Jamani, katika hili JK apongezwe!!

Jamani, katika hili JK apongezwe!!

Tatizo lako chuki zinakusumbuwa inawezekana juu ya chama chake au dini yake au vyote viwili ila tumia akili sio kila kitu kupinga tu kama viongozi wako wa chama chako

Na wewe tunaweza kusema vilevile kutumia maneno yako hayo hayo na kusema kwamba tatizo upendo wako kwake unakusumbuwa inawezekana juu ya chama chake au dini yake au vyote viwili ila tumia akili sio kila kitu kutetea tu kama viongozi wako wa chama chako
 
Hata wanafiki hupenda kuhudhuria misiba, japo ni ngumu kuwatambua. Jambo la msingi watu makini ni kuchukua maamuzi magumu ambayo wote watakuheshimu, wengi wanamcheze "RAIS WETU MSIKIVU" Sharubu. Eti kwakuwa ni msikivu.
 
Wana jamvi naomba tuwe watu wa kufikiri,
hivi ni nani kati yenu ambaye mtoto wake akiwa mla unga wa mda mrefu na baadae akaamua kucha asimpongeze?
Je mtoto akiwa mwizi na akaamua kuacha humpongezi?
Marais wa nchi hii hawakuwahi kufanya tendo alofanya JK la kurudi home kabla ya kukamilisha ratiba yake Kuwait, hata kama aliwahi lisaa limoja tu, bado ni element ya utafauti na watangulizi wake (isipokuwa Mwalimu) na kuonyesha mabadiriko kidogo.
Naomba nitambulike wazi kuwa mie sio muumini wa JK na wala hakuipata kura yangu na wala siutarajii u DC!!!

This to be considered pls!!!
 
Halafu kingine cha kushangaza siku ya nne leo tangu bomu lilipuke bado yuko kimyaaaa!!! Labda anasubiri mwisho wa mwezi ndio atoe zile hotuba zake fyongo.

Wacha urongo,

JK alikuwa na ziara ya siku 2 kuanzia jumapili hadi jumatatu. JK aliondoka nchini jumapili asubuhi, na huku nyuma bomu likalipuka. Ina maana wakati JK anatua Kuwait, Jumapili mchana alikuwa na taarifa. JK aliendelea na ziara yake hadi Jumatatu mchana ndipo akarudi. Kumbuka masaa ya Kuwait yapo sambamba na ya bongo... angekuwa anajali saana angegeuza ile ile jumapili...
 
Mkuu! Sema unatafuta kujua hisia za waTanzania katika hili. Hivi unakubaliana na wanao sema aliahirisha ziara yake? Ki diplomasia/ protokali nini maana ya ziara ya siku mbili nje ya nchi? Hata kama ulifika nchi ile saa moja jioni, ile ni siku ya kwanza. Na unaye mpongeza alitumia MA-USIKU MAWILI (2 NIGHTS) ambazo tayari ni siku mbili hata angeondoka asubuhi ya saa kumi na mbili. Ili mradi alihitaji kupewa huduma zote za kiitifaki na kidiplomasia. Na kwa taarifa ya ofisi yake, tuali tangaziwa kwamba ni ziara ya siku mbili. Hivyo huko mnaoita kuahirisha kunatoka wapi? Au ndio ule muendelezo kwamba "NYUMBA YA MUONGO HAIISHI VITUKO?"[/QU Upo sahihi sana mkuu in short hakuarisha bali alimaliza ziara kama inavyotakiwa... Bongo bana jambo liko wazi sema basi tuu siasa kila sehemu
 
Huwa nawashangaa sana wanaume wengine na huwa najiuliza hivi wakifunga zipu wanafungia nini humo ndani

Omba mkeo akathibitishe aje kukupa za kiitelijensia nini kimefungiwa!
 
alikatisha dinner, huo ndio uzalendo unaotaka tumpongeze nao?
bado una akili za panzi.
ziara ya JK ilikuwa ya siku 2 kuanzia tarehe 5 hadi 6, alirudi tarehe 6, sasa alikatiza wapi zaidi ya dinner?
Mie hata kwa bunduki siwezi kumpongeza maana yapo mengi yaliyotokea na hakufanya lolote na mengine yametokea akiwa njiani kuelekea airport wala hakuahirisha.
 
Wacha urongo,

JK alikuwa na ziara ya siku 2 kuanzia jumapili hadi jumatatu. JK aliondoka nchini jumapili asubuhi, na huku nyuma bomu likalipuka. Ina maana wakati JK anatua Kuwait, Jumapili mchana alikuwa na taarifa. JK aliendelea na ziara yake hadi Jumatatu mchana ndipo akarudi. Kumbuka masaa ya Kuwait yapo sambamba na ya bongo... angekuwa anajali saana angegeuza ile ile jumapili...
Asante tuko, tushaanza kilazimishwa kusifia mtu hapa,
 
Ndg wanajamvi,

Kama ulivyo usemi wa wahenga wetu kuwa "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" Nijuzi baada ya mlipuko wa bomu kanisani huko Arusha, Rais Kikwete alikuwa ziarani nje ya nchi kama kawaida yake ya kutotulia nchini kwake lakini baada ya kutaarifiwa janga hilo la bomu, aliamua kukatisha ziara yake na kuacha malengo yake yote ya ziara hiyo na kurudi nyumbani kushirikiana na wananchi wake katika mkasa huo.

