Tatizo letu bongo tuna copy sana halafu hatuwezi kufikia viwango. MAISHA PLUS ni idea ya BI BROTHER hiyo haipingiki mana kila kitu kinajionyesha tatizo Masoud na wenzake wamekurupuka kama wengine wanavyokurupuka katika maigizo ambayo wao wanayaita MUVIE? bongo hakuna MUVIE ni maigizo tu! Maisha plus wameshindwa kutonesha reality mana kauli mbiu yao ni kuonyesha maisha halisi ya kitanzania lakni ukijaribu kuangalia ni upumbavu tu. BIGBROTHER south africa wenzetu wanajiandaa kamera kibao zipo zilizofichwa ambazo washiriki hawazioni, pia mandhari ni poa. MAISHA PLUS ni wizi mtupu yani washiriki wanachukuliwa na kikamera cha birthday? ili waweze kuonyesha real life kamera zingefichwa ili washiriki wasiweze ku-act mana unaona kabisa kuwa washiriki wana-act kwasababu anachukuliwa live na mpiga picha kwahiyo pale lazima mshiriki aogope au ajilazimishe kuwa katika hali fulani. kwahiyo MAISHA PLUS ni wizi mtupu sijaona chochote ni mradi tu wamebuni wakuwaweka town. location mbaya, me sijaona kijiji pale sijui wengine wanaweza kunishawishi pale ni kijijini au? 😕🙄