Hii pressure ya wanawake wakifikisha 26 na kuendelea imekuwa tatizo sana, wanabaki kuchukua maamuzi magumu

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,956
Nilikuwa nasikia jua likianza kuchowea kwa hawa wenzetu wanapatwa na kiwewe nilifikiri ni utani, ila kwa sasa nimethibitisha ni kweli.

Nina ushahidi wa wanawake 3 ambao nafahamiana nao wenye 26+. Wawili kati yao wamefikia kuchukua uamuzi mgumu wa kutafuta familia(kuzaa bila ndoa almaarufu nje ya ndoa) ili kukabiliana na hii pressure.

Hao ni wanawake wenye elimu zao na wana uhakika wa milo miwili ya kushiba kwa siku(achana na chai hii ni kama maji ya kandoro) ila hiyo pressure imewasukuma kutafuta familia(mtoto) haraka iwezekanavyo. Je wanakwama wapi? na wanaogopa nini wakifika 26+?

Huyu mwanamke wa 3 kwa sasa yuko 30+, kipindi akiwa na 26 niliwahi kumtania "vipi endapo nikitaka kukuoa utakubali"? aliishia kunijibu kuwa "wewe ni kaka yangu, hilo hapana". Mimi sio kaka yake ila tangu tujuane tukazoeana kama ninavyozoeana na watu wengine ndipo akawa ananichukulia kama kaka yake.

Baadae nikapotezana naye kwa takribani miaka 4 nikiwa busy na kujitafuta ila sikuwahi kufuta namba yake. Mimi ndani ya miaka hii 4 tayari nishapata familia yangu(ikumbukwe kabla sijapotezana naye tayari nilikuwa nishapata mtu wangu ambaye ndio tukafunga naye ndoa ndani ya kipindi nilichopotezana na yule mwanamke).

Sasa juzi kati nikamtafuta bana kumsalimia, kwanza akawa haifahamu namba yangu maana alishaipoteza, nikanitambulisha ndipo akanitambua.

Katika kusalimiana nikamuuliza alipo kwa sasa, akasema yupo sehemu fulani, pia akaniuliza na mimi nipo wapi kwa sasa nikamwambia.

Akawahi kuniuliza hivi fulani(mimi) si una familia siku hizi? nikamwambia bado, naendelea kujitafuta kwanza nikijipata natafuta mtu niingie kwenye familia moja kwa moja maana umri nao ushaondoka maana niko 30+. Hilo swali nikamrudishia na yeye tena, "ila wewe si tayari una familia"? akasema bado na ndio analifikiria hilo umri umemtupa.

Nikamwambia basi tutafutiane maana mimi sina muda wa kutafuta niko busy na kujitafuta na siwezi kupoteza muda kwenye kutafuta ila nilitafutiwa nabeba ili niokoe muda na niendelee na mishe zangu. Akasema sawa.

Nikajaribu kumtania tena nikamwambia "unaonaje sisi tumalizane wenyewe ili kuokoa muda" yaani nimuoe yeye badala ya yeye anitafutie, akasema ATASHUKURU SANA. Tukumbuke kipindi akiwa 26 aliwahi kuniambia wewe ni Kaka yangu na hilo haliwezekani(nimesema kule juu), iweje leo akubali kirahisi hivi? hii pressure ya 26+ na yeye yupo 30+ lazima aone maruweruwe.

WITO: Mwanamke kama una nia ya kuwa na familia ndani ya ndoa, hakikisha unafanya maamuzi sahihi ingali mapema kabla ya msimu wa kusema bora liende haujawadia, mambo yanaweza yasiende kama unavyotarajia ila kwa kiasi fulani inabidi uwe flexible ili kuruhusu yaende
 
Shemeji kila mtu na kipaumbele chake, waache kutupangia ndio kwanza tupo “Ngoswe mapenzi kitovu cha uzembe” 😂😂😂
Mm nikaoa mapema kabisa shemeji. Hapa unatoa wazo la kusaidia vichwa maji huku uswahilin... Kwa watu wazima kama mm na wife hatuwez kuwa na experience ya hizi mana tumenyooka. Hatuna mbambamba! Mda kama huu na kabolingo nangae kwa mbali sanaaaa ..
Wewe toa opinion yako mana mada huru hii

Cc. Antonnia
 
Mm nikaoa mapema kabisa shemeji. Hapa unatoa wazo la kusaidia vichwa maji huku uswahilin... Kwa watu wazima kama mm na wife hatuwez kuwa na experience ya hizi mana tumenyooka. Hatuna mbambamba! Mda kama huu na kabolingo nangae kwa mbali sanaaaa ..
Wewe toa opinion yako mana mada huru hii

Cc. Antonnia
Mi bado nipo nipo kwanza, sasa nitahadithia nini wajukuu kuhusu babu yao 😂😂😂
 
Mm nikaoa mapema kabisa shemeji. Hapa unatoa wazo la kusaidia vichwa maji huku uswahilin... Kwa watu wazima kama mm na wife hatuwez kuwa na experience ya hizi mana tumenyooka. Hatuna mbambamba! Mda kama huu na kabolingo nangae kwa mbali sanaaaa ..
Wewe toa opinion yako mana mada huru hii

Cc. Antonnia
Baelezeee baelezeee baeleeee!

Tatizo banachukulia watu poa sanaa!
 
Back
Top Bottom