Jamani kuapply kazi serikalini na Masters ni kosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani kuapply kazi serikalini na Masters ni kosa?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by RISCA, Jun 26, 2012.

 1. R

  RISCA Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman nimeaapply sana tume ya ajira na Masters lakini nimeishia kutoswa kila,juzi hadi nimeapply nafasi ya afisa tarafa lakin najua nitapigwa chini tu.wenye uzoefu na serikalin naombeni msaada nini tatizo kama unaomba kazi kwa Masters? Note.. nafasi ninazoomba ni hizi za first degree za tume ya ajira.
   
 2. King2

  King2 JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikalini Wako Strictly wakisema Wanataka Degree basi wanachukua degree. Pia Mfano wakisema Mfano wanataka Administrative officer wanataka watu waliosoma degree ya Administration.
   
 3. R

  RISCA Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  basi imekula kwangu kaka
   
 4. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  pole
  sana
  kaka
  ndo
  maana
  sitaki
  kusoma
  masters
  kabla
  ya
  kupata
  ajira
  ya
  kudumu.
   
 5. R

  RISCA Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni mbaya sana kufanya Masters bila kuwa na experience ya kazi...mimi nimekwama kabisa nipo hoi sijui pakwenda kila sehemu nakataliwa
   
 6. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mdau mbona kazi za Masters zipo nyingi tu?Jaribu kuomba kazi za masters uone itakuwaje!
   
 7. R

  RISCA Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeomba nyingi tu sijafanikiwa.. and kwenye Goverment kazi za Masters ni zile kubwa zinaitaji uzoefu miaka mitano..na mimi sina experience niliunganisha from BA to MA.....so huwa sipotezi muda kuapply hizo kubwa kny Goverment
   
 8. T

  TUMY JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inategemea wao wanataka nini kaka, sio kosa wewe kuwa na masters ila kama nafasi inataka degree ya kwanza wanajua kabisa kukuweka wewe hapo na masters wakati wanakulipa mshahara wa mtu wa first degree sio sahihi, kama una masters basi omba ajira kwenye category inayotaka watu wa masters ili uweze lipwa sawa sawa na elimu yako pia.
   
 9. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Poa mdau!Usikate tamaa,mambo mazuri hayataki haraka wewe endelea tu kuapply lazima ipo siku mambo yatatulia!
   
 10. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Inshu sio kuwa na Masters kaka, inshu ni kujuana na watu. Ofisi zinazojali qualification sikuiz bongo zimebaki chache sana, nyingi wajali kwanza "U-Godfather", afu ndo wanaangalia Quali, tafuta Taita mmoja town hapo akushike mkono
   
 11. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ushauri japo utaona kama natania,
  Tumia BA kuomba kazi, CV yako pia ionyeshe kwamba una BA,habari ya MA ni siri yako. Ukishapata kazi, ndipo utaendelea kutafuta kazi ya MA na atleast utakuwa na angalao experience ya kazi. Pia kuwa na kazi itakuondolea pressure au stress, hivyo utaaply kazi na utapata kazi nzuri tu.

  Ni vema ukazingatia mahitaji ya kazi (qualifications). Kama wanahitaji BA , peleka BA, kama MA pereka MA, na kama una Diploma na ndiyo mahitaji ya kazi, peleka Diploma. Pia CV siyo Static object, CV ni dynamic always. CV inaandikwa kulingana na mahitaji ya kazi yenyewe. Nafahamu utaniona mwehu kukuambia uombe kazi ya Diploma wakati una MA, lkn nakuambia kitu ambacho itakusaidia sana na ipo siku utanitumia likekwasababu ya hiki ninachokuambia leo.

  Ni mara 1000 kuwa kazi ambayo inakupa uhakika wa kuishi kwanza, pia inayokupa uzoefu kuliko kukaa kijiweni au tegemezi au ombaomba huku ukisubiri kazi ya MA au BA au PhD. pia naomba nikufahamishe kitu tena hapa, kwamba hata hiyo MA ukikaa nayo bila kufanya kazi yoyote pia haitakusaidia kabisa, kwani waajiri watagundua kwamba elimu uliyo nyo ni HARD SKILLS (Elimu Vyeti) lkn hauna SOFT SKILLS ambyo ndiyo inahitajika kwenye Industry.

