Jamani CHADEMA na CCM mmekunywa maji ya bendera?

komedi

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
204
17
Kutoka kwenye maktaba yetu ya matukio yanayohusu bunge la jamhuri kuna matukio mawili yanayohusu wabunge wa CCM na CHADEMA wakati wa kuapishwa kama ifuatavyo:

Tukio la kwanza.

Mbunge mmoja wa CHADEMA ilibidi asahihishwe mara moja na spika pale alipoanza kuapa kwa kusema '' mimi fulani bin fulani......'' akakaa kimya kidogo kisha akapaza sauti kwa kelele '' peopleeeeeeeezzzz!!!!!

Mama yetu ikabidi aingilie, '' wewe fulani, hata kama ni Power lakini hapa unatakiwa uape kwa mfumo wetu hayo mengine huko huko jukwaani.


Tukio la Pili.

Mbunge mmoja wa CCM akiwa ndio amekabidhiwa msahafu naye akaanza kuapa akasema '' mimi fulani bin fulani...kwanza kabisa nikupongeze wewe Mwenyezi Mungu kwa kuchaguliwa bila kupingwa kuwa Mwenyezi Mungu.....!!!

Mama akaingilia tena, '' wewe fulani, unatakiwa uape kwanza kupongeza baadaye.
 
Mwenyenzi amechaguliwa bila kupingwa?
Hii kweli kali...............:smile-big:
 
Mwenyenzi amechaguliwa bila kupingwa?
Hii kweli kali...............:smile-big:

Kwanza kabisa nikupongeze wewe TANMO kwa kuchaguliwa kwako kusoma stori hii, Nikupongeze pia kwa kupongezwa kwa kuchaguliwa, kisha tena niwapongeze.....yaani!!!!
 
Back
Top Bottom