Nina rafiki yangu alikupendana na mdada ambae ametoka kutengana na mwanaume wake.
Jamaa akaanza msumbua bi dada akiwa tayari anaishi na rafiki yangu. Rafiki yangu akawasiliana nae, jamaa akajitetea kuwa anafanya hivyo sababu anataka kujua hali ya watoto hakuna ubaya mwingine....
Mtoto wa kwanza ana miaka 6, wa pili ana mwaka na miezi. Jamaa akasubiria mtoto amalize muda wa kunyonya. Huku jamaa akisumbua sana. Mtoto alipotimiza miaka miwili na nusu, jamaa akaona huu ufala.
Jamaa alikuwa bado anaendelea kumsumbua bibie na kubembeleza. So jamaa akamwambia mwanamke awaandae watoto awapeleke kwa baba yao.
Wakaenda na house girl, jamaa akawapokea vizuri, yule dada akalala hapo hapo akiwa na watoto na house girl, walilala chumba tofauti na jamaa asubuhi jamaa akatoka na kwenda kazini akiahidi atarejea mchana mapema ili waketi na kuongea....
Alipoondoka tu yule bi dada akampa maagizo beki tatu kuwa awatazame watoto vizuri yeye anarejea. Akaondoka akarudi home kwake.
Jamaa kurejea anakuta bi dada hayupo na sim yake haipatikani, kumbe amebadili namba kabisa. Mshikaji akampigia mwanaume(aliomba namba kwa beki 3) alipoona hampati bi dada hewani.
Kumpigia jamaa na kujitambulisha jamaa akamwambia unataka nini, jamaa oooh mbona bibie amewaacha watoto na watoto wanahitaji malezi ya mama, akawambia ulikuwa unasumbua kutaka kujua kuhusu watoto. Haya hao hapo upo nao, usimsumbue tena huyu mwanamke sio mkeo tena, na kuhusu malezi hao watoto hawanyonyi tena ni wakubwa wanakula chakula cha kawaida.
So pambana na watoto wako ulee maana ulikuwa unasumbua kisa watoto haya hao hapo na wewe ni baba yao, lea damu yako. Kama hauwataki tuandikishiane kabisa na iwe ni makubaliano kuwa hautaki hao watoto tena, nitalea mimi, na tutarekodi hadi video ukikubaliana kabisa na haya masharti kuwa hautakuwa tena katika maisha yao.... La si hivyo, hao hapo lea watoto wako acha kusumbua mtu asiye kuhusu tena.....
Jamaa akawa wabaridi balaa...... Kurudisha watoto hawezi, kukaa nao bila mwanamke anaona amekomolewa...... Balaa akawa nalo....