Jamani anataka kufia bungeni huyu tumwokoaje?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani anataka kufia bungeni huyu tumwokoaje??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Mrema wa TLP atangaza kumvaa Kimaro wa CCM Vunjo[​IMG]Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, anawania kiti cha bunge Vunjo.[​IMG]*Kimaro ampuumza asema 'alifulia, atafulia tena'

  Na Zaina Malongo

  BAADA ya kushindwa kufua dafu mara tatu katika mbio za urais, hatimaye mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema amerejea kwenye kinyang'anyiro cha ubunge baada ya kutangaza kuwa atapambana na Aloyce Kimaro kuwania jimbo la Vunjo.

  Mrema, ambaye amewahi kugombea urais akiwa na NCCR Mageuzi na baadaye TLP, alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20 kabla ya kutofautiana na serikali na baadaye kujiunga na upinzani katika miaka ya tisini.

  Wakati hali ikionekana kumuendea kombo Kimaro kwenye jimbo hilo, Mrema anaonekana kutaka kutumia mwanya huo kurudi Vunjo ambako TLP ina nguvu kubwa.

  Mwenyekiti huyo wa TLP aliliambia gazeti hili jana kuwa baada ya kumtikisa Kimaro katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda katika vijiji 20 na vitongoji 48 dhidi ya vijiji 47 vya CCM, sasa anajipanga kwenda jimboni humo kugombea ubunge mwakani.

  "Baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa namtangazia rasmi Kimaro kwamba mwakani naenda Vunjo kulichukua jimbo langu. Kimaro ameshindwa kuwasaidia wananchi ndio maana wamemzomea," alisema Mrema alipoongea na Mwananchi jana.

  Mrema, ambaye alikuwa waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya awamu ya pili, alitoa tamko hilo wakati akizungumzia tuhuma za Kimaro kwamba wanachama wa TLP ndio waliomzomea wakati akihutubia mkutano wa uliofanyika mji mdogo wa Himo ulio kwenye jimbo la Vunjo, Moshi Vijijini Jumatatu iliyopita.

  Kimaro alishikwa na maswahibu hayo baada ya kundi la takribani watu 100 wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa chama hicho kumpigia kelele likisema "hatukutaki", muda mfupi baada ya kuwatambulisha wenyeviti wa TLP waliohamia CCM.

  Kimaro alidai kuwa kundi hilo ni la watu wachache wa TLP waliotumwa na Mrema kwenye mkutano wake.

  “Kundi lilozomea liliandaliwa na Augustino Mrema lililetwa kwenye mkutano wangu na daladala kutoka eneo la Njia Panda, ilipo gesti house na baa yake inayoitwa Twiga. Wao waendelee kuzomea mimi sitishiki na siachi ngozi yangu ngumu nitapambana nao mpaka kieleweke,” alisema Kimaro.
  Â
  Hata hivyo, Mrema alilieleza gazeti hili jana kuwa Kimaro hakuzomewa na wanachama wa TLP bali alizomewa na wananchi wa jimbo hilo baada ya kuwakera kwa hoja alipokuwa akizungumza jukwaani.

  Alisema Kimaro aliwakera wananchi hao kwa kutozungumzia kero ya maji ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu na badala yake akaanza kupiga siasa ambazo hazikuwasaidia.

  "Mbunge huyo kuzomewa Vunjo si mara ya kwanza," alidai Mrema. "Alishazomewa sana na wananchi sehemu nyingi... alishazomewa Kilema Kaskazini, Kilema Kusini, Marangu Magharibi, leo anashanga nini kuzomewa Vunjo?"

  Alisema kutokana na Kimaro kuonyesha kushindwa kuwahudumia wananchi, sasa anaamua kurudi jimboni humo kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

  "Kimaro haliwezi jimbo la Vunjo... ni bora angetafuta jimbo jingine mapema kwa kuwa mimi sasa narudi kumnyang'anya ubunge," alitamba Mrema ambaye baada ya kuondoka CCM alikwenda jimbo la Temeke na kushinda katika uchaguzi mdogo.

  Lakini Kimaro hakuonekana kutikishwa na uamuzi huo wa Mrema baada ya Mwananchi kuwasiliana naye kutaka maoni yake.

  "Kama anakuja aje, lakini akumbuke yeye ni mtu wa kushindwa tu... kushindwa hakuanza leo; alishindwa mwaka 1995, 2000, 2005 haoni kwamba ni mchovu na kachoka?

  "Mrema kafulia miaka yote hii kwenye urais, mwache aje atatukute tukimsubiri na atafulia tena.

  "Sio Mrema tu, amefulia yeye na TLP yote , TLP sio chama cha kitaifa, ina watu wawili tu; yeye na kiongozi mmoja hapa Vunjo, mbaya zaidi wote wamefulia, mwenyekiti kafulia na chama kimafulia." Kimaro alisema hatishwi na ujio wa Mrema jimboni humo kwa kuwa ushindi wake umeanza kujidhihirisha katika matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao KImaro alidai CCM ilishinda vijiji 48, TLP 19 Chadema 10 na NCCR Mageuzi kiti kimoja.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Lyatonga mrema nadhani sasa anaumwa kichwa... yaani pamoja na maradhi yote anaamini anaweza kuwakilisha wananchi?!!
   
 3. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tatizo la viongozi wengi hawana uchu wa kuwaletea maendeleo ya kweli wana nchi wao ila karibu wote wametanguliza maslahi binafsi.Huyu mzee anataka kurudi bungeni kuboresha maisha yake na si kuwasaidia wananchi wake hata afya naona haimruhusu apumzike tu ni mtazamo wangu tu.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Lakiini inasikitisha sana mtu ambaye alishawahi kuwa nainbu waziri mkuu anafikia hatua ya kuhangaika kufungua bar, na kuishi isivyo na uhakika!!! Yeye ni zao la poor forecast la leaders wetu na pia mpango mbaya wa social security systems zetu!!!

  Inasikitisha lakini kumpa mrema kura ni sawa na kuunga mkono matumizi ya siasa kama ajira na kuidhinisha kiu binafsi kutawala mioyo ya leaders wetu!!
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Lyatonga anakumbuka Shuka/Blanket wakati Alarm ya saa yake ya mezani inamwamsha kuwa kumepambazuka! KWELI IMEBAKI STORY kama baadhi ya daladala na Ma-Guta yalivyoandikwa!!
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu ndo maana mi huwa naona kama vile kungekuwa na ukomo wa ubunge ingeweza kutatua mambo kama haya yasijirudie atakuwa na jipya gani huyu ndani ya mjengo? Huyu kweli anatafuta ajira kama vipi si asake zinazotangazwa magazetini.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hahaaa, unaifkiri wankubali hao?? huwa wanaanza vizuri na nia bora lakini wakishalambishwa vile vi-allowances wanakuwa kama wanyama!!! Inasikitisha kusikia mtu anasema "oh jamaa ananyemelea jimbo langu" badala ya kusema jimbo letu...

  Leadership bado na siasa zetu bado, ningefurahi kama Tanzania tungekuwa na sera za majimbo na kupunguza idadi ya wabunge halafu tuweke kikomo cha mtu kuwa mbuge!! kuna watu wapowapo tu!!
   
 8. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha jimbo langu si letu, hapa ndo pana tatizo kubwa kwani kuna baadhi ya majimbo wabunge wake kwanza wameyageuza kuwa ndo miradi yao.Pia Kuwa na mabunge wengi tena wasio na tija ni tatizo kubwa sana na ni mzigo kwa nchi wabunge zaidi ya mia tatu wanini? Nadhani kila mkoa hata ungekuwa na wabunge 5 ingeweza saidia kuliko kuwa na utitili wa wawakilisha wanaosubiri vikao ili wakatoe kero za majimbo yao badala ya kutatua kero hizo kwa vitendo huko majimboni kwao.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bwana weh, haamini hivyo... anajua watu wanampenda na watamchagua hata kuwa rais akitaka!!

  Hivi chama chake kina hali gani kwa sasa?
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na akirudi Bungeni atakuwa siyo yule wa zamani aliyekuwa akiishika serikali pabaya. Atakuwa anaongea mandazi -- ikiwa ni pamoja na kuwatetea mafisadi, kupiga debe mitambo ya Dowans inunuliwe, na mambo mengine yenye kuchefua.

  Hawezi kuungana na wapinzani wenziwe katika kuibana serikali kuhusu ufisadi.

