Jamani kama Intellectuals hebu tuweke ushabiki pembeni, tujadili haya madai ya madereva wetu

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,520
10,432
Hivi mi nauliza jamani haya madai ya madereva wetu ni sahii kung'ang'ana na serikali badala ya waajiri wao? madai yao ya msingi ni haya hapa;
1. kufuta kusoma kila lesen inapo-expire (hili limeishafutwa tayari)

2. madai ya mikataba bora ya kazi

3. posho za safari

4. mishahara inayokidhi malipo ya pango

5. bima (nadhani hapa wanamaanisha bima ya afya)

6. nauli ya kazini kwa dereva

Ila yote tisa, kumi ni kwamba haya madai yao mwisho wa siku yatapandisha nauli za mabasi na dalala halafu watu wataanza tena kulalamika. Wote tunajua mfanyabiashara habebagi hasara, sisi abiria ndo tutabeba huo mzigo kwa kupandishiwa nauli
 
1.Bima inayoongelewa hapo si bima ya afya ni bima kazini
2. Serikali ni baba na wananchi ni watoto, hivyo serikali inapaswa kusimamia wananchi(madereva) wake na kuhakikisha wanapata maslahi yao kwa Serikali kuweka utaratibu wa kudumu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri dhidi ya madereva ili kuondoa kero zao.
Mfano wizara ya kazi inaweza kutengeneza mikataba huru ikawaamrisha wamiliki waifuate, nk.
 
kabla basi halijapewa leseni sumatra lazima ukatie comprehensive insurance na nakala ipelekwe sumatra bima hiyo inakinga gari dereva na abiria wanapodai bima hapa kuna tatizo limefichika kama sio haya mabasi kusajiliwa kama pikipiki.

kabla haujapewa leseni na sumatra mmiliki anapeleka mkataba wa dereva sumatra pamoja na picha ya dereva, haya malalamiko yanatokea wapi hasa?
 
Mimi sio intellectual however i still have an opinion to air on this.

Ukitoa hilo la bima yote yanawezekana provided wapanda mabasi wako tayari kulipia hizo gharama za nyongeza kama mleta mada alivyogusia. Sasa basi tujikumbushe tu mwaka jana nauli zilivyoongezwa ni jinsi gani abiria walivyo chachamaa na hakuna exactly hoja kutoka kwa wafanyabiashara wa mabasi ni kiasi gani inabidi abiria wafidie hili kuweza timiza madai ya madereva im thinking na makonda pia.

Lakini hilo la bima ni hadithi kwanza huo mshahara sijui unatakiwa upande kwa kiasigani ili kuongeza huu wa sasa ambao aumudu maisha na kuwe na cha juu ili kuweza kulipia pension fund. Isitoshe kuna wafanya biashara wangapi ambao wako stable kwa sababu pension fund nyingi zinamuda wa kuchangia kabla ya kufikiriwa kimalipo.

The only way ili linawezekana kama wafanyakazi wenyewe wanaweza ridhia kujikatia bima wao wenyewe na kazi ikisimama wajue ni muda gani wanatakiwa kuchangia watafute mbinu za kuendelea kulipia, kwa sababu hakuna pension fund inayolipa bila ya muda fulani wa mchango wako sasa.

Apart from that ni madai ya msingi kabisa isipokuwa mazingira sidhani kama yanaruhusu utekelezaji.
 
kabla basi halijapewa leseni sumatra lazima ukatie comprehensive insurance na nakala ipelekwe sumatra bima hiyo inakinga gari dereva na abiria wanapodai bima hapa kuna tatizo limefichika kama sio haya mabasi kusajiliwa kama pikipiki.

kabla haujapewa leseni na sumatra mmiliki anapeleka mkataba wa dereva sumatra pamoja na picha ya dereva, haya malalamiko yanatokea wapi hasa?

Comprehensive insurance inacover gari na abiria tu dereva hayumo, usiongelee kitu kama hukifahamu. Dereva hatambuliki kwenye bima ya gari kimkataba wa bima(insurance policy), ndio maana wanahitaji kuwa na bima zao wakiwa kazini, wao wanajua hivyo.
 
