hivi: hivi ni kwanini ninyi wanaume
mnakuwa vicheche na mnakuwa watu wa ajabu sana kuwatenda wake zenu?
Hamuoni kuwa mnasambaratisha ndoa zenu na kuleta mitafaruku ndani ya
ndoa na mgawanyikano kati ya kizazi na kizazi? Mkipenda kujibu haya kazi kwenu.
Jambo ambalo nimeona niliseme ni hili kwa upande wa wanaume ambao wamekuwa
vicheche hata kwangu imenitokea kwani nimejaziwa wanawake lukuki hata wengine
sijui majina hao hasa nimebaki naumia ndani kwa ndani nimemuomba kaka
Erickb52
asaidie jahazi hili linaingia majini kajitahidi kaka wa watu kunisaidia laikini wapi?
nimeona sasa ninyi marafiki zangu mnisaidie kwa huyu mtu kwani bado nampenda
na sitaki kumuacha kwani tuliahidiana mbele ya mashahidi kuwa
sisi tu mwili mmoja
na
Alichokiunganisha Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha, hivyo naendelea
kuvumilia tu japokuwa ni karaha na mateso ndani ya ndoa lakini bado naendelea kuwepo
tu msije sema kuwa mm ni king'ang'anizi lahasha wala ni ndoa lazima niijenge japokuwa
inayumba sana sasa, ugomvi, manyanyaso yamekuwa mengi, ingawaje ananipenda
naye hawezi nitamkia chochote kuhusu kutalikiana kwani bado ananipenda japokuwa
ananiletea wanawake humu home.
Juzi kati kwenye majira ya jioni tumekaa tunasubiri msosi akaniangalia na kunikodolea macho
kisha akasema mwenyewe kupitia kinywa chake "My love barafu wa moyo wangu
unataka nikufanyie nini ili uone nakupenda japokuwa
nimekuwa mtu nisiyemwaminifu? maneno
haya aliyatamka yeye mwenyewe kwani aliona anavyonifanyia na kunipa stress kila wakati
ingawaje nilishamwambia kuhusu tabia yake ya kicheche na kutamanni wanawake wa nje.
Nikamwangalia kwa macho maangavu na yenye mvuto wa mapenzi kisha nikamwambia
niletee au nipe chochote upendacho, mume wangu laaziz wangu
Mentor wa maisha
Akaniangalia na kusema kuwa
nitakununulia gari aina ya VITZ (sijui kama nimedanganywa hapa)
ila moyoni nilijawa na furaha na nilifurahia nikamrukia na kumpa kiss la agape, kwa furaha niliyonayo
japokuwa ..............bado ANANIPENDA jamani mpaka nikasahau machungu, manyanyaso yote hapa
nilipo nasubiri huo muujiza utendeke nipate kufurahi na kuwa mwenye kicheko ndani ya ndoa yangu
waungwana je mmelionaje hili?
Nawatakia siku njema na kazi njema