Kweli huo ni uzalendo na ninashauri vyombo vya habari viliweke wazi jambo hilo kwa watanzania kama vilivyokuwa vinaweka wazi pale marais waliomtangulia JK walipokuwa wanaendelea na mambo yao nje ya nchi wakati watanzania wanumia bila msaada. Mfano wakati wa mgomo wa madaktari muhimbili na wakati huo Raisi yuko majuu miaka ileeeeee!!!!

niivi kaka, that is the president, ndivyo alivyopaswa kufanya na divyo anavyo takiwa ku react kwa maswla kama hayo. pongezi za nini sasa! uwezi kuwa raisi bila kuwa mzalendo wa nchi unayo tawala. for me no credit there ila nita mpa kama walio fanya tukio husika wame kamtwa na kufikishwa mahala husika. hizi pongezi kwa maswala ya siyo ya msingi ndo zimetufikishahapa

take example fro our parliament waziri anaulizwa swali ana jibu mipasho afu mbunge ana sema nampongeza mwheshimiwa waziri kwa majibu mazuri. tuache unafki mtuanapotimiza majukumu yake effectively hakuna haja ya pongezi bali anapo fanyazaidi yaile effectively kwa lengo la kuboresha tasnia fulani au jambo fulani, true we kan credit him but for this, hakuna haja ni responcibility yake kama president
 
wabongo noma.......... ki2 kidogo 2 ligi.:angry::teeth:
 
JK Alishamaliza ziara na hakuairisha kwa habari za ndani ni kwamba baada ya wasaidizi wake hususani wa habari kuona vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ikiwemo JF wamekosoa Rais kuwa yupo nje ya nchi na Wananchi wanalipuliwa mabomu hajali...wakaamua kutengeneza Press fasta kuwahadaa watanzania..kwani baada ya kurudi amefanya nini...
 
Ndg wanajamvi,

Kama ulivyo usemi wa wahenga wetu kuwa "mnyonge mnyongeni lakini haki take mpeni" Nijuzi baada ya mlipuko wa bomu kanisani huko Arusha, Rais Kikwete alikuwa ziarani nje ya nchi kama kawaida yake ya kutotulia nchini kwake lakini baada ya kutaarifiwa janga hilo la bomu, aliamua kukatisha ziara yake na kuacha malengo yake yote ya ziara hiyo na kurudi nyumbani kushirikiana na wananchi wake katika mkasa huo.

Kweli huo ni uzalendo na ninashauri vyombo vya habari viliweke wazi jambo hilo kwa watanzania kama vilivyokuwa vinaweka wazi pale marais waliomtangulia JK walipokuwa wanaendelea na mambo yao nje ya nchi wakati watanzania wanumia bila msaada. Mfano wakati wa mgomo wa madaktari muhimbili na wakati huo Raisi yuko majuu miaka ileeeeee!!!!

Sugu alisema kuna siku TUTAMPONGEZA RAISI HATA KWA KUNYWA CHAI...Sasa kwa ushauri wako nafikiri ndiko tunakoelekea mkuu...nini kipya hapo?????
 
Kwa taarfa ni kuwa JK alikuwa ameshamaliza ziara na HAKUAIRISHA ZIARA bali wasaidizi wake wakiwemo wa habari baada ya kuona magazeti,mitandao ya kijamii mfano JF wamekosoa kuwa Rais yupo nje ya chi anatanua na wananchi wanalipuliwa na mabomu kuwa hajali wakaamua kutengeneza Press fasta kuwa Rais ameairisha safari ili kuwahadaa watanzania...Watanzani wa 2013 si wa mwaka 1970 wameelimika na wanajua kutofautisha kati ya propaganda na news...lakini haya yana mwisho tutachoka saa na wakati usiojulikana watanzania wenye nia njema na nchi hii.
 
unatafta UDC kwa hawa guest 108 apo chini au uktaka udc au RC muone dogo si naskia anagawa ukshampa cash
 
MLETA HII MADA..unatafta UDC kwa hawa guest 108 apo chini au? uktaka udc au RC si naskia unamuona dogo si naskia anagawa ukshampa cash​
 
alikatisha dinner, huo ndio uzalendo unaotaka tumpongeze nao?
bado una akili za panzi.
ziara ya JK ilikuwa ya siku 2 kuanzia tarehe 5 hadi 6, alirudi tarehe 6, sasa alikatiza wapi zaidi ya dinner?
Nyie waganga njaa hamkosi cha kusema; kwani tatizo lilikuwa wapi? Serikali yote ilikuwepo Arusha na wote walitekeleza majukumu yao chini ya maelekezo ya Raisi mlitaka ajigeuze upepo?
Chama
Gongo la. Mboto DSM
 
Si kila anayevaa suruwali ni Mwanaume, na kuna tofauti kubwa kati ya Mwanamume na mtoto wa Kiume.
Afadhali mtoto wa kiume leo umelielewa hilo
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom