Jakaya Kikwete simkubali katika uongozi lakini maisha yake binafsi yananivutia sana(nayakubali)

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Sometimes unaweza kuwa unamchukia mtu lakini ukajikuta unacheka kwa hasira yenye majonzi.

Huyu jamaa ametufikisha pabaya sana nchi hii.lakini kutokana na mambo yake huwa najikuta kupenda kusoma sana habari zake.

Suala la uongozi simkubali kabisa na sipendi lakini napenda maisha yake nje ya uongozi kutokana na tabia zake yani:

1: Hana tabia ya kupanic mambo hata liwe jambo la kutisha vipi.

2: Ana subira sana (hana on spot decision)

3: Utani wa uswahilini na lugha anaimaster vizuri

4: Vidharau vyake na kejeli

5: Hayupo serious hata kwenye mambo mazito yenye userious yani yeye ni kutabasamu tu.

6: Anapenda utalii sana. Yaani kila siku safari ulaya tu. Anakula maisha.

7: Hata umtukane au umseme vibaya hakujibu na kama atakujibu basi kwa dharau sana na kukukejeli. Mfano Tundu Lissu analijua hili.

8: Anapenda starehe sana yani maisha ya ujana, hadi kuvaa.

9: Ukichunguza vizuri ana utozi fulani ukichanganya na uhandsome wake na uvaaji.

10. Ongea yake hasa kuwe kuna jambo kubwa la kitaifa. Lugha inambeba sana kwenye presentation.

11: Ushikaji wake kwenye mali za umma. Umewasevu sana masela ila jamaa ananyang'anya hadi sukari.

12: Ulitudekeza sana wapinzani hata Ikulu chai ilikuwa kawaida sana ila naona ikulu ya sasa haina sukari wala bomba la maji.

Tutakumis sana JK na wengine wameanza kujutia kwa huyu wa sasa JPM. Nimemisi kukuona unauza sura kwenye media basi uwe unaonekana hata kidogo masela wako wanakumisi sana.

Najua Msoga hakukaliki tena japo umemaliza upresidaa.

Nakutakia heri katika utalii huko ulaya

LIVE LONG JK. GOD BLESS YOU..
 
Huyu ni jamii ya wale aliowasema Jery Muro. Na kwa kawaida watu wa pwani they do not care much about life.
Hawana hasira kama watu wa bara. Watu wa pwani ni laissez-faire. Akipata dagaa, uono, bangala, kipande cha papa and the like maisha yanatosha. Siyo kujisumbua na nyama choma, ndafu, bia moja baridi, hapana.
Akipata ubwabwa wa nazi na ugali kwa mchunga anamalizia na mwanamke basi. Life is good!
 
Mhhhhhhh kadiri nilivyokuwa nazidi kusoma hii thread nilikuwa nashangaa kwanini hadi sasa iko hapa!
Au ndio zama zimepita?

Nami ngoja nikuunge mkono mtoa mada kwenye suala moja la kuhandle issues.
Hapa Kikwete yuko njema zaidi ya mrithi wake na hili halina ubishi.
Hakuwa mtu wa kukurupuka,bali masuala yalijadiliwa kwanza.
Ah,ndio hivyo tena....mabaya yanapozidi mazuri hata yale mazuri hayaonekani.
BTW...hii thread itamfurahisha kwa kiasi fulani FaizaFoxy
 
Kikwete ni Charismatic leader, Mwalimu alilijua hili, Lowasa alilitambua hili, Mkapa aliliona hili.
Ubovu wa Kikwete ni Usimamizi lakini ilipokuwa linakuja suala la kuonyesha Leadership, huyu mtu ni Kiongozi.

Halafu huyu mtu ni mwanajeshi, Kafundisha siasa jeshini. hawezi kubabaishwa na vi crisis vidogovidogo vya kisiasa.

Huyu mtu aliongoza Unification ya TANU na ASP zanzibar kutengeneza CCM upande wa Zanzibar, utambabaisha kwamba hajui siasa za nchi hii na CCM?

Huyu mtu alikuwa ana enlist watu kwenda vitani Uganda, anajua maana ya mapambano, uvumilivu na kusimamia unachokiamini.

Kikwete ana roho ya utu, ni binadamu kwelikweli, tumeona akifariji watu misibani, kwa vigogo hata watu wa kawaida, tumeona akiwatoa akina Diamond Platinumz na kuwapa platform ( Diamond alipata audience nchi nzima mwaka 2010 pale JK alipomuintegrate ktk timu ya waimbaji kwenye kampeni zake, before that Diamond alikuwa hajapata jina sana), Kuna kina Ray C wamesaidiwa na mzee ktk ishu ya madawa ya kulevya.

Bob Marley aliimba
" You can't miss the water, until your well runs dry.
No matter how you treat them, Men will never be satisfied"
 
Back
Top Bottom