Ubaya haulipwi kwa ubaya na mzazi ni mzazi tu...hivyo sitakubaliana na dhana ya kumpotezea au kuishi mbali nao : that isn't a solution.
Kama una shida mwombe pesa uhakiki je atakunyima? kama akitosa usiuzunike yasahau then tafuta kwa jasho lako kwani pia ni bora kujua akunyimae samaki anakupa uwezo wa kujifunza kuvua. ridhika na kidogo unachopata ndo chako, kisha truggle for better future of urs..lastly mpende baba zaidi ya awali.
Mimi sijaelewa kidogo. Wewe nadhani ni mtu mzima kwa maana umeshapita umri wa utegemezi. Kwa nini unataka baba yako akupe ela? Kwa sababu na wewe ulimpa au kwa kuwa una shida kweli kweli? Mh. mimi hata sijawahi kuwaza kupata mtaji toka kwa baba japo have different story kwani mimi sikutelekezwa.
Haina haja ya kusema piga chini..vita mbele.. kwa nini usumbue akili?
Naungana na mdau aliyesema ubaya haulipwi kwa ubaya. Kuna watu walishatendewa ubaya na wazazi wao lakini hawakulipa ubaya. Waliendelea kuwaheshimu kama wanavyoheshimu majirani zao..
Umeshakuwa mtu unayejitegemea. Sahau senti za baba au mali yake. Mheshimu Baba kama unavyowaheshimu wazee wengine pasipo na cha ziada.
Kama baba ameomba umsaidie kumtafutia kijana mwingine sehemu ya biashara, fanya kama unaweza, yaani kama vile mimi niku-pm na kuomba kama unajua sehemu yeyote iko free kufanya biashara.. kwa upande mwingine unamsaidia kama ungemsaidia jirani yako... kama hauwezi hakuna kusumbuka.
Cha muhimu angaika na maisha yako..usilipize kisasi.. heshima baba na ndugu kama unavyowaheshimu jirani zako waliokuzidi umri.
mpendwa Loly,
kwanza naona kama tayari unalo jibu kichwani kwako kuhusu soala unalotaka ushauri na jibu lenyewe ni kuwa hupendwi na ni vyema ujiangalie mwenyewe na kuwageuzia kisogo baba yako na ndugu zako upande wa baba yako. hili linajitokeza hasa kutokana na namna unavyopokea kwa mikono miwili ushauri wa aina hiyo. ukisoma vizuri majibu yako kwa post zilizokushauri hivyo utaligundua hili ninalolisema.
pili, mi siko mbali sana na michango hiyo hapo juu.
ila nionavyo, tatizo unalo wewe na kwa kuwa umelelewa na mama pekee unaamini kuwa kwa kuwa sasa baba ana pesa na huko nyuma umekuwa ukimsaidia, basi unahitaji special treatment tofauti na ya ndugu zako wengine mliochangia baba. na pia kuna uwezekano kuwa hata mama yako akawa anakuaminisha mamabo hayo na hata kukuchochea utafakari upya upendo wa baba yako
katika jamii yetu kuna sababu nyingi sana zinazosababisha mtoto kujikuta analelewa na mzazi mmoja, kwa hiyo usimchukulie baba yako kama "mhalifu" moja kwa moja bila kuzingatia kilichosababisha ulelewe na mama peke yake. pengine hata sababu kubwa ni tabia ya mama yako, au nini kinine tena, hapo wanajuana wenyewe, labda kama walikudokeza kidogo japo hawawezi kukueleza kila kitu katika mahusoiano yao.
nijuavyo mimi, mtu asiyejiweza, mfano asiye na kazi ama biashara ya kipato cha kueleweka ndiye huwa anasaidiwa ili anyanyuke kimaisha na huenda baba yako anajitahidi kuwanyanyua ndugu zako ili nao wajitegemee hasa uizingatia kuwa pesa kachelewa kuzipata na huenda hakuwa amewaandaa vizuri kielimu kama wewe ulivyoandaliwa na ndio maana anaona basi bora ajaribu kuwapa mitaji wajaribu biashara. kwa upande wako, umesema mwenyewe kuwa una elimu na kazi na umekuwa hata ukimsaidia huyo baba yako. sasa na wewe unatakiwa kusaidiwa? aache kusaidia wasio na kazi na wasiojiweza kiuchumi, akusaidie wewe unayejiweza? au unataka akulipe pesa uliyokuwa ukimsaidia alipouwa na hali ngumu? nasikitika kusema kuwa, kwa kweli huu sio ubinadamu!
kama tatizo ni wasiwasi ulionao kuwa huenda hana mapenzi ya kweli kwako, basi chukua hatua ya kumjaribu, jifanye una matatizo kazini au tatizo jingine lolote ambalo kama mzazi litamshtua, kisha uone anavyo-react. na ukishaprove kuwa anakupenda, basi mweleze ukweli kuwa ulikuwa na mashaka na upendo wake ndio ukaamua kumjaribu na kama alikupa pesa mrudishie mwambie umethibitisha upendo wake ili naye ajue kulikuwa una mawazo gani upande wa pili. ila tahadhari ni kwambasi vyema kumjaribu mtu, kazi ya kuleta majaribu ni ya shetani, sisi tunapaswa kupambana na kuyashinda majribu, siyo kuyaleta ili kuwakwaza watu.
zaidi sana tafakari vizuri ushauri unaopewa na mama yako kumhusu baba yako, kuna mifano mingi sana ya watoto waliolelewa na mzazi mmoja kupotoshwa na huyo mzazi aliyehusika na malezi kumwelekea mzazi mwingine, so watch out my dear.
mwisho, kama ulimsaidia baba, ulifanya vyema na usichukulie kama ilikuwa investment ambayo unataka anze kuklipa na riba. tenda wema usitafute shukrani, upendo wa kweli huvumilia, hufadhili (1 Wakorintho 13:1-13). mwachie Mungu ndiye atakayekulipa kwa wema wako. sisi tunatakiwa kuwapenda hata adui zetu, sembuse kumpenda baba yako?
nakuombea amani ya Bwana ipitayo akili zote
Jina la Bwana libarikiwe
Glory to God!