Jamani kuna ukweli!

MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,318
6,391
f1d662247d94324562a725900587987b.jpg
 
Nchi hii inakigeu geu.. Mara watangaze SOKO HURIYA!!..MARA WAKARIBISHE WAWEKEZAJI..mara wafute mikataba..mara warambe matapishi yao!!
 
mi sioni mantiki ya kuwazibia wawekezaji wa shule hizi. mbona shule zipo za bei tofauti nyingi, unaangalia pa uwezo wako
 
Kaka MANI ni kweli kabisa kabisa pale bei zao ni za kufa mtu, na watoto wao hawavai uniform aisee, hizo nguo zinazovaliwa pale hahahahahaa, ada zao zinachezea hapo kwenye $13,000 na ile French school wao wanalipa kwa Pound, ada ya chini kabisa ni Pound 800.

Ila wanapata kila kitu aiseee, wana safari za kufa mtu ambazo zinawapa exposure ya kutosha na mazagazaga mengine, sasa sisi tumefuta michango kwa kuiga tu matokeo yake shule hazina hata senti tano ya mlinzi au ya walimu wa kujitolea! I swear hii ya makufuli itakua ndio kaburi la elimu ya Tanzania
 
uwekezaji unatakiwa. ila kwenye taifa masikini kama tz na shule za milioni 30 kwa mwaka ni uhuni! wanaolipa hizo ndio ni pamoja na hao wanaoweka makontaina kwenye boksi la kibiriti na kuweka mfukoni mtu asione, tuimarishe elimu yetu na sio kuhesabu mamilioni na kulipa huku tunasifu wakati maraisi wote wliopita walisoma shule za kawaida!!, huyo anaelipia mtot milioni 30 kwa mwaka alisoma nvtc, dar tech,udsm bure!!!, mungu ibaraki tanzania (ya 1961-1985) pia tanzania ya sasa.....
 
Nyingi mmesha zoea za wazungu chakwako unakiponda
Mamilion ya WaTanzania tumesoma shule hizi hizi za serekali na tunaishi vizuri tu
Mpaka kuku awe wa (kitaira) kizungu ndio roho zenu zifurahi wakati kuku wetu watamu tu
 
Kaka MANI ni kweli kabisa kabisa pale bei zao ni za kufa mtu, na watoto wao hawavai uniform aisee, hizo nguo zinazovaliwa pale hahahahahaa, ada zao zinachezea hapo kwenye $13,000 na ile French school wao wanalipa kwa Pound, ada ya chini kabisa ni Pound 800.

Ila wanapata kila kitu aiseee, wana safari za kufa mtu ambazo zinawapa exposure ya kutosha na mazagazaga mengine, sasa sisi tumefuta michango kwa kuiga tu matokeo yake shule hazina hata senti tano ya mlinzi au ya walimu wa kujitolea! I swear hii ya makufuli itakua ndio kaburi la elimu ya Tanzania

Wanavaa Uniform.

Wiki mara moja, wanaruhusiwa kuvaa za kawaida.(Jumatano ).
 
Kama mnataka watoto wenu wakajifunze kivuta unga na bangi wapepekeni huko kwenye mamilioni
 
Kama mnataka watoto wenu wakajifunze kivuta unga na bangi wapepekeni huko kwenye mamilioni

Mbona wasela wengi tu wanavuta msuba. Mateja wapo kibao uswahilini. Wamesoma IST?

Hiyo ilikuwa sababu wazazi wasio na uwezo walikuwa wanawaambia watoto wao kuwapoza.

Somesha mtoto kwa uwezo wako, usishindane na jirani yako.
 
Back
Top Bottom