Jamani kuapply kazi serikalini na Masters ni kosa?

tueleze una BA ktk field ipi au masters katika field ipi, mbona kazini kwangu mnahitajika tu, sema field yako kaka wote tulihangaika kama wewe lkn tulipata
 
field ya administration kote BA na MA.....Highest level Masters in Business Administration (MBA)......
 
Ushauri japo utaona kama natania,
Tumia BA kuomba kazi, CV yako pia ionyeshe kwamba una BA,habari ya MA ni siri yako. Ukishapata kazi, ndipo utaendelea kutafuta kazi ya MA na atleast utakuwa na angalao experience ya kazi. Pia kuwa na kazi itakuondolea pressure au stress, hivyo utaaply kazi na utapata kazi nzuri tu.

Ni vema ukazingatia mahitaji ya kazi (qualifications). Kama wanahitaji BA , peleka BA, kama MA pereka MA, na kama una Diploma na ndiyo mahitaji ya kazi, peleka Diploma. Pia CV siyo Static object, CV ni dynamic always. CV inaandikwa kulingana na mahitaji ya kazi yenyewe. Nafahamu utaniona mwehu kukuambia uombe kazi ya Diploma wakati una MA, lkn nakuambia kitu ambacho itakusaidia sana na ipo siku utanitumia likekwasababu ya hiki ninachokuambia leo.

Ni mara 1000 kuwa kazi ambayo inakupa uhakika wa kuishi kwanza, pia inayokupa uzoefu kuliko kukaa kijiweni au tegemezi au ombaomba huku ukisubiri kazi ya MA au BA au PhD. pia naomba nikufahamishe kitu tena hapa, kwamba hata hiyo MA ukikaa nayo bila kufanya kazi yoyote pia haitakusaidia kabisa, kwani waajiri watagundua kwamba elimu uliyo nyo ni HARD SKILLS (Elimu Vyeti) lkn hauna SOFT SKILLS ambyo ndiyo inahitajika kwenye Industry.

Ushauri wa Mwisho,
Omba kazi ya kufundisha hata part-time kwenye Private schools ili ikupe exposure na experience na uhakika wa kuishi. Hata kama hiyo shule inahitaji BA, just go for that na I can assure you kwamba with time utakuwa huna pressure na stress na utakuwa unaendelea kutafuta kazi unayohitaji. Na ukienda kwenye Interview,utakuwa na basics atleast za kuonyesha kwamba you have both hard and soft skills. Katika hili la private schools, usikae ukasubiri watangaze kwenye vyombo vya habari tu, hapana wewe fanya yafuatayo:
1. Tambua shule za secondary za private katika eneo husika (eneo husika namaanisha kama uko Dsm au Arusha, n.k) kwa kuzingatia wapi unaishi, n.k
2. Baada ya kutambua hizo shule, panga siku uanze kwenda shule moja moja ukiwa na CV yako na omba kuonana na HR au mkuu wa Shule. Kwenye Reception usiseme unatafuata kazi, kwani walinzi watakurudisha.Wewe sema kuna ndugu yako anataka kusoma, hivyo kuna taarifa muhimu unahitaji kutoka kwa Mkuu wa shule. Ukishaingia, wewe utaanza kuongea naye na uonyeshe kwamba you really have soft skills plus hard skills.
3. Pia kumbuka kuvaa nadhifu. Hachana na ujana wa kuvaa mitepesho mara Jeans mara T-shirt wakati unaenda kutafuta kazi inayohitaji unadhifu. Hili ni la muhimu, kwani muonekeno wako unaakisi tabia na utendaji wako (japo si mara zote), lkn waajiri wengi wanaangalia muonekano wako wa nje kama unauza?
4. Hata kama atakuambia kwamba kwa wakati huo hakuna nafasi, lkn mwambie kwamba unaweza ukamuachia CV yako ili nafasi ikitokea basi aweze kuwasiliana na wewe. Pia wkt unaongea naye, zingatia kwamba muda ni pesa, hivyo ongea direct why you are there. Usije anza kuzunguka kama unatongoza vile katika enzi za babu na baba zetu, kwani kizazi cha sasa hivi cha dot.com nao hawana meanders sana siku hizi wanapotongoza. Lkn katika hilo la kusema shida yako, pia jitahidi uwe short, accuracy, and precise.
5. Muda umeniishia na kesho nina mkutano.