Hivi mi nauliza jamani haya madai ya madereva wetu ni sahii kung'ang'ana na serikali badala ya waajiri wao? madai yao ya msingi ni haya hapa;
1. kufuta kusoma kila lesen inapo-expire (hili limeishafutwa tayari)
2. madai ya mikataba bora ya kazi
3. posho za safari
4. mishahara inayokidhi malipo ya pango
5. bima (nadhani hapa wanamaanisha bima ya afya)
6. nauli ya kazini kwa dereva

Ila yote tisa, kumi ni kwamba haya madai yao mwisho wa siku yatapandisha nauli za mabasi na dalala halafu watu wataanza tena kulalamika. Wote tunajua mfanyabiashara habebagi hasara, sisi abiria ndo tutabeba huo mzigo kwa kupandishiwa nauli

We ndio unataka kuchanganya mambo, utaratibu wa sasa ni kuwa, mtu ukiagiza basi, ukimalizana na tra, unakwenda wizara ya kazi na ajira, kujaza form ya mkataba wa ajira baina ya tajiri na dreva, yote mliokubaliana yanakuwa kwenye mkataba, mnasaini mbeleya afisa kazi, unabandika na picha ya dreva husika, wanaipitisha na kugonga mihuri, wanampa tajiri anazipeleka SUMATRA, nao wakishazikagua ndio wanatoa, kibali cha route husika. Sasa cha ajabu kinachofanyika sasa ni kuwa tajiri anakwenda wizara ya ajira na picha ya mtu anayodai kuwa ndio atakuwa ni dreva wake anagongewa mihuri na mkataba unapita kimagumashi, anaupeleka sumatra anapewa route, bila kumuona huyo dreva physically!! Sasa unaposema kuwa madai yao yataongeza nauli sio kweli, na serikali hapa sio kwamba inapanga kiwango cha mshahara wao, kila sector, ina kiwango chake cha chini cha kulipa wafanyakazi ambacho serikali ilikipanga siku nyingi, wao wanataka waajiliwe wamechoka kuwa vibarua, na sheria za kazi zipi wazi, sifa za kibarua ni zipi, sasa mtu anaefanya kazi miaka 10,bado ni kibarua!! anakuja kwa baba yake ambaye ni serikali unamkana na kumwambia mi hayo hayanihusu kakae na boss wako, mtayamaliza!! siku zote bepali yeye ni ku maximise profit tu, Can u imagine dreva analipwa mshahara wake kwa kupitia mpesa, tg pesa?? hapo serikali kodi inapata vipi? matokeo yake ni kuzidi kuwaumiza hawa wafanyakazi wengine ambao wako kwenye ajira rasmi, kwani tax Base, inakuwa ni ile ile miaka nenda rudi, Wao wanataka ajira rasmi ambapo hataweza kufukuzwa kwa njia ya simu, na wengi wao wanalipwa posho na sio mishahara. Ila ugumu unakuwa wenye kusimamia haya mambo ndio hao hao wanyonyaji, kwani ukiwaajiri kwenye mifuko ya jamii lazima upeleke, nakufukuzana ovyo hakutakuwepo, Kuhusu bima hapa wanataka bima ya maisha, na sio bina ya afya kama unavyosema wewe, wewe fanya utafiti kidogo tafuta dreva wa hata roli wa zambia, kenya au rwanda akwambie maslahi yake, wa hapa kwetu utawaonea huruma, na tajiri hamtambui tingo, wewe kama una mtaka mtafute kwa pesa yako wewe!! utakuwa una mlipa kwa mileage yako!! Tuwe wakweli mchawi wa yote haya ni SERIKALI,. Watu wakose haki zao eti huku wengine tutapata shida!! wee umekula maharage ya wapi??? Mbona wenyewe kwenye ESCROW hawakuona kama watatuletea balaa kubwa kama hili la pesa yetu kupolomoka kiasi hiki!??? mtu adai ujira wake halali unatwambia atakuletea balaa!! hiyo miradi inayojengwa kila leo chini ya viwango huzioni impacts zake, we bwana vipi?!!
 
Hii nimeipenda sana, safi wizard!!
 
white wizard

Walau umetufungua zaidi kuhusu asili ya mzozo

Lakini bado kuna maswali hususan kuhusu daladala.

Ni kiasi gani daladala moja inatengeneza kwa mwezi na majukumu ya mfanyabiashara ya madeni kila mwisho wa mwezi (ata kama kanunua cash lazima hiyo hela iangaliwe in terms returns pia); kwa sababu ukisha muweka mtu permanent ina maana akiumwa pia unatakiwa umlipe sehemu ya mshahara wake (kama siko sahihi nisahihishwe). Je daladala wakati inatumia huyo temporary driver wakati huyu anatibiwa ina uwezo wa kujiendeshwa kwa faida? What about gari ikiaribika mwajiri anaweza lipa mshahara au hela yake ya mfukoni ndio inabidi iwe contingency pia?

How much costs/profit ratio iliyopo kwa fair za sasa (kwanza ni kiasi gani fair), maana hivi vitu vyote lazima vizingatiwe na kiasi gani ni mshahara wa sasa roughly kwa dereva, wao wanadhani ni kiasi gani kiwe kima cha chini after the owner has paid for their security funds and tax deductions to the new salary.

Mantki ni kujua kama inawezekana kwa nauli za sasa.
 
