Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

Jakaya Mrisho Kikwete, Mungu atakulipa!

MJENGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
883
Reaction score
852
Ndugu zangu watanzania wenzangu, kupitia jamvi hili, kwa heshima na taadhima nichukue fursa hii kumwandikia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kwanza kumpa pole kwa majukumu mazito aliyonayo katika kulitumikia taifa lake. Ninampa pole kutokana na kutambua ugumu wa majukumu aliyonayo.

Kwa nafasi yake, yeye ndiye wa kutupiwa lawama zote pale mambo yanapokwenda si sawa. Pia ni mtu wa kupongezwa pale mambo yanaponyooka. Hii ni kawaida kwani wahenga walikwushasema kuwa mkubwa ni jalala.

Ndugu zangu watanzania wenzangu, mimi leo ningependa kuzungumzia kazi nzuri ambayo Rais Kukwete ameifanya ambapo hata kama baadhi yetu tutaibeza, ukweli utajidhihirisha.

Kikwete, katika kipindi cha miaka 9 amefanya yafuatayo mazuri;
1. Uchumi; amefanya mabadiliko kwenye kilimo ambapo wakulima wengi kwasasa wanalima kisasa na kwa msaada wa pembejeo za ruzuku.

Walau imesaidia taifa kuwa na akiba ya chakula cha kutosha hivyo kutokuwa na hofu ya wananchi kufa njaa. Kilimo cha umwagiliaji kimeongezeka, kilimo cha biashara kimekua. Mabadiliko ya sheria ya uwekezaji angalau yamewezesha nchi kuanza kunufaika na kodi ya uzalishaji ingawa bado si kwa kiasi kikubwa. Uboreshaji wa huduma za kibenki, mikopo ya saccos, uboreshaji wa njia za uchukuzi kama barabara, vivuko, reli kwa kununua vichwa na mabehewa, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege e.g. Rungwe, Katavi, Gombe, DSM. n.k.

2. Kisiasa; Ni katika kipindi cha Kikwete ambapo uhuru wa shughuli za kisiasa umetolewa. Watanzania sote ni mashahidi kwamba vyama vya siasa vimekuwa huru kiasi kwamba baadhi vimeshindwa kuutumia uhuru huo ambapo baadhi vimeishia kuitisha maandamano, kukitisha chama cha mapinduzi na kutishia uvunjifu wa amani kama mbinu ya kutaka kutimiza adhma zao za kisiasa.

Ni wakati huu ambapo majukwaa ya siasa yametumika kuvitukana na kuvidhalilisha vyombo vya dola kwamba havina lolote. Ni wakati huu ambapo wanasiasa wa vyama pinzani wameachwa kuichambua serikali kwa kadiri ya hazina ya maneno iliyoko vinywani mwao.

Ni wakati huu ambao hakuna mwanasiasa aliwekwa kizuizini kwa kutoa kauli zenye kuhatarisha usalama wa nchi. Wanasiasa baadhi yao walifikia hatua ya kutisha kuwa wanao uwezo wa kuifanya nchi isitaealike, hakuna aliyeshughulika nao.

Aidha ni wakati huu ambao siku moja watu walikuwa wakishuhudia chama fulani kimeitisha maandamano nchi nzima kisha muitisha maandamano akakimbilia South Africa! Kiukweli ni wakati unaelekea mwishonu lkn kwa wanasiasa hasa wa upinzani mtaukumbuka!!!

3. Kijamii; Rais Kikwete amejitahidu kuimarisha huduma za kijamii kama usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, Ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa gesi asilia huko Mtwara ambapo sote tunajua jinsi wanasiasa walivyoupinga na kufanya kila aina ya uchochezi ili usifanikiwe, leo tunashuhudia mradi unelekea kujamilika.

Miradi ya maji vijijini imetekelezwa kwa kasi awamu hii. Upande wa elimu mafanikio yako wazi ambapo ongezeko la ajira za walimu, ongezeko la shule za msingi na sekondari na pia ujenzi wa vyuo vikuu kwa ujumla vimetokea wakati wako.

Maboresho ya mishahara kwa wafanyakazi yamefanyika wakati wako. Kwa upande wa afya, siyo siri ununuzi wa vifaa vya kisasa mahospitalini walau umefanyika wakati huu kwa kiwango cha kuridhisha, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kupitia TASSAF, hospitali za mikoa kuwa za rufaa, mapambano dhidi ya malaria na UKIMWI, uzuiaji wa vifo vya mama wajawazito, juduma bure za matibabu kwa wazee (bado changomoto katika utekelezaji), maboresho ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo sasa ina uwezo wa kutibu magonjwa ambayo awali matibabu yake yalipatikana nje yanchi n.k.