  Nyie mtamuona tu mzee huyu.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  huyu mzee mbona ashakufa kabla ya kuingia bungeni uoni kama kapigwa manati na rostam...sijui ataongeaje kwenye kampeni...embu ccm kumbukeni waliofika ngazi za juu jamani watatufia njiani....yameshinda babu....loooh haya ndio matatizo ya kushindw akurekebisha maisha ukiwa kazini unataka kurekebisha kwenye pesa za ridandas nani kakwambia pesa za ridandas zinajenga nyumba ...mrema kanyi ruwa oko mndumi ngiseka mpaka ngifa...richa kapsa mbe oko wekunyamala nuichi nkui kolimba,kombe, wakeri ambuya necha mleu kanyi...ulakucha wose
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  wana JF,

  Kwa nini mzee huyu ambaye alishawahi kuwa naibu waziri mkuu anahangaika hivi?

  Mimi naona anatupa ujumbe kuwa yeye hakufanya ufisadi/hakujilimbikizia mali. Na kwa kuwa style ya siasa yetu siyo ya kuwalinda viongozi, basi jamaa hana akitu na hana mbele!

  Kwa style hii Mrema atakuwa mfano hai wa watu kuendelea kufanya ufisadi kwa madai kuwa ukizeeka kama 'mrema' upumzike!!

  Ni ujumbe tosha kuwa wale watu waliowasafi serikalini mwisho wao ni mbaya at the end anakuwa YEYE NA FAMILIA YAKE!!

  we need to discuss this in different orientations!

  I submit
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nyi kwelyi kabsa mse!! maan si alishanyewa na mfua kule dodoma ensi sile!!??

  atamwaga upupu hapooo ilimradi wasimuonye na kukosa posho!!
   
 14. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Umefanya vizuri kuangalia upande wa pili wa shilingi ila si kweli kwamba kwa mda aliokaa madarakani ndo awe hana kitu kwavile tu hakufanya ufisadi hii siyo sahihi kwani hakujiandaa hata kwa kuweka kile kidogo alichokuwa anapata na hata kufanya ubunifu wa kukiongeza? Kwa maana nyingine ukiwa kiongozi usijiwekee akiba kwavile tu we si fisadi na utakuwa mbunge milele.Hapana mi naona kuna mahala lazima tukubali atakuwa aliteleza.
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  inshallah ngoja tullale tuamke tutamfikiria....ila ,yoyote aliepita ccm ni mwizi hakuna asie mwizi ccm nanukuu-waziri s.simba
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hii ni supa mkuu, it has to be put into context!!! Hapohapo na mimi nauliza, mrema alikuwa na priviledge zote hata za ardhi, vitega uchumi (tena vya halali), je wakati akiwa na exemption sio yeye aliwahi cruiser badala ya trekta? sio yeye aliyesahau kuhamia kwake akarudi nyumba za serikali?? Mimi bado naamini kufa maskini ni kuwa msafi!!!

  Ninaamini Mrema had all teh clean chances za yeye kuendeleza maisha yake kwenye sekta ya kilimo na kuwekeza elimu kwa wanawe... Kumbuka kwamba familia yako ndio kioo chako!!! unajua watoto wake wana mitazamo ipi??

  Mrema hakuwa akiangalia mbele kwenye maisha, usafi upi wa kutimua kila anayekubishia ??

  I beg to differ
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,842
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  Tatizo pesheni, ni hatari sana kwa nchi zisizo na mfumo mzuri wa pesheni. Huyu Mzee amelitumikia Taifa vizuri miaka ya huko nyuma alistahili kuwa na pesheni.
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  I concur with u sir

  Ila wengi wetu hatuna huo uwezo wa akiba, ndiyo maana hapo juu MTM kasema kuna tatizo kwenye social security systems zetu.Kama alitumia vibaya fedha zake is another case.

  My set was that, kwa nini aende bungeni kwa umri huu, kama hiyo point unaikataa basi ya pili kuwa ni Mamluki wa CCM inaweza ikawa valid!

  Sipati picha ndiyo maana najiuliza!
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  embu nisaidien analipwa ngapi kama pension kwa mwezi??
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  maana hii nchi ndio maana wakati mwingine kesi za kushambulia mafisadi naogopa nahisi wote tumo ndani..mama yangu mmoja kaitumikia serikali miaka 20 majuzi nakuja kujua alikuwa akilipwa sh 25,000 na ppf kwa mwezi...uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
  wameingezewa wote ati mpaka 50,000...kazi ipo kwa nini tusiibe???
   
Loading...