Jaman naomba ushauri wenu ili nipone!

Labda ana wasiwasi anaenda kwenye "mazoezi" mengine?
Si unaona NN alivo sema hapa chini?
ndio maana nilizema ni bora wawe wanaenda wote.

Sijui mshikaji yuko wapi lakini kama ana membership kwenye health club basi ninaweza kuelewa kidogo maana huko huwaga ni balaa. Kuna vishawishi vingi sana.
Hii ni mara ya pili nakusoma ukilalamika kuhusu hao wadada wa health club,
tena ulilalamika zaidi kuhusu wale wanao kuja kwa usafiri wao wenyewe. lol

Tena kama ingekuwa ni health club angempeleka na yeye huko. Kuna mtu hapa alishaleta exactly the same thread huko nyuma. Ila mkewe alikuwa na wasiwasi jamaa alikuwa anaenda "kucheza mpira" sehemu nyingine.
Sasa si ndio waende wote huko? inaweza kupunguza suspicions.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mi nina umri wa miaka 23 na yeye ana umri wa miaka 20 kwa wale waliouliza umri!

At least sasa nimejua. Kumbe ana miaka 20 tuu? Na wewe uko kwenye umri ambao kwa kweli ndio unatakiwa uyatengeneze maisha yako ya baadae. Kama angekuwa matured sidhani kama angekukataza kwenda kufanya mazoezi. In fact wanawake walio kwenye ndoa wanafuta jinsi ya kuwafanya waume zao wawe wanafanya mazoezi. Lakini yeye kwa umri wake na akili ndogo anakukataza.

Kama nilivyosema tokea mwanzo piga mpira. Kama una dream yoyote unayotaka ku-achieve maishani jikite kwenye kufanikisha hiyo ndoto. Unasema unapenda sana kama vile unataka kusema kuwa huwezi kumwacha. Well, kwa umri wako chagua moja: Kucheza mpira au yeye. Na hata ukiamua kuacha mpira na kuwa nae sidhani kama kuna uhakika kuwa atakuja kuwa mkeo.

Hivi na yeye hana hobbies za kufanya wakati wewe uko mpirani? Kwangu huyo atakuwa ananiboa.
 
Czms anakupenda ndo mana.
1.Wewe ni mwaminifu kwake? Cse inawezekana kapata tetesi kua unatoka na mwingine
2.Unamtengea muda wa kua nae? Mana baadhi ya wanaume wapenda mpira mcmu Mechi mpenzi anapewa nafasi ya mwisho
3.Uyo girlfriend mnaishi nae kama mume na mke? Muda wote mko pamoja!mpakaakubane kiasi icho?
Tenga muda wa kuzungumza nae naamini ukimuelewesha atakuelewa,kumbuka kutumia lugha laini
 
mmmh kaka hapo pagumu maana mapenzi yamechukua sehemu kubwa sana ok achana na mazoezi endelea kumtumikia yeye
 
Back
Top Bottom