Jamaa pumba kabisa!

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
May 24, 2013
3,564
1,991
Jamaa mmoja karudi nyumbani gafla akasikia sauti za ajabu kutoka chumbani kwake,
akavunja mlango na kuingia akamkuta mkewe anatetemeka akauliza "Vipi mke
wangu?"
Mkewe akajibu "Presha Imepanda." Jamaa akakimbia sebuleni kupiga simu kuita Ambulance wakati anahangaika
Kupiga simu mwanae mdogo akamfata
Akamwambia "Baba, ba'mdogo yuko uchi
kwenye kabati chumbani."
Jamaa kwa hasira akatupa simu chini akarudi chumbani haraka alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo
wake bila nguo na yeye anatetemeka, Jamaa akauliza "Na
wewe vipi unazubaazubaa bila nguo
unamtisha mtoto wakati shemeji yako
ameshikwa na presha, vaa haraka ukaite Ambulance."

Tehe tehe tehe tehee!
 
tehe tehe tehe
ukiwa na akili kama hizo utaishi maisha marefu sana huwezi pata ya magonjwa ajabuajabu
 
Last edited:
Back
Top Bottom