Jamani, katika hili JK apongezwe!!

Jamani, katika hili JK apongezwe!!

Jamii forum is in TRANSITION PERIOD. THERE IS A CONTRARY BETWEEN RESPONSIBILITY AND VOLUNTEERING THIS IS HIS RESPONSIBILITY AND HE CANT DESERVED THAT CONGRATS.

"WHEN I DO GOOD I FEEL GOOD AND WHEN I DO BAD IFEEL BAD AND THAT IS MY RELIGION" ABRAHAM LINCOLN.

he doesnt deserve the(any) congrats......
 
Alijua ni M23 wamevamia magogoni na angechelewa angebakia ukouko uhamishoni, huyu jamaa sijui kama atamaliza muda wake?
 
Mleta mada nina wasiwasi na elim yake, au ndo wale waliofutiwa matokeo nini?
Niliposoma kichwa cha habari sikutegemea kama ningekutana na utumbo kama huu, any way na yeye ndo thinking kapacity yake imeishia hapo.
 
Mkuu unaendelea kujichanganya hapa tunajadili siasa; kazi unafanya mpaka ushindwe kujihusiha na siasa? Siku mapadri; mashekhe wote tunao kwenye siasa; mkuu njaa yako sema nayo
Chama
Gongo la mboto DSM

chama mbona unakuwa na matatizo ya kufikiri jamani?ivi kwa nini unabadili mwelekeo wa mada?unapenda uchamb,uccm uchadema!utakupeleka wapi?ebu angalia michango ya watu timamu ujifunze ndugu...kuhusu kujihusisha na siasa sipingi ila kwa nini unamlazimisha lokisa akubali mawazo yako,eti mapadre,padre yupi anajihusisha na siasa?apa uctaje akina dr slaa kwa kuwa hawa upadre ulikoma zamani. Nasema ivi kwa kuwa kiukweli tupo wengi tusioruhusiwa kufanya siasa kutokana na kazi zetu ila tuna uhuru wa maoni. Gsana.
 
Hakika huu ni mfano mfu, yaani unadhani uchungu wa JK kwa wale waliokufa kwenye mlipuko wa bomu ni sawa na angefiwa na Riz1? Angekufa Riz1 hiyo ndege ingepiga riverse angani..! Utakuwa umesahau kuwa ''Damu ni nzito kuliko Maji''

Hata kama ni mfano mfu, mfufuka au hai, ujumbe umekufikia ndio maana umeweza kuandika hayo uliyoandika. Kwa kuwa Rais alirudi kabla ya muda wa kurudi, ni hakika kuwa alishtushwa na kusikitishwa na yale yaliyotokea. Kama una chuki binafisi na yeye ni wewe, sio lazima maono yako yawe yangu.
 
Tatizo lako chuki zinakusumbuwa inawezekana juu ya chama chake au dini yake au vyote viwili ila tumia akili sio kila kitu kupinga tu kama viongozi wako wa chama chako

Hamna chuki zozote, watu wanapenda amani ila wachache wanaipoteza na bado mpaka sasa kesi zake hazijatolewa maamuzi. Je tuendelee kupongezana wakati maafa yanaendelea kila kukicha? Tayari matukio mengi yametokea kipindi kifupi sana unategemea kesho kitatokea nini kama unataka tupongezana wakati hatujadhibiti matukio?
 
maandamano arusha watu walifariki hakusema kitu na aliendelea za ziara zake kama kawaida, siku ya hili tukio aliondoka nchini na baada ya kumaliza kikao ndiyo akakatisha tu kisehemu kidogo cha kitalii. ok labda kaambiwa arudi kunusuru chama
 