NB: Inaweza ikakuchukua muda na ukawa dissapointed,lkn kwa Imani yako mwombe huyo unayemtegemea ili akufunulie njia. Mimi kwa Imani yangu ya UKRISTO, basi ningesoma mafungu haya kila siku, asubuhi kabla sijaondoka kwenda kutafuta kazi, au kuomba kazi na kila siku jioni kabla sijalala. Isaya 41:10, Mathayo 7:7-8, I Yohana 1: 9 na I Yohana 5:14-15.

Ukizingatia hayo pamoja na hapo kwenye NB, basi AMINI kwamba kazi unayo na Mungu akubariki.
TELO.

To be honest this is one of the best reply I ever seen since I join jamii forums,

I wish one day senetor aje kujibu watu hivi jamvini na siku hiyo nitajitoa MMU na chit chat na kuamia jukwaa la siasa
 
  • Thanks
Reactions: SG8

Thank you very much for your appreciation and acknowledgement.
 
My view:You are one of the great thinker in this Forum!!!
God bless You..
2TIMOTHY 4:22 (NIV)
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Nami nichangie hivi,karibuni nimeona application ya kijana amemaliza Mzumbe University-MPA na pia ana BA-ADMINISTRATION.Ofisini kwangu alihitajika mtu wa HR.Watu wengi waliomba hiyo nafasi lakini mapungufu mengi nitayatolea kwa huyo kijana aliye na MPA katika mazingira yafuatayo.
1.Application letter yake ilikuwa mojawapo ya mbovu kabisa.Aliandika kwa mkono na mwandiko wenyewe ni kama vile akusoma darasa la pili.Ni vema barua ya maombi ikachapwa kwa computer isipokuwa kama ni SHARTI iandikwe kwa mkono.
2.CV yake ilikuwa shallow sana.Hivi mara nyingi wanafunzi wanakwenda kwenye intership-kwa nini mnatafuta kazi hata kama hujaajiriwa kulemba sehemu na kuipa nguvu inayostahili na kuonyesha kazi ulizofanya.Wakenya ni wazuri sana katika kutengeneza sehemu hizo hata kama hajawahi kufanya kazi na hana experience ya kutosha ataonyesha na ukijichanganya kumwita kwenye interview inakula kwako.
3.Nashauri andika cv yake kama inayoishi siyo kama imekufa.Onyesha kama hata unajitolea kufanya kazi kulingana na elimu yako kwenya shirika la kibiashara au NGO.NGO ni nyingi sana siku hizi jiattach kwenye mojawapo na utapata mafanikio.
4.Watafuta kazi hasa wasasa hawana exposure na curiosity.Jitahidini pia unajiweka vizuri na job description na job summary.
5.Vyuo vingi vimeendelea kuchemka kushindwa kuwekeza kwenye idara za students career counseling kuwapa wanafunzi upeo mpana juu ya job opportunities kwa miaka inakuja.
 
Jaman nimeaapply sana tume ya ajira na Masters lakini nimeishia kutoswa kila,juzi hadi nimeapply nafasi ya afisa tarafa lakin najua nitapigwa chini tu.wenye uzoefu
na serikalin naombeni msaada nini tatizo kama unaomba kazi kwa Masters? Note.. nafasi ninazoomba ni hizi za first degree za tume ya ajira.

Apply kwa kutumia shahada yako ya kwanza..unaweza kufanikiwa
 
Back
Top Bottom