4. Kimataifa; Kwanza amejitahidi kukwepa mitego ya maadui zetu waliotaka kuliingiza taifa vitani kwasababu za chuki binafsi na wivu kutokana na nchi yetu kuanza kukua kiuchumi kwa kasi. Mfano wa nchi hizo sote tunao. Kikwete alijua kwamba vita kwasasa siyo kipaumbele cha nchi ingawa uwezo wa kuwachapa hao maadui zetu tunao.

Alifanya uamuzi mzuri na wa kizalendo. Isingekuwa rahisi kwa Rais asiye busara kuacha kuiingiza nchi vitani dhidi ya Rwanda, Malawi na Kenya wakati ambao nchi hizo zilionesha wazi kuichokoza Tanzania. Ni busara ya kiwango cha juu aliyonayo Kikwete hata kufanikiwa kuukwepa mtego huo.

Pia amejitahidi kusuluhisha migogoro katika nchi mbalimbali kama vile ule wa Kenya mwaka 2008, wa Sudan ya Kusini, Congo DR, Comoro, Afrika ya kusini (wa ndani ya ANC). Amekuwa na ushawishi mkubwa kwa mataifa makubwa kwa kuifuata sawasawa sera mama ya taifa ya kutofungamana na upande wowote kwa lengo la kuiepusha nchi kuwa na uadui unaotokana na mivutano baina ya mataifa makubwa.

Katiba mpya; Jambo hili halijaisha, tumwombe Mungu liishe salama!. Sote ni mashahidi juu ya umahiri alionao Kikwete katika namna anavyolihandle swala hili muhomu kwa mstakabali mwema wa taifa letu. Siyo siri swala hili limegubikwa na mambo mengi lkn mbaya na hatari inayoonekana ni kuibuka kwa kundi la watu linaloipinga katiba iliyopendekezwa.

Sina tatizo na kupingwa huko ola nina tatizo na sababu za kuipinga. Mfano wengi wanadai kuwa katiba pendekezwa imekiondoa kipengele cha uadilifu, si kweli kwani kipengele hicho kipo isipokuwa kiliondolewa kwenye Ibara inayohusu tunu za taifa na kuwekwa kwenye ibara ya maadili ya mtumishi wa umma. Kiukweli uadilifu siyo tunu kwa tafsiri yake bali ni swala la uadilifu.

Tunu ni kama vile Lugha ya kiswahili,amani, muungano n.k. Swala la katiba limeingiliwa na siasa kiasi kwamba watu hawajadili tena kwa uchungu wa kulinda misingi ya utaifa wetu bali kwa maslahi na kupata upenyo wa kisiasa.

Ninaamini kwa umakini wa Rais wetu atasimamia na hatimaye tutapata katiba yenye maslahi mapana ya historia ya taifa letu hasa Muungano, udugu na amani.

My take; Pamoja na mafanikio hayo wapo baadhi ya watanzania ambao wameendelea kubeza kwa namna yoyote ile. Baadhi yao wamediriki kukashifu kwa matusi na kumdhihaki Kikwete kwa lugha mbaya kabisa. Ni kweli hakuna binadamu aliyetimilika kwa kufanya bila kukosea.

Inawezekana katika utendaji wake kuna mahali amekosea hata hivyo sidhani kama anastahili kulaumiwa kiasi hicho. Ninawaambia ndugu zangu watanzania wenzangu, tutamkumbuka Kikwete siku moja!. Wanasiasa hasa wa vyama pinzani iko siku mtamkumbuka Kikwete!.

Waropokaji msio na staha katika kauli zenu mtamkumbuka Kikwete!. Na kwako Mheshimiwa Rais, nikusihi usokate tamaa, endelea kuchapa kazi kwani kama ni ng'ombe umebakiza kipande cha mkia tu!. Ulishawashinda tayari mbona!. Up to this moment, you are the winner Sir!.

Cha muhimu malizia kazi zako na Mungu Baba Mwenyezi atakulipa kwa kazi nzuri uliyowafanyia watanzania. Jifunze kwa Prof. Muhongo, aliyekuwa waziri wako ambaye pamoja na mazuri yote aliyoyafanya mwisho wa siku watanzania wasio shukurani walimwandalia manila na kumnyonga kisiasa hadharani!.

As you signing off Sir keepon praying for your nation ili kikombe cha siasa chafu ya wasaka madaraka hali mikono yao ikinuka rushwa, kiliepushe taifa kuingia kwenye machafuko.
 
Hovyo!!!!


Sawa bwana najua saa hizi mko Mbeya mnapanga mikakati ya kulazimisha matokeo uchaguzi mkuu 2015. Imekula kwenu!. Mtakutana sana!. Ninyi ni weupe peeee!
 
Watakuja watu kubeza hayo mafanikio. Mimi huwa nnawaambia wachanganye awamu zote waone kama Kikwete hajafanya zaidi ya wote.
Faiza hawana kitu hao. Jana walikuwa na vikao usiku vya viongozi wa kanda mbalimbali. Eti wanapanga kugomea matokeo 2015 na kuwaamuru redbrigade kufanya kazi za jeshi siku ya uchaguzi. In short wanataka kuingia msituni kuasi kwa kuwatumia redbrigade.
 
