Kumbe Jakaya Kikwete ni kiongozi mzuri sana, haya hakuyafanya pengine ana sababu za msingi sana!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Sasa nisiposema kwa kweli nafsi itaendelea kunisuta sana. Nauchukulia uongozi wa Jakaya Mrisho Kikwete enzi akiwa rais kama uongozi wa aina yake kuwahi kutokea Tanzania.

Ndiyo, na nakumbuka sana alipoingia tu madarakani mwaka 2005 mambo yalianza kwa uzuri kabisa, ashukuriwe huyu Kikwete aliyewazikiliza kina David Silinde waliogoma mwaka 2008 kwani mwaka mmoja baadaye yaani 2009 nilisoma bure kabisa na nakumbuka nilitia timu chuo nikiwa na Tshs 15000 mfukoni ila ile naingia tu nikaenda moja kwa moja pale UDBS nikapewa kitita cha Tshs 500000 mkononi na kuambiwa kuwa hizo ni fedha zako za matumizi kwa miezi miwili ya kwanza ukiwa chuo!

Nikajilipia na kwa mara ya kwanza nikaanza kujisomesha kwa ada ya Tshs 1500000 kwa mwaka! Sikuwahi kubughudhiwa! Mwisho wa kila mwaka wa masomo naingiziwa Tshs 620000 kwenye akaunti yangu kama fedha za PT! Hazikuwahi kutoka kwa mafungu wala kuchelewa! Kwa wazazi ilikuwa kusalimiana tu nakujuliana hali!

Hakuishia hapo, tuligoma tena mwaka 2012 kwa kudai madai ya nyongeza ya hela ya chakula na kwa kweli muhula uliofuata akatusikiliza mzee yule! Hela ikaongezwa bila bughudha wala kufukuzana chuo! Hakukuwa na porojo, makelele wala maneno mengi kutoka kwake!

Leo nani wa kufanya hivyo? Anayetuongoza mwenyewe anasema "nawategea tu mufanye kitu, mtaondoka wotee" huyo ndiye mtu tunayeamniniwa kuwa ni wa wanyonge. Hao kina Silinde na sisi tulimaliza chuo na matakwa yetu kusikilizwa. Nafikiri ingekuwa kwa huyu "tungepotezwa"

Huo ulikuwa tu ni utangulizi wa ule wimbo wa "Nitaondoka nitarudi kwa baba yangu na kumwambia kuwa nimekosa mbele yako na mbele ya Mungu wangu! Nimetoka kwako baada ya kushiba na kusaza nikaenda kijiweni nikasota na kuuona ukuu wako na moyo wako wa ajabu.

Ulinipa hadhi pamoja na ndugu zangu kwa utashi wako uliojaa busara na maamuzi yenye utu uliotukuka. Ulikuwa mvumilivu kwetu na hata pale tulipokichafua kiganja chako kwa kinyesi hukukikata bali ulikiosha na kuendeleza upendo kwetu mbali na kuwa tuliendelea kukichafua, hukuchoka kukiosha.

Mbali na utukutu pamoja na ukorofi wetu ulituenzi kama wanao wapendwa. Ulikuwa na uwezo wa kufanya lolote kwetu kutokana na mamlaka uliyopewa, lakini ulitambua kuwa mamlaka yako ilitoka kwetu na kuamua kututumikia kwa moyo mmoja na upendo wa hali ya juu. Hukupiga kelele na kutoa vitisho, hukusema sana nje bali ndani ya moyo wako.

Zaidi nasema kuwa "Namshukuru Mungu baba mfalme wa Mbingu na Nchi yeye aliyenijaalia kufaidi mema ya nchi hii ndani ya kizazi chako. Kwa hakika leo naona kama muujiza wewe kuyafanya hayo. Namuomba Mungu baba akujalie nyongeza ya maisha mema na marefu yenye ziada ya hekima, busara na utu kama alivyokujalia hapo kabla, na mwisho akujalie maisha mema mbele ya kiti chake cha enzi.