Mkuu Ritz
Hawa waganga njaa wa Chadema wanafurahisha sana hebu watueleze Mbowe alikuwa Dodoma; slaa alikuwa Dar wao walienda lini? Kikwete alikuwa maili nyingi tu nje ya nchi. Na isitoshe makamu na waziri mkuu ambao ni viongozi waandamizi walikwenda Arusha mara tu baada ya tukio sasa tatizo ni kitu gani? Waganga njaa hawa hawaakosi cha kuandika hata kama pumba wataandika ili mradi wakatiwe posho na mtaa wa Togo
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
chama mbona unakuwa na matatizo ya kufikiri jamani?ivi kwa nini unabadili mwelekeo wa mada?unapenda uchamb,uccm uchadema!utakupeleka wapi?ebu angalia michango ya watu timamu ujifunze ndugu...kuhusu kujihusisha na siasa sipingi ila kwa nini unamlazimisha lokisa akubali mawazo yako,eti mapadre,padre yupi anajihusisha na siasa?apa uctaje akina dr slaa kwa kuwa hawa upadre ulikoma zamani. Nasema ivi kwa kuwa kiukweli tupo wengi tusioruhusiwa kufanya siasa kutokana na kazi zetu ila tuna uhuru wa maoni. Gsana.
Hebu nionyeshe mwenye akili timamu kati yenu; nyote nyie ni waganga njaa. Mnaifanya server kujaa kwa kuandika pumba zenu;kama kazi haziwaruhusu kujiingiza kwenye siasa mnatafuta nini JF? Sio ndio maana nasema nyie niwanafiki waganga njaa; nyie tekelezeni majukumu yenu haya ya siasa hayawahusu.
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kilichonifuraisha kwenye mada hii ni kuwa wachangiaji wanabishana kwa hoja si matusi. Tofauti na id moja tu ya Isalia, waliobaki hongereni kwa michango mizuri kuanzia mleta mada. Hata kama hoja haikupendezi,kutukana si njia sahihi. Hongereni.

Nafurahia kupata changamoto na challenges nyingi tofauti tofauti lakini zikiwa na misingi ya hoja.
Nadhani huu ni ukomavu wa wana Jamvi.
Wapo wachache ambao kama si kuwa na kiwango duni cha elimu, kipato kidogo(wenye maisha tegemezi na kutokuwa na uhuru wa kimaamuzi) au pengine tuwaite wale walokunywa maji ya bendera za vyama vyao mpaka wakashindwa kujadiri hoja wakaishia ushabiki wa kivyama.
Mimi kama mleta mada huru pasipo fikra za itikadi yangu, nakiri nimejifunza kitu na kugundua uwezo wa kujenga hoja za msingi kutoka kwa wanajamvi.
Nimefarijika na simchukii mchangiaji yeyote hata wale walonikashifu kwa msukumo wa ushabiki wa vyama vyao.
Ahsanteni.
 
Ndg wanajamvi,

Kama ulivyo usemi wa wahenga wetu kuwa "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" Nijuzi baada ya mlipuko wa bomu kanisani huko Arusha, Rais Kikwete alikuwa ziarani nje ya nchi kama kawaida yake ya kutotulia nchini kwake lakini baada ya kutaarifiwa janga hilo la bomu, aliamua kukatisha ziara yake na kuacha malengo yake yote ya ziara hiyo na kurudi nyumbani kushirikiana na wananchi wake katika mkasa huo.

Kweli huo ni uzalendo na ninashauri vyombo vya habari viliweke wazi jambo hilo kwa watanzania kama vilivyokuwa vinaweka wazi pale marais waliomtangulia JK walipokuwa wanaendelea na mambo yao nje ya nchi wakati watanzania wanumia bila msaada. Mfano wakati wa mgomo wa madaktari muhimbili na wakati huo Raisi yuko majuu miaka ileeeeee!!!!

hovyooo hıı mbegu kaıpanda mwenywe sasa mavuno yake ndiyo haya halızanı anaıkomowa chadema.
 
