VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Leo kulikuwa na Kongamano la kusindikiza Maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika.Maadhimisho hayo yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Wanazuoni wa UDSM-UDASA,yalifanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Ukumbi wa Nkrumah. Wachokoza hoja na Wachangiaji walikuwa wengi.Lakini nilikuwa 'bias'.Niliwafuatilia kwa ukaribu wa kutoka chama tawala-CCM hasa Deo Filikunjombe na January Makamba.
Makamba alijinadi kwa hoja mbili: kwanza, urais wa 2015 uende kwa aliyezaliwa baada ya 1961.Na pili, elimu bure inawezekana. January,kabla ya kuwa Mbunge wa Bumbuli, alikuwa Mwandishi wa Hotuba wa Rais Kikwete kwa muhula wote wa 2005-2010 akisaidiana na Prof. Mukandala wa UDSM. Ni yeye aliyekuwa akipamba hotuba za Kikwete wakati wa kampeni za 2010 kukejeli hoja za CHADEMA kuwa elimu bure inawezekana na Kikwete,aliyezaliwa miaka 11 kabla ya uhuru,ni chaguo sahihi kwa watanzania. Leo akisema hivi,tumueleweje? Si muongo,mzandiki na mnafiki huyu?
Deo naye kasema Tanzania si mali ya CCM....ni mali ya watanzania wote. Mbona yeye ni mwimbaji mzuri wa kidumu chama cha mapinduzi na wa kuwaaminisha watanzania kuwa bila CCM hakuna Tanzania na 'vice versa is true'? Alitaka aeleweke vipi Deo? Si muongo huyu kwakuwa bado yupo ndani ya CCM na mtawanyaji mzuri wa ujumbe wa kifisadi kuwa Tanzania ni mali ya CCM?
Niliondoka mapema kwakuwa waliniudhi sana.Wana bahati kulikuwa na ulinzi.Pia,nililinda heshima yangu.Humchukia sana mtu mnafiki hasa anapokuwa karibu yangu!