Mema uliyotenda kwetu ni ya hali ya juu sana na kwa hakika thamani yake tunaiona kwa ndugu zetu wanaolilia walau sehemu ya wema kama huo ila imekuwa vigumu mno kuipata.. Wasalaam tena mzazi wangu na mlezi wangu wa mfano Jakaya Mrisho Kikwete. Ninatoa shukrani sana kwako na la muhimu ninalosema leo ni kuwa "Mungu akubariki sana kwa utumishi wenye unyenyekevu wa hali ya juu uliotuonyesha"

Sasa turudi kwenye mada.
Kwa kutambua uajabu wa Kikwete kwa kweli nimeanza kumuona mwerevu sana na mambo ambayo hakuyafanya kwa kweli alikuwa na makusudi yake na alipiga hesabu sawasawa na pengine siyo mkurupukaji kabisa. Alikuwa na maana kubwa kwenye akili yake!

1) Sitaki kuamini kuwa Kikwete alikosea kutoifufua ATCL, kwa kweli huenda alipiga hesabu za kibiashara na uendeshaji akaona haina haja ya kushindana na kina fast Jet ama PW! Kikwete angeshindwa kweli kununua tundege tuwili kama Magufuli? Hapana alikuwa na sababu ya msingi kabisa. Tungoje muda uongee. Hapana, haiwezekani JK apate sifa kote huko ashindwe kupata sifa kwenye ATCL ambako angefanya tu kwa visiku vichache.

Nakumbuka kuhusu MRI ya Muhimbili, Kikwete aliposikia kuwa Magufuli mbiombio katoa mabilioni ya kuifanyia ukarabati akaishia tu kucheka na kutoa pongezi. Kweli baada ya muda yakaonekana! Mabilioni yakaenda na maji kumbe plan ilikuwa ni kununuliwa MRI mpya na tufedha alizomega Magufuli ilikuwa ni makusanyo. Muda ukaongea.

2) Sitaki kuamini kuwa Kikwete alishindwa kukimbilia Dodoma mbiombio kama ambavyo inafanyika sasa. Alipiga hesabu akaona biashara haimlipi, akatulia kuboresha Dar. Hapa tena baada ya muda tutasema.. muda ndiyo kila kitu.

Nasema hivyo kwa kuwa sakata la mbiombio la sukari muda umeshaongea tayari.

3) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakuipenda CCM kuliko Magufuli kiasi cha kutowateua makada wake kuwa DEDs na DAS. Alipiga hesabu akaona kufanya hivyo ni ujinga... miiko ya urais inakataza, akawajaza kwenye U-DC kama katiba zao zinavyosema. Kwa hakika alionyeha dhahiri kujitambua kiuongozi.

4) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakumpenda Nape Nnauye kuliko Magufuli kiasi cha kutokumpa ubunge na baadaye ampe wizara, aliona mahali panapomfaa na akamtimizia.. Magufuli amempenda Nape Nnauye sasa tumeona matokeo yake! Hatimaye Nape amekuwa sumu nyingine nchini.

5) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakuuona umuhimu wa mifuko ya jamii kuwekeza kwenye viwanda, alipiga hesabu akaona jinsi sekta ya viwanda inavyosuasua akaona kuwaingiza hawa na kuwalazimisha ni sawa na kuvaa bomu kwa kujitakia akaona kuwa mambo yao na fedha za wananchi wajuane wenyewe jinsi watakavyofanya. Huyu kiongozi wetu mpendwa anatoa miezi mitatu kuishinikiza mifuko kujenga viwanda jambo ambalo ni la hatari kwa taifa.

6) Mbali na maandamano na kusemwa kwa kila namna JK aliruhusu uwazi. Hakuliziba bunge achilia mbali bunge hilohilo kutumika kumchanachana kila bunge linapokaa. Hakuagiza ni yapi yajadiliwe. Aliruhusu mijadala ya katiba, makongamano ya kisasa na bado akaweza kuleta Maendeleo kwa kiasi chake. Alisemwa kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kunung'unika wala kupiga makelele. Aliongeza mishahara, akaongeza na wana taaluma pia. Ikiwemo tuliosoma bure kama sisi (bure isiyo na maneno mengi wala karaha)

Kiongozi wetu wa sasa mbali na kusema kuwa yeye ni mtu wa watu nasikitika kusema kuwa kila kitu ni kinyume kabisa na miezi kadhaa tu tangia aondoke JK mambo yote ni tofauti kuanzia kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hakuna tena uwazi, tumeingia kwenye uchama hadi kwenye kazi za kila siku. Siasa za kubaguana kiitikadi zinahubiriwa waziwazi akiziongoza yeye!

Kwa kweli mwezi wa kumi na mbili nafunga safari kwenda Msoga nikaonane na Kikwete kumfikishia salamu pamoja na kuteta naye....!
 
