Madaraja bado hayajapandishwa hadi sasa,waliopandishwa hakuna nyongeza mpaka sasa. Wilaya fisadi kuliko zote nchini wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga walimu wanaostahili kupandishwa madaraja hadi sasa haijulikani itakuwa lini,kwani wapo waliodumu miaka 7,6,5 lakini hawajapandishwa. Jamani huu ni uonevu. TUCTA wawatazame walimu Kishapu pia kamati ya bunge ya Mh.Mrema iende ikafanye uchunguzi huko maana pesa zetu za kodi wanazifaidi wajanja. Walimu mnatakiwa mchukue hatua na sio kulalamika tu huko vituoni kwenu,kibaya zaidi hamna umoja kwani CWT hawana msaada zaidi ya kukusanya fedha za uanachama tu. Jiungeni mdai vyenu!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.