Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,851
Hii imemtokea rafiki yangu kipenzi, Jana aliniomba nimsindikize Lenana Hotel jioni akisema kuwa kuna binti kampenda sana sasa anataka amweleze intention yake ya kumuoa, mimi nikamsindikiza, kufika Lenana Hotel baada ya dakika kama 20 binti akafika, ukimwangalia kwa haraka haraka atakuwa na umri wa miaka 21-25 hivi, basi, tukasalimiana pale, mazungumzo ya kuchumbiana yakaanza, kilichonistua zaidi ni hili, katika kuulizana maswali ya hapa na pale mfano, unafanya kazi gani, umri wako, kwenu mpo wangapi, wazazi wako wapo, unasali dhehebu gani, nk. ndipo yule binti akauliza wewe ni chama gani? duuu!! ikabidi nimuwahi kwa kumuuliza swali, chama una maana gani? akasema, Chama cha siasa, Bahati nzuri yule rafiki yangu akasema hana chama ila ni mshabiki wa vyama tu! binti akasema yeye alitaka kufahamu tu!!
Sasa nauliza, hivi siku hizi mkichumbiana ni lazima hili swali umuulize mwenzio? na nafasi ya hili swali katika mahusiano ni ipi?
Hahahahah dah binti alikua anahofia asije kulamba magwanda,maana ni washari sana!
acha uongo mkuu, ina maana ulikaa nao meza moja wakati wakit.ongozana?
Una akili fupi mnoo...jaribu kuirefusha
Una akili fupi mnoo...jaribu kuirefusha
huyo dada anohofia kuwa na bwana kutoka ccm
Sio kutongozana mkuu, kuchumbiana, jamaa aliniambia nimsindikize, sasa wakati wanazungumza mimi nilikuwa na kinywaji changu najifanya kama vile sisikilizi kinachoendelea kumbe huku sikio moja liko pale kwao, na kumbuka katika issue ya kuchumbiana unaweza kumchukua rafiki au ndugu yako wa karibu ambaye hana tamaa akakusindikiza, hapa ni kuongeza nguvu tu mkuu.

Umeona eee sijui alikuwa anamaanisha CCM au CHADEMA au CUF?