Comprehensive insurance inacover gari na abiria tu dereva hayumo, usiongelee kitu kama hukifahamu. Dereva hatambuliki kwenye bima ya gari kimkataba wa bima(insurance policy), ndio maana wanahitaji kuwa na bima zao wakiwa kazini, wao wanajua hivyo.

nashukuru kunielewesha sikujua kama dereva hayuko covered,ni kweli katika manufest jina la dereva na utingo halimo
 
white wizard

Walau umetufungua zaidi kuhusu asili ya mzozo

Lakini bado kuna maswali hususan kuhusu daladala.

Ni kiasi gani daladala moja inatengeneza kwa mwezi na majukumu ya mfanyabiashara ya madeni kila mwisho wa mwezi (ata kama kanunua cash lazima hiyo hela iangaliwe in terms returns pia); kwa sababu ukisha muweka mtu permanent ina maana akiumwa pia unatakiwa umlipe sehemu ya mshahara wake (kama siko sahihi nisahihishwe). Je daladala wakati inatumia huyo temporary driver wakati huyu anatibiwa ina uwezo wa kujiendeshwa kwa faida? What about gari ikiaribika mwajiri anaweza lipa mshahara au hela yake ya mfukoni ndio inabidi iwe contingency pia?

How much costs/profit ratio iliyopo kwa fair za sasa (kwanza ni kiasi gani fair), maana hivi vitu vyote lazima vizingatiwe na kiasi gani ni mshahara wa sasa roughly kwa dereva, wao wanadhani ni kiasi gani kiwe kima cha chini after the owner has paid for their security funds and tax deductions to the new salary.

Mantki ni kujua kama inawezekana kwa nauli za sasa.

hii biashara ukiendesha kisomi inakushinda, fikiria una nunua tata mil 90, halafu unaanza kuletewa sound, leo hatukufanyakazi kulikuwa na mgomo, leo hatukufanyakazi kulikuwa na msafara wa obama!
 
Lakini hizo demands wanazotaka madereva inabidi zijibiwe kwa uhalisia wa faida ya biashara yenyewe without Obama au mgomo period.

Ebu tuangalie mazingira halisi ya sasa na new demands hili kuweza support mgomo, tuangalie jinsi serikari inavyoweza intervene (maana si sawa dereva kuumia kazini alafu awezi tibiwa na mwajiri), mwisho wa siku lazima tujiridhie kipi kinawezekana na kipi ni too much or unrealistic. Hili tuchague upande kwa sababu za kuwa informed as opposed kuunga tela tu la ushabiki (upande wowote) bila ya facts.
 
Mgomaji dereva,tajiri yuko bar msuluhishi Serikali mie sielewi hapa jamani
 
madereva hawapo ktk mifuko ya kijamii kama NSSF, kwa kuwa wengi ni vibarua.

wamechoka kuwa vibarua.
 
Laiti kama mimi rubii ningekua raisi wa nchi.....Mungu anajua ningeliwafanya nini hawa madereva
 
Last edited by a moderator:
1.Bima inayoongelewa hapo si bima ya afya ni bima kazini
2. Serikali ni baba na wananchi ni watoto, hivyo serikali inapaswa kusimamia wananchi(madereva) wake na kuhakikisha wanapata maslahi yao kwa Serikali kuweka utaratibu wa kudumu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri dhidi ya madereva ili kuondoa kero zao.
Mfano wizara ya kazi inaweza kutengeneza mikataba huru ikawaamrisha wamiliki waifuate, nk.

Nilishawahi kwenda kusajili trucks SUMATRA,moja ya masharti ni lazima upeleke mkataba wa kazi wa dereva uliopitishwa na kusainiwa wizara ya kazi! Na nilikwenda wizara ya kazi ni kitu kinachochukua si zaidi ya saa moja kama una documents zote. Taratibu na sheria zipo ila kuna watu hawafanyi kazi yao.
 
In short ni kuwa madereva wanataka utaratibu wa mtu kuwa na daladala moja au mbili uondolewe.
Ili kukidhi mahitaji yao inabidi kuwe na kampuni zenye magari mengi na mfumo madhubuti wa kuwasimamia. In the end hata mapato yao yale ya magumashi yatakosa mwanya, watalalamika tena.

Mimi naona wanajikaanga wenyewe.

Kuhusu kufukuzwa kazi kiholela, sidhani kama mmiliki anaweza kumfukuza mtu anayeheshimu masharti ya kazi na kulitunza gari.

Halafu,next mgomo kwenye hili utakuwa wa mahouse girl. Hawa pia ajira yao haijadalimishwa na hawalipiwi nssf. Kwahiyo kama unaunga mkono madereva, jiandae kuunga mkono mahousegirl pia.
 
dereva ni wa ndege, meli na treni.
dereva wa gari sio proffesional... ni kibarua tu.

Hujui unachoongea!

Nahodha,rubani,dereva.....captain,pilot,driver! Dereva ni kwenye malori,gari etc sio meli wala ndege.
 
Back
Top Bottom