" mshkaji yuko SAUZI hadi muda huu tunamuongelea, Mbayuwayu"
 
Hata kama ni mfano mfu, mfufuka au hai, ujumbe umekufikia ndio maana umeweza kuandika hayo uliyoandika. Kwa kuwa Rais alirudi kabla ya muda wa kurudi, ni hakika kuwa alishtushwa na kusikitishwa na yale yaliyotokea. Kama una chuki binafisi na yeye ni wewe, sio lazima maono yako yawe yangu.
Endelea kuamini kuwa aliahirisha ziara yake huko Kuwait, sisi tulioenda naye huko tunajua alimaliza visit yake ndo akageuza
 
Tatizo lako chuki zinakusumbuwa inawezekana juu ya chama chake au dini yake au vyote viwili ila tumia akili sio kila kitu kupinga tu kama viongozi wako wa chama chako

Kukukubali kila kitu pia si akili kama ilivyo viongozi wa chama chako na hata wabunge wa chama chako, kila kitu ndiyoooooooooo! Hata hoja ya kuliangamiza taifa!
 
Ndg wanajamvi,

Kama ulivyo usemi wa wahenga wetu kuwa "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" Nijuzi baada ya mlipuko wa bomu kanisani huko Arusha, Rais Kikwete alikuwa ziarani nje ya nchi kama kawaida yake ya kutotulia nchini kwake lakini baada ya kutaarifiwa janga hilo la bomu, aliamua kukatisha ziara yake na kuacha malengo yake yote ya ziara hiyo na kurudi nyumbani kushirikiana na wananchi wake katika mkasa huo.

Kweli huo ni uzalendo na ninashauri vyombo vya habari viliweke wazi jambo hilo kwa watanzania kama vilivyokuwa vinaweka wazi pale marais waliomtangulia JK walipokuwa wanaendelea na mambo yao nje ya nchi wakati watanzania wanumia bila msaada. Mfano wakati wa mgomo wa madaktari muhimbili na wakati huo Raisi yuko majuu miaka ileeeeee!!!!

Hivi we unaakili kweli! Apongezwe kwani kazuia bomu lisitupwe kanisani!! Kawaelekeza UWT wawe bize na Chadema huku nchi inavamiwa na magaidi!
 
Ndg wanajamvi,

................... "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" .................

Mkuu, tupe unyonge wa JK na haki unayotaka tumpe kwa unyonge huo. Kwa maoni yangu, huyu jamaa hatufai na haki yake ingefaa ajiuzuru ili nchi itawaliwe na watu wengine.
 
Hata kama ni mfano mfu, mfufuka au hai, ujumbe umekufikia ndio maana umeweza kuandika hayo uliyoandika. Kwa kuwa Rais alirudi kabla ya muda wa kurudi, ni hakika kuwa alishtushwa na kusikitishwa na yale yaliyotokea. Kama una chuki binafisi na yeye ni wewe, sio lazima maono yako yawe yangu.

Tukio linatokea yeye alikuwa anajiandaa kuondoka!alipofika anamaliza ziara ya siku 2 akasema amekatisha ziara!akarudi kuzuga faster akatimkia zake SA!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Kuwait City mchana wa leo, Jumapili, Mei 5, 2013, kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika Taifa la Kuwait kwa mwaliko wa Mfalme wa Kuwait, Amir Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al Sabah.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM

5 Mei, 2013

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, akifurahia jambo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kuwait Center for Autism Dr. Samira Al Saad mara baada ya bkusaini kitabu cha wageni baada ya kuwasiri kituoni hapo tarehe
6.5.2013.

Amueni wenyewe nani mkweli hapo kwani picha hiyo ya mama Kikwete ilichukuliwa tarehe 06/05/2013
 
Kukatiza ziara siyo issue,watutafutie wahalifu wote kuanzia waliompiga risasi Fr Ambrose,waliomuua Fr Mushy,waliochoma makanisa na waliofanya uhalifu wa kutupa bomu olasiti Arusha,wasiishie kula kodi zetu tu wakati tunapoteza maisha,Kwa taarifa yenu kabla ya lile tukio hakukuwa na ulinzi wowote zaidi ya askari trafiki wawili,muulizeni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae ni mkuu wa mkoa kwa nini hakukuwa na ulinzi wa kutosha wakati kulikuwa na ugeni mzito wa balozi wa papa.
 
Back
Top Bottom