Jamani hii kitu ni ndege ama nini

Sio mbali tu. Hata hapa hapa duniani.
Mfano RPG, Ina rusha Rocket.

Au mabomu karibia yoote ya kutisha umbali mrefu ni rocket. Ukiondoa ya kumtumia gravity. Ya kudrop.
 
Ni ndege ya kawaida, huo kama moshi ni wingu jepesi linalotengenezwa na joto la injini linachemsha unyevu angani na ukipozwa hutokea wingu jepesi, hakuna tofauti lifanyavyo jua kutengeneza mawingu.
 
Hongera kwa serikali ya awamu ya5 kwa kuwezesha kidude hicho kupita, haikuwa kazi rahisi hapo awali kwani miundombinu ya anga za juu ilikuwa haijatengenezwa, vidude hivyo vilipita kwa tabu kutokana na anga kuwa bovu
 
Hongera kwa serikali ya awamu ya5 kwa kuwezesha kidude hicho kupita, haikuwa kazi rahisi hapo awali kwani miundombinu ya anga za juu ilikuwa haijatengenezwa, vidude hivyo vilipita kwa tabu kutokana na anga kuwa bovu
Tunamshukuru mweshimiwa rais kwa kutuwezesha kuona contrails
 
mkuu anga la kimataifa likoje? nieleweshe tu kwa hapa.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Anga la Kimataifa ninavyofahamu Mimi ni kuanzia 10 km kwenda juu zaidi.

Rocket Engine Muanzilishi wake ni German kipindi cha Hitler.
Baada ya Vita ya 2 ya Dunia kuisha, USA na Russia walikimbilia kuchukua Know How ya Hitler na kuiba Wanasayansi wa German.

Huo Mvuke tunaouona, kuna Mtanzania aliugundua na mwisho wake Hadi leo hicho kitu wamekipa jina lake yaani MPEMBA EFFECT.
Erasto Mpemba alikuwa Mwanafunzi aliyegundua kwamba Maji ya Moto na Maji ya Baridi ukiyaweka kwenye Freezer, yataganda Kwanza maji ya Moto.

Hewa ya Moto ilitokea huko juu kwenye baridi basi inaganda na ndicho tunakiona.
Mpemba Effect.....

Samahani kuuliza, unaposema anga la kimataifa inamaanisha nn? na hua zinaelekea wapi? haziwezi tua hapa kwetu?
 
Mmmh Mpemba effect tena kaka???? Noo pale kinachotokea ni hewa yenye ubaridi inakuwa heat up na jotoo la ndegee inaform kitu kama Mvukee ndo unaona kwa mbali as Clouds nyeupe.. Mpemba effect is all abt freezing na pale hakuna freezing ni heating up ya hewaa kuform steam..
 
Ni kweli urusi ndio ilikuwa ya kwanza kutengeneza rockets za kwenda anga za juu na ndege kubwa kama antonnov,corncord,nk kipindi hiko marekani anasubiri kwenye rockets anga za juu
Hapana ujeruman ndo ilikuwa nchi ya kwanza kuunda loketi.
 
Water can be in three forms: Solid, Liquid and Air.
Vinginevyo, tupo pamoja.
 
Swali la nyongeza.

Wanasema; Moja ya kazi ya Ozone layer ni kupunguza ukali wa miale ya jua,
Wanasema tena; Shughuli za viwanda na uchomaji misitu vimesababisha Ozone layer kuharibika na miale ya jua inapenya direct kusababisha joto kali,
Sasa hii ozone layer inapunguza miale inatoka juu kwenye hiyo source au inayohit ground kuelekea juu?
Na inakuwaje baadhi ya sehemu huwa hawahisi kuungua na hiyo miale inayorudi juu baada ya kuhit ground, mfano Makambako na Dar uunguaji wa watu na hiyo miale ni tofauti
 
Kwa uelewa wangu huu mdogo, ila wanaojua zaidi watasema hii ni Ndege Kasi aina ya Concorde ambayo kwa Afrika inatua tu Cairo na Cape Town.
Ndege za Concorde zilisitishwa miaka mitatu iliyopita kwa kuwa zilikuwa zinafanya kazi kwa hasara. Kwa Afrika zilikuwa zinakwenda Abidjan, Ivory Coast. Shirika lililokuwa likiunda ndege hizo, ambalo lilikuwa ni la ushirikiano kati ya Uingereza na Ufaransa, lilifungwa rasmi miaka mitatu iliyopita.
 
mkuu anga la kimataifa likoje? nieleweshe tu kwa hapa.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app

Ni sehemu ya anga ambayo hatuna mamlaka nayo kama nchi japo mpaka sasa hawajaweka mipaka ya kwenda juu (vertically) kama iliyo kwa bahari ambapo tuna mamlaka ya mile 12 tu kutoka eneo la pwani yani beach mfano kutoka pale coco beach unahesabu mile 12 kwenda baharini hapo ndipo unaanza mpaka wa kimataifa wa bahari na kwa upande wa ndege pia ukiwa juu ya eneo hilo la bahari la kimataifa napo napa hesabika kama anga la kimataifa
 
Mkuu hujanisoma.

Umeshawahi kufanya jaribio la Mpemba Effect kwenye baridi Kali? Mie nilifanya nje kwenye baridi kama -10*C.
Nilimpata Mpemba ingawa hakuwa Mzuri sana.


Tafadhali jitahidi kwenda deep zaidi ndiyo utanielewa. Vinginevyo namalizia hapa

Yaah mkuu nimekusoma but issue its all abt freezing kile unachokiona ni Steam sio Ice...!!
 
[Dah hata mimi tokea tukiwa wadogo tulikua tunaambiwa n rocket,,na m najuag n hivyo mpaka leo
 
Asante.

Ila naomba kuuliza Tena huo ukimataifa Ina maana haturuhusiwi kupafanya Nini, au tunaruhusiwa kufanya Nini

mfano wa bahari baada ya hizo miles ambazo umesema je haturuhusiwi kuvua samaki?


kwa ufupi nakaribia kukuelewa Ila sijakuelewa.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi sijawahi kuona hii hali Tz, ila ughaibuni. Si ndege ya abiria au mizigo, nahisi kama sio chombo cha kijeshi, basi pengine ni cha utafiti. Baba yako anaweza kuwa sahihi kuwa ni rocket.
 
Hawakukosea sana,nyingi ktk hizo ni ndege za antonov zinatengenezwa urusi ndio ndege kubwa zaidi duniani upande wa migo zina uzito wa tani 200,000+
You can't be serious..!! Tani what??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…