Habari zenu wanajukwaa,
Kuna rafiki yangu wa kike ambaye nafanya naye kazi katika kampuni moja hapa jijini ametokea kunipenda ghafla, japo sikuwahi kufikiria kama siku moja angetokea kunipenda maana namheshimu. Ilianza hivi, aliniomba namba ya simu nikidhani ni kwa nia nzuri ya mawasiliano hapa kazini,baadaye akanitafuta facebook. Ikafika hatua akanifahamisha anapoishi na siku moja akaniomba nimpitie. Nilipofika, akanisalimia kwa uchangamfu, then akanikumbatia akawa hataki kuniachia. Akaanza kunifnyia vituko vingi vya kunipagawisha nikiwa nimepigwa butwaa. Mwisho wa yote akaingia chumbani akaja na condom, akavua nguo mbele yangu huku akiwa amefunga mlango na kuutoa ufunguo na tukadoo ile kitu.
baada ya pale akanisihi sana mapenzi yetu yawe ya siri sana tusimwambie mtu. Baada ya wiki mbili, shosti yake anayefanya naye ofisi moja (section moja) akaanza kunichangamkia kupita kawaida. Akaanza kunipigia simu, mara facebook, mara msg etc. Alipoona mimi sishtuki akawa anakuja ofisini kwangu na kujiachia achia sana. mwishowe akaamua kusema lililo moyoni mwake kuwa ananitaka tuwe wapenzi. Nikasita kwa sababu najua ana mtu wake tena amezaa naye. Akasema hiyo siyo sababu, anachotaka penzi langu.
Nilipobisha akaniambia mbona wengine nawapa, kwa nini nimnyanyapae yeye? Nikashtuka kuliko kawaida. Nikawa mpole nikaanza kumpeleleza akasema umetembea na mwanamke gani hapa kazini? Nikagundua kitu. Nikamwambia mtaje akagoma. Nikamtishia kiaina, baadaye akasema, "Umetembea na ........ unabisha?" Nikawa kama vile nimenyeshewa na mvua. Nikamwuliza umejuaje? akasema mwenyewe kanisimulia tena kwa mbwembwe, sasa wewe unaninyima nini?
Kwa ufupi, nimechanganyikiwa najuta na roho inaniuma, nawaza nianze wapi kuliondoa hilo sooo? Nikimtolea nje huyu shosti mtu sijui atanifanyia nini, lakini na yeye pia amenisihi nisimwambie kama yeye ndo kaniambiaa hiyo habari. Pili najiuliza huyu shosti mtu anataka nini kwangu, ananijaribu tuu? au mwenzake alinisifia kwake na yeye anataka kuonja muziki wangu? Na je nikimkatalia itakuwaje? Nikiwaza kumgombeza yule wa kwanza naona ndo nitakuwa nimeharibu kabisa maana wataanzishiana bifu wenyewe kwa wenyewe, na pia kwangu.
Hebu nipeni ushauri jamani