Sasa nisiposema kwa kweli nafsi itaendelea kunisuta sana. Nauchukulia uongozi wa Jakaya Mrisho Kikwete enzi akiwa rais kama uongozi wa aina yake kuwahi kutokea Tanzania. Ndiyo, na nakumbuka sana alipoingia tu madarakani mwaka 2005 mambo yalianza kwa uzuri kabisa, ashukuriwe huyu Kikwete aliyewazikiliza kina David Silinde waliogoma mwaka 2008 kwani mwaka mmoja baadaye yaani 2009 nilisoma bure kabisa na nakumbuka nilitia timu chuo nikiwa na Tshs 15000 mfukoni ila ile naingia tu nikaenda moja kwa moja pale UDBS nikapewa kitita cha Tshs 500000 mkononi na kuambiwa kuwa hizo ni fedha zako za matumizi kwa miezi miwili ya kwanza ukiwa chuo! Nikajilipia na kwa mara ya kwanza nikaanza kujisomesha kwa ada ya Tshs 1500000 kwa mwaka! Sikuwahi kubughudhiwa! Mwisho wa kila mwaka wa masomo naingiziwa Tshs 600000 kwenye akaunti yangu kama fedha za PT! Hazikuwahi kutoka kwa mafungu wala kuchelewa! Kwa wazazi ilikuwa kusalimiana tu nakujuliana hali!

Hakuishia hapo, tuligoma tena mwaka 2012 kwa kudai madai ya nyongeza ya hela ya chakula na kwa kweli muhula uliofuata akatusikiliza mzee yule! Hela ikaongezwa bila bughudha wala kufukuzana chuo! Hakukuwa na porojo, makelele wala maneno mengi kutoka kwake! Leo nani wa kufanya hivyo? Anayetuongoza mwenyewe anasema "nawategea tu mufanye kitu, mtaondoka wotee" huyo ndiye mtu tunayeamniniwa kuwa ni wa wanyonge!

Huo ulikuwa tu ni utangulizi wa ule wimbo wa "Nitaondoka nitarudi kwa baba yangu na kumwambia kuwa nimekosa mbele yako na mbele ya Mungu wangu! Nimetoka kwako baada ya kushiba na kusaza nikaenda kijiweni nikasota na kuuona ukuu wako na moyo wako wa ajabu"

Sasa turudi kwenye mada!
Kwa kutambua uajabu wa Kikwete kwa kweli nimeanza kumuona mwerevu sana na mambo ambayo hakuyafanya kwa kweli alikuwa na makusudi yake na alipiga hesabu sawasawa! Pengine siyo mkurupukaji kabisa! Alikuwa na maana kubwa kwenye akili yake!

1) Sitaki kuamini kuwa Kikwete alikosea kutoifufua ATCL, kwa kweli huenda alipiga hesabu za kibiashara na uendeshaji akaona haina haja ya kushindana na kina fast Jet ama PW! Kikwete angeshindwa kweli kununua tundege tuwili kama Magufuli? Hapana alikuwa na sababu ya msingi kabisa. Tungoje muda uongee!
2) Nakumbuka kuhusu MRI ya Muhimbili, Kikwete aliposikia kuwa Magufuli mbiombio katoa mabilioni ya kuifanyia ukarabati akaishia tu kucheka na kutoa pongezi. Kweli baada ya muda yakaonekana! Mabilioni yakaenda na maji kumbe plan ilikuwa ni kununuliwa MRI mpya na tufedha alizomega Magufuli ilikuwa ni makusanyo. Muda ukaongea.

3) Sitaki kuamini kuwa Kikwete alishindwa kukimbilia Dodoma mbiombio kama ambavyo inafanyika sasa. Alipiga hesabu akaona biashara hamlipi, akatulia kuboresha Dar. Hapa tena baada ya muda tutasema.. muda ndiyo kila kitu.
4) Nasema hivyo kwa kuwa sakata la mbiombio la sukari muda umeshaongea tayari.
5) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakuipenda CCM kuliko Magufuli kiasi cha kutowateua makada wake kuwa DEDs na DAS. Alipiga hesabu akaona kufanya hivyo ni ujinga... miiko ya urais inakataza, akawajaza kwenye U-DC kama katiba zao zinavyosema.

6) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakuipenda Nape Nnauye kuliko Magufuli