Jamani kuna ukweli katika hili jambo

Sgaga

Member
Sep 28, 2011
76
13
Hivi ni kweli kwamba binadamu huwa tunatokea kupenda mara moja tuu! katika maisha yetu na hatuwezi penda mwanamke/mwanaume kwa mara ya pili kwa kiwango kilekile?
 
Sio kweli, unaweza kumpenda kuliko yule wa mwanzo sababu kila mtu anakua na sifa zake mungu alizo mjaalia.
 
mie ninavyofahamu mtu ni mmoja tu, kama yule hakuna, unaweza ukakutana na wa kulingana nae, lakini kupenda unaweza kumpenda zaidi ya mara moja, sasa sijuwi ni mapenzi yale kutoka moyoni au vipi? mana hata cinema nyingi zinaonesha kupenda ni mara moja tu.
 
it's once in a life time.
Wengine ni kwamba lazima maisha yendelee.
 
kupenda ni mara 1 tu, mengine inabaki basi tu huna la kufanya. Na hii haina maana kuwa yule wa mwanzo ndo utaempenda saaannna, yawezekana ukawa umepita kwenye mahusiano tofauti bt ukaja kupenda kidhati kwenye uhusiano labda wa 3 au wa 5 na yakaja mahusiano mengine baada ya hapo bt pale ulipopenda kwa dhati penzi halibadiliki mpk utiwe kaburini. Hata hizi ndoa tunaingia tu lkn nyingi hakuna uwiano wa mapenzi kati ya mume na mke.
 
Hiyo sio kweli kabisa mimi mwenye nilimpenda mwanamke sana lakini baadae tukaachana nimempata mwengine yaani nampenda sana zaidi ya yule wa mwanzo na pesa kwao nishapeleka tena nashukuru kuachana na yule wa mwanzo kwani hamfikii kwa lolote huyu wa sasa
 
Hivi ni kweli kwamba binadamu huwa tunatokea kupenda mara moja tuu! katika maisha yetu na hatuwezi penda mwanamke/mwanaume kwa mara ya pili kwa kiwango kilekile?

Si kweli...tunaweza tukapenda zaidi ya mara moja!
 
Hiyo sio kweli kabisa mimi mwenye nilimpenda mwanamke sana lakini baadae tukaachana nimempata mwengine yaani nampenda sana zaidi ya yule wa mwanzo na pesa kwao nishapeleka tena nashukuru kuachana na yule wa mwanzo kwani hamfikii kwa lolote huyu wa sasa

Na huyo ukijakuachana nae utatuambia tena hivyo umempata mwingine ambae ni bora zaidi
 
Hiyo sio kweli kabisa mimi mwenye nilimpenda mwanamke sana lakini baadae tukaachana nimempata mwengine yaani nampenda sana zaidi ya yule wa mwanzo na pesa kwao nishapeleka tena nashukuru kuachana na yule wa mwanzo kwani hamfikii kwa lolote huyu wa sasa
So ths means hapa sasa ndo kwenye penzi la dhati
 
Mweka mada ungetueleza nini maana ya upendo na aina ya upendo unaosema kwanza
 
Hiyo ni kweli ila inategemea mahusiano yako na hao watu wawili yakoje!
 
Hivi ni kweli kwamba binadamu huwa tunatokea kupenda mara moja tuu! katika maisha yetu na hatuwezi penda mwanamke/mwanaume kwa mara ya pili kwa kiwango kilekile?

Ndio. Kupenda ni mara moja tu, japo si lazima awe wa kwanza au wa tatu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom