Jamaa yangu anataka kumfumania mke wake leo

Jamaa yangu anataka kumfumania mke wake leo

Kama hajui cha kufanya anaenda kufumania ili iweje??????


Jamani leo saa kumi jioni kuna rafikiangu anaenda kumfumania mkewe. Amepewa information zote kuhusu mkewake na guest ambayo huwa anapenda kuitumia wanapokutanaga na huyo mtu wake.Sasa hapa ameniuliza nini cha kufanya endapo akifika na kumfumania mkewe aanze na kufanya nini?

Kaeni tayari kwa mrejesho
 
Mwambie asiende na mtu mwingine yeyote ila yeye peke yake, kisha akiwakuta sifanye jambo lolote ahakikishe tu kwamba mke wake ameuona na amejua na huyo mgoni wake pia. Kisha arudi nyumbani kupumzika, mke wake akirudi nyumbani asimsemeshe chochote kuhusu tukio. Na aendelee na maisha na mke wake kama kawaida. Kwa kufanya hivi mke wake atajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu na ni psychological torture kwa mke wake na hatorudia tena ila mwisho wa siku amsamehe.
 
Tushasepa hiyo GH tumehamia nyingine yaani barabara tofauti kabisa ha ha hakamatwi mtu hapa
 
Mi namshauri amuangalie mwenzake Kwa makini anchomganyia mkewe ili ajue mapungufu yake yako wapi ajirekebishe kupitia msela aendelee na mkewe kama kawa

Eti eeehhh usikute anakosa dushelele ama mkwanja
 
najua atakuwa na hasira lakini cha msingi asiwahi kufanya uamzi wa haraka. ni vyema akajaribu kutumia akli kwanza na kufikiria cha kuwafanya palepale kuliko kuziacha hisia zikachukua nafasi yake mara tu atawakuta.
 
Ni aje director wa fumanizi!? Wamestuka na kuhamisha Kiwanja?
 
Huo ni ujinga tu,
anaenda kujiaibisha, amwambie mkewe kuwa ana mpango wake wote hivyo aache uzinzi.
Kufumania anataka aibu tu huyo.

Labda anataka apate uthibitisho ili aweze chukua hatua stahiki...!
 
Wanaokwenda kufumania hufanya "surprise " si kama hivi. Naona unawatisha wazinzi waliomo JF!
 
Wandugu sasa ndio tupo eneo la tukio kwa pembeni kidogo tukiwa tumetega hapa
Subiri kazi iiishe ili nije na mada iliyokamilika

MREJESHO PLZ; Vp kiongozi kuna usalama kweli mbona kimya bado hamjafumania au mmezimia wenyew maana yahtaj moyo
 
Asipanic,apige picha tu kwa ajili ya ushahidi kisha asiwafanye chochote awaache waendelee yeye arudi nyumbani..
 
Mi namshauri amuangalie mwenzake Kwa makini anchomganyia mkewe ili ajue mapungufu yake yako wapi ajirekebishe kupitia msela aendelee na mkewe kama kawa


Hapo umenena, afuate ushauri huo, mambo yakumpiga mgoni wakati labda yeye ndio chanzo cha mke kutoka hayakubaliki.
 
Back
Top Bottom