Jamani huku si kupoteza muda?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,519
7,553
kumekuwepo na wingi wa watu wanaokwenda kusajili siimu zao kipindi hiki ambapo zoezi linakaribia kufungwa kiasi kwamba watu wanatumia muda mwingi sana na usumbufu mkubwa.nadhani watu wanatakiwa kujifunza au kufundishwa namna ya kutumia vizuri muda wao.
 
Juu ya suala la matumizi ya muda, hili ni gonjwa kubwa na pengine yafaa kuliita donda ndugu! Angalia tunavyovamiana kutembeleana, tunavyopangana mistari katika ATM, tazama ratiba za vyombo vyetu vya usafiri, jiulize juu ya muda wanaoutumia wakulima wakisubiri mikopo toka taasisi za fedha ama Halmashauri zetu mwanzo wa msimu hadi mwisho. Kweli inahitajika juhudi ya dhati kuifanya jamii ijue kuwa muda ni bidhaa isiyo na dhamani kama haukutumika namna inavyositahili.
 
Hilo zoezi mi nadhani ni futile process, maana hata wakazi wa Tanzania hawana physical address, hata wakisajili, uovu utaendelea kama kawaida.
Maana utakuta mtu anaishi manzese, akisha fanya uhalifu kwa kutumia hiyo simu, kesho yake anahamia magomeni.. Utampataje?
Kuhusu muda, watz tushazoea kuzuga zuga tu, wala hatuna wasiwasi kuhusu kupoteza muda!
 
Back
Top Bottom