Jamani hivi mastaa wa bongo ndiyo wako hivi??

IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,184
7,819
Wana JF muda mfupi uliopita nilikuwa naangalia EATV kuna kipindi kipya kaanzisha Salama Jabir (yule jaji wa bongo star reasch), nikaona anamuhoji dada mmoja mrembo na star wa bongo movie kama sikosei, anayeitwa Irene Uwoya. Wako saloon na wanahojiana mambo mbalimbali but kitu kimoja ndiyo kimenifanya niilete hii hoja hapa kwenye jamvi: Salama kamuuliza huyu star umeshawahi kulewa talalila?? naye akajibu hapana na akaendelea kwamba yeye anakunywa sana lakini cha ajabu huwa halewi, anaendelea kwamba yeye akiamka tu asubuhi cha kwanza pombe! maisha yake yote. Sasa naomba kujuzwa hivi huu ndiyo mvumo wa maisha wa hawa mastaa/wasanii wetu? Hivi ukiwa msanii (ambapo wenyewe wanapenda kusema ni kioo cha jamii) ni lazima pombe ukitawale kiasi kwamba unaigeuza kuwa chai au supu?? Mimi nimeshindwa kuamini nilichokuwa nakiona kwani mdada mwenyewe mrembo wa ukweli halafu cha pombe!!!!
 
haiwezekani huyo kaamua kuosha tu ..kama vipi nimpige siku mizinga tuone kama hatatembea na bikini kichwani hapa ..
 
Mimi sijashangaa sana kwani uwezo wake wa kufikiria ndio umegota pale. Kumbuka amesema hata shule aliona inampotezea muda ndio maana hakuendelea baada ya form IV ingawa baadaye alijisahau akasema ana hamu tena ya kusoma. Watu kama hawa wangetafuta spokesman, labda ingesaidia.
 
Kwa raha zake. .
Angesema hamywi mngesema muongo
Kasema ukweli wake bado mnamwangukia.
 
Sasa jamani, mambo mengine bwana:

1. Hizo ni hela zake kazitafuta kwa jasho lake so hata akinywa 24 hrs everyday si mipango ya maisha yake

2. Ni watu wangapi ni walevi kuliko yeye wako huko ktk jamii zetu kwani wao si kioo cha jamii, wao hawaonwi na jamii au wananyea ndani ya kontena hakuna mtu anayewaona.

3. Tabia ya kufwatilia mtu mwingine anaishi vipi ndo inayofanya watu wengi kuwa maskini masikini badala ya kufikiria kila wakati utatatuaje matatizo uliyonayo

4. Jamii haijifunzi kutoka kwa mastaa tu hata wewe tabia mbaya ambazo unaweza kuzionyesha katika jamii yako unapoishi zinaweza haribu jamii hiyo. Mlevi anayelewa na kupita mitaani akiimba matusi si anaharibu jamii pia??

Nimeandika haya sio kwamba namtetea, simtetei ila hii haibadilishi ukweli kuwa ukweli. Kila mtu ana matatizo yake sasa badala ya kutumia muda kufikiria utafanikiwa vipi unakaa kufuatilia mambo ya watu. Si ndo maana unaona wazungu wenzetu wanaendelea coz hawana taimu na mtu.
 
Hebu waulize wachezaji nyota wa mpira wa miguu hapa nchini kifungua kinywa na kifunga kinywa chao ni kipi ,jibu ni Bob Marley(bangi)
 
Nakikumbuka hiki KIPINDI.

Ni kweli wanakukaribisha SALON, ambapo ndipo yanapofanyikia Mahojiano.

Kuna siku walimkaribisha KAJALA alipokuwa ameshatoka LUPANGO.

SALAMA akawa anamuhoji KAJALA kuhusiana na Maisha yake alipokuwa LUPANGO.

KAJALA akawa anazungumzia Maisha ndani ya LUPANGO mpaka Machozi yakawa yanamtoka
 
Back
Top Bottom