Jamal Malinzi: TFF imemshinda, ni bora akae pembeni

Chief wa kibena

JF-Expert Member
Mar 13, 2016
686
394
Huyu kibosile wa TFF, sio siri shirikisho limemshinda, kwani toka aingie ni kuwa TFF imekumbwa na majanga makubwa ambayo naona kazi imemshinda, moja ya tatizo kubwa no suala la kodi kwa TRA.

Mwaka jana TFF ilishindwa kufanya mkutano wake mkuu kwa kuwa TRA walishikilia akaunti za TFF. Lakini cha kushangaza huyu bosi anahojiwa na waandishi anajibu kihuruma tu, kwamba hana njia za kufanya kunusuru hili.

Juzi magari ya TFF yamekamatwa still haonyeshi TFF wanafanya jitihada gani kurekebisha hilo, ila anataka kuhurumiwa na kidizaini analaumu uongozi uliopita. Nilitegemea TFF anayoiongoza atumie njia yoyote na ajicommit TRA kwamba hizo pesa zitalipwaje.

Suala la mkwasa ndio kichefuchefu yaani hata haieleweki, na anaulizwa eti anasema suala la Mkwasa ni suala la mwajiri na mwajiriwa lakini kasahau mwanzo alisema Mkwasa atalipwa pesa alizokuwa analipwa kocha mgeni.

Huyu bosi ni bora akae pembeni! Soka analoliendesha inaumza kichwa. tunammiss sana Chilla Tenga.Ndio maana wahafidhina walitaka kumzuia kuingia TFF kuwa kiongozi ni jambo kubwa lazima utoe mwelekeo na maamuzi sahihi badala ya kulalamika na kutaka aonewe huruma.
 
Suala kubwa hapa ni kwamba watanzania tulikosea. Na kubwa zaidi ni wale walioshiriki kumchagua naona wako kimya kama vile hakuna kitu kinachoendelea pale TFF. Huyu bwana amekuwa ni mtu wa kulalamika ili aonewe huruma, hivi kipindi kile alipo hamisha ofisi za TFF na kwenda kodisha maofisi hakujua TFF ina matatizo ya kifedha?
Hivi alipokuwa anagombea hiko cheo alikuwa anadhani pale ni peponi? Huyu bwana sio mbunifu kwa kawaida CEO anapoingia madarakani anarithi mafanikio, madeni na matatizo, sasa yeye alitaraji arithi mafanikio pekee? Hapana alikuwa na wajibu wa kufikiri na kutafuta majibu ya madeni na matatizo ya TFF ili soka la Tanzania liweze kusonga mbele. Sasa hivi anavyotulalamikia tumuonee huruma? Akwende, ameshindwa kutawala.
Hivi anafikiri suala la kodi lina huruma, wasiishie hapo TRA waikamue TFF mpaka ilipe madeni yote ya kodi za wananchi. Sote twafahamu umuhimu wa kodi na wajibu wa kulipa kodi, kama aliikacha Cargo Stars asitarajie TFF ni kichaka cha kutolipa kodi, lazima kodi ilipwe!
Kama aliingia madarakani na kukuta watu wametafuna hizo pesa yeye alichukua hatua gani? Asitafute huruma ili aendelee kutuumiza, kama alitegemea ubwete wa Sheikh Salman, sasa mambo iko kwa Infantino. Ukiuliza watu wa Mwanza kuhusu ule mradi wa kuweka nyasi bandia ndo utachoooka kabisa. Alichokifanya anajua yeye, uwamnja hadi leo haujawekewa nyasi. Huyu jamaa akwende waliomchagu tunawaomba mtondolee huyo jamaa.
 
TRA wasiishie TFF waingie Simba na Yanga hizi timu zimekuwa vichaka vya wakwepa kodi huyu malinzi ndio zero kabisa badala ya kutafuta ufumbuzi analilia
 
Majanga ya Malinzi ni ya kujitakia kabisa. Mwanzoni mwa uongozi wake alifanya makosa mawili makubwa yenye gharama kubwa kifedha.
Kwanza ni kumtimua Kim Poulsen na kulipa fidia kubwa tu. Kama hela ya fidia anayo kwa nini asilipe PAYE?
Pili, aliamua kuacha ofisi za TFF pale Karume na kwenda kupanga maghorofani kwa gharama kubwa sana hadi alipolazimishwa na FIFA kurudi Karume.
Hayo yote yanaonyesha ni kiongozi wa ovyo kabisa.

Malinzi aondoke mwenyewe kwa heshima. Najua anasoma JF. Ujumbe umefika.
 
Kwanza kbs niungane na other jf member kumlaumu na kumshutumu kwa uongozi wake mbovu ambao kiukweli haustahili kuwepo tena
lkn lawama kubwa nazipeleka kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa tff ambao kimsingi ndo wapiga kura
Hawa wajumbe wengi ni njaa kali na wengi wao wapo kimaslahi zaidi kuliko kutanguliza maslahi ya soka la taifa letu na hii yote imesababishwa na kuingia tff watu ambao hawaupendi na wala hawajui nn maana hasa ya soka,wengi wamevamia fani,mcheza ngoma ya kienyeji anakuja kuwa kiongozi mkubwa wa soka,mtu hajawahi kupiga ht danadana mbili leo ni kiongozi mkubwa,matokeo yk ni kufanya maamuzi mabovu kbs ambayo yanaendelea kuigharam ygf
 
Tulishasema humu humu wakati anaomba uongozi wa TFF baada ya Tenga kumaliza muda wake kuwa Jamal Malinzi hana uwezo wa kuongoza mpira ila alikuwa anatafuta nafasi ile kwa madhumuni ya kwenda kuiba $$$$ alizoambiwa FIFA ya Blatter ilikuwa inawahonga viongozi wa fooball Associartions worlwide!!! Lengo lake hilo limegonga mwamba kwana TFF sasa ni bankrupt hivyo hana budi kusalimu amri na kujiuzuru kwani Magufuli hana mchezo na hawa team Lowassa waliodhani watafanya mambo yao kienyeji bila kulipa kodi.
 
Malinzi you better go for good,you are disgrace to our soccer,hufai hata kwa kulumagia,kila mahala umepandikiza wahaya na wt ea musoma na kwsbb wengi wao ni mizigo na njaa kali,hakuna wa kukupinga,lkn kiukweli sk zinavyozidi ndivyo unavyoua mpira wetu wa bongo,ulaaniwe ww na kizazi chako,kila mahala ww ni madudu tu,shinyanga umetuwekea kina mbasha lugora of who these are all rubbish ,badilika na jipange upya jambo hifai kbs,kika kitu unaharibu,what a shame????
 
Majanga ya Malinzi ni ya kujitakia kabisa. Mwanzoni mwa uongozi wake alifanya makosa mawili makubwa yenye gharama kubwa kifedha.
Kwanza ni kumtimua Kim Poulsen na kulipa fidia kubwa tu. Kama hela ya fidia anayo kwa nini asilipe PAYE?
Pili, aliamua kuacha ofisi za TFF pale Karume na kwenda kupanga maghorofani kwa gharama kubwa sana hadi alipolazimishwa na FIFA kurudi Karume.
Hayo yote yanaonyesha ni kiongozi wa ovyo kabisa.

Malinzi aondoke mwenyewe kwa heshima. Najua anasoma JF. Ujumbe umefika.
Tatu kutengeneza timu ya vijana aliyoiita maboresho kwa ushauri wa vijiwe vya wauza kahawa
 
Wote hao hao ila kwa jamaa wanufaika walikuwa wengi huyu kawapunguza, lazima wamtoe roho watu wameshinda kulipa ada kwa uchoyo wake.
Tenga aliusogeza mbele mpira Malinzi ameurudisha nyuma tena
 
Timu anayoinoa Kocha Selemani Matola
ya Geita Gold Mine imeteremshwa daraja
hadi la pili.
Geita imepatikana katika hatia ya upangaji
matokeo katika mechi yao ya mwisho ya
Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya JKT
Kanembwa ambayo pia imeteremshwa
daraja.
Katika mechi hiyo, Geita Gold Mine
ilishinda kwa mabao 8-0 na JKT Oljoro
ikakubali kipigo cha mabao 7-0 kutoka
kwa Polisi Tabora, timu hizo mbili pia
zimeteremshwa daraja pia kwa
kuhusishwa na upangaji wa matokeo.
Ila JKT Kanembwa iliyokuwa imeteremka
daraja yenye inashushwa hadi Ligi ya
Mkoa.
Uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ya
TFF, umetangazwa leo mchana lakini
uongozi wa Geita Gold Mine umesisitiza
kwamba utakata rufaa kwa kuwa hakuna
sehemu inayoonyesha timu yao ilipanga
matokeo.
 
Back
Top Bottom