Faiza hawana kitu hao. Jana walikuwa na vikao usiku vya viongozi wa kanda mbalimbali. Eti wanapanga kugomea matokeo 2015 na kuwaamuru redbrigade kufanya kazi za jeshi siku ya uchaguzi. In short wanataka kuingia msituni kuasi kwa kuwatumia redbrigade.

Vp Albino, wakaombe hifadhi nje au hilo mnalipinga?
 
Faiza hawana kitu hao. Jana walikuwa na vikao usiku vya viongozi wa kanda mbalimbali. Eti wanapanga kugomea matokeo 2015 na kuwaamuru redbrigade kufanya kazi za jeshi siku ya uchaguzi. In short wanataka kuingia msituni kuasi kwa kuwatumia redbrigade.

Mimi huwa nnawaambia siku zote, kama ni wapinzani wa kweli na mnaitakia mema Tanzania, mtaonesha aliyoyafanya Kikwete kisha mtasema sisi tutafanya zaidi hiki na hiki na hiki, hivi na hivi na hivi. Hapo tutawaelewa. Lakini huu upinzani usio na la kufanya mimi nauona ni ujinga tu na si upinzani.
 
Hukuyapenda mafanikio ya Kikwete? au hovyo uliloona wewe ni lipi?

Mafanikio ya kushindwa kuwalinda albino na tembo? Au mafanikio ya kuiacha nchi na madeni mazito? Au mafanikio ya kuuza gesi ya Mtwara kwa Wachina ili Riz 1 asinyongwe? Au mafanikio ya kujenga lijumba la kifahari Msoga kwa hela za walipa kodi?
 
Umesema kweli, mazuri aliyofanya yanaonekana wazi tumpe haki yake!
 
Kwakweli rais wetu amefanya kazi kubwa sana,hadi kuweza kuziona billion 300 ni fedha za madafu amejitahidi sana???watu wamepigwa hadi kusokomewa vijiti kwenye nyeti zao(operation tokomeza)amejitahidi sana kuwakenulia wezi rais wetu mpendwa sio eti???Nashindwa kuelewa mnaposifu akili zenu huwa mnaficha kwapani au?
 
Watakuja watu kubeza hayo mafanikio. Mimi huwa nnawaambia wachanganye awamu zote waone kama Kikwete hajafanya zaidi ya wote.

Dada yangu. Hbari za leo. Mzee Mwinyi ana msemo mzuri ila sijui kama na yeye kautoa kwa mtu mwingine "Kila zama na kitabu chake" Hatuwezi kuangalia mafaniko ya Kikwete kwa kulinganisha na awamu zilizopita and that how to think beyond time and space. Lakini tukiangalia kwa kulinganisha na awamu zilizopita tunaweza tukajikuta Kikwete si lolote wala chochote maana unaweza ukakuta plans na financial resources ziliandaliwa na serikali zilizopita na hapo tukaanza ubishi wa kati ya kuku na mayai ni kipi kilianza? Tuangalie mafanikio ya Kikwete na tuyapime kutegemea na resources tulizojaliwa na kuona je kuna urari? Kama kuna kasoro kwenye hizi projects either architected or implemented by him tuseme na tutakuwa tumemtendea haki maana anaweza kurekebisha kabla ya kuondoka na kuweza kuiacha positive legacy. Lakini tukimpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa kila alilolifanya halina mawaa kesho akishatoka tutaanza kumwanika wakati haya mapungufu yalikuwepo na yeye alikuwa na uwezo wa kuyarekebisha. Mfano ni hili la katiba mpya na mapungufu. Yapo na mengi katika uadaaji wake na utekelezaji wake ambapo CCM wamelazimisha vitu ambavyo wenyewe wamekuwa na wanaendelea kuvilalamikia na ukiwauliza wanasema bunge la katiba lilikuwa mradi wa kula hela. Yaani nchi inawekwa rehani kwa maslahi ya chama kimoja sijui kwa faida ya kudumu au isyo ya kudumu. Kuna kashfa zilizojitokeza katika kipindi cha awamu na zimemalizwa kishabiki na kulindana kiasi kwamba taifa limejiandalia bomu litakalokuja kulipuka baadae. Nchi haina dira na maadili ya kitaifa(hili sio tatizo lake peke yake) na hili kidogo rasimu ya Warioba ilijaribu kulipatia ufumbuzi ingawa sio wa kimalaika lakini wajumbe walionyesha uzalendo mkubwa ilikuwa ni kuongezea uzito na kuzifanya kuwa sehemu ya katiba. Hayo ni kwa ufupi. Mbali na mafanikio yake lakini bado ana mapungufu tena mengi ambayo anaweza kuyatatua baadhi au kumwekea misingi chanya ajaye ili apate pa kuanzia
 
Back
Top Bottom