Kama uwezi kutunza siri ya nywila (password),basi ushauri ni kutumia nywila moja au zisizo zidi tatu...!Habarini,
Ukubwa ni jalala jamani.
Sasa hivi nimegundua nina vitu vingi sana nashindwa kuvimanage. Mfano nina password za bank 3 tofauti, jamii forums, yahoo, hotmail, Vodacom Mpesa, facebook....nakadhalika.
Juzi nahitaji mtumia mtu pesa kwa M-pesa ya voda nimesahau pin no yangu siwezi kumtumia.....
Wakuu huwa haya ma-password munaya-manage vp? Je munakua na password moja kwa mambo yote yahitajiyo password? Na hii naiona ni risk au ?!....
Hem sheeeni ujuvi hapa
Ziandike hizo password sehemu na uzifunge kwa "password" ili mtu mwingine asiweze ku-access...lol :teeth:
Kama uwezi kutunza siri ya nywila (password),basi ushauri ni kutumia nywila moja au zisizo zidi tatu...!
Nywila ya kwanza ni kwa ajili ya yanayo husu simu, namba mbili ni kwa ajili ya social network kama JF, Facebook a twitter, namba tatu ni kwa ajili ya kusoma email zako kwenye hotmail au yahoo.
Binafsi ninazo nywila kumi tofauti tofauti, na ninazikumbuka zote...!
Siku ya kusahau jina la mama watoto wako (kama unaye) ndio utatia akili.Habarini,
Ukubwa ni jalala jamani.
Sasa hivi nimegundua nina vitu vingi sana nashindwa kuvimanage. Mfano nina password za bank 3 tofauti, jamii forums, yahoo, hotmail, Vodacom Mpesa, facebook....nakadhalika....