  Ushauri wa Mwisho,
  Omba kazi ya kufundisha hata part-time kwenye Private schools ili ikupe exposure na experience na uhakika wa kuishi. Hata kama hiyo shule inahitaji BA, just go for that na I can assure you kwamba with time utakuwa huna pressure na stress na utakuwa unaendelea kutafuta kazi unayohitaji. Na ukienda kwenye Interview,utakuwa na basics atleast za kuonyesha kwamba you have both hard and soft skills. Katika hili la private schools, usikae ukasubiri watangaze kwenye vyombo vya habari tu, hapana wewe fanya yafuatayo:
  1. Tambua shule za secondary za private katika eneo husika (eneo husika namaanisha kama uko Dsm au Arusha, n.k) kwa kuzingatia wapi unaishi, n.k
  2. Baada ya kutambua hizo shule, panga siku uanze kwenda shule moja moja ukiwa na CV yako na omba kuonana na HR au mkuu wa Shule. Kwenye Reception usiseme unatafuata kazi, kwani walinzi watakurudisha.Wewe sema kuna ndugu yako anataka kusoma, hivyo kuna taarifa muhimu unahitaji kutoka kwa Mkuu wa shule. Ukishaingia, wewe utaanza kuongea naye na uonyeshe kwamba you really have soft skills plus hard skills.
  3. Pia kumbuka kuvaa nadhifu. Hachana na ujana wa kuvaa mitepesho mara Jeans mara T-shirt wakati unaenda kutafuta kazi inayohitaji unadhifu. Hili ni la muhimu, kwani muonekeno wako unaakisi tabia na utendaji wako (japo si mara zote), lkn waajiri wengi wanaangalia muonekano wako wa nje kama unauza?
  4. Hata kama atakuambia kwamba kwa wakati huo hakuna nafasi, lkn mwambie kwamba unaweza ukamuachia CV yako ili nafasi ikitokea basi aweze kuwasiliana na wewe. Pia wkt unaongea naye, zingatia kwamba muda ni pesa, hivyo ongea direct why you are there. Usije anza kuzunguka kama unatongoza vile katika enzi za babu na baba zetu, kwani kizazi cha sasa hivi cha dot.com nao hawana meanders sana siku hizi wanapotongoza. Lkn katika hilo la kusema shida yako, pia jitahidi uwe short, accuracy, and precise.
  5. Muda umeniishia na kesho nina mkutano.

  NB: Inaweza ikakuchukua muda na ukawa dissapointed,lkn kwa Imani yako mwombe huyo unayemtegemea ili akufunulie njia. Mimi kwa Imani yangu ya UKRISTO, basi ningesoma mafungu haya kila siku, asubuhi kabla sijaondoka kwenda kutafuta kazi, au kuomba kazi na kila siku jioni kabla sijalala. Isaya 41:10, Mathayo 7:7-8, I Yohana 1: 9 na I Yohana 5:14-15.

  Ukizingatia hayo pamoja na hapo kwenye NB, basi AMINI kwamba kazi unayo na Mungu akubariki.
  TELO.
   
 12. R

  RISCA Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh thanks much kwa ushauri wako.nice one..nitayafanyia kazi yote hayo muhimu.thanks more
   
 13. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  mkuu nakupongeza sana, big up!
   
 14. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu pole sana! unajua professional ipo kwenye first degree na ndiyo elimu ya juu katika ku-apply kazi hapa Tz, Masters ni added advantage tu. Tafuta kazi kwa BA ukishapata ndio uanze kutafuta hizo za MA. Infact serikalini elimu kubwa siyo deal !!!! watu wenye diploma wana maisha mazuri kuliko wenye degree.
   
 15. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  is this the way we should raise our society?
   
 16. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  usitumie cheti cha Masters bro, kifiche kwanza ukishaingia utakionesha
   
 17. M

  Mudamali Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo neno mkuu
   
 18. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mkuu natumia simu hapa , Hamna hata kitufe cha LiKE najaribu kufikiria kama mtu unaweza kutumia muda wako kumshauri binadamu mwenzako mambo ya maana kama haya, then u r such a valuable man in our society...
   
 19. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Usijali ndugu, uwe na amani tu na ninashukuru kwa appreciation yako. Kila la kheri.
   
 20. Davich

  Davich Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani watu mnapo ingiza mambo ya imani katika swala la Ukweli kama la ajira inaudhi sana.Kwa sababu mnakuwa mnamaanisha kuwa mtu akisali na kukosa kazi ambayo ana meet all requirements amlaumu MUNGU.Hebukuweni na imani za kweli na endelezeni ukweli wa mambo kwani mnakuwa mnapotosha sana watu.Hadi mnataka watu wakasome vifungu wakati kazi inatangazwa wanakuwa washajua wanampa nani.Niwakati wa kuishi Ulimwengu wa kweli na imani itumike ipasavyo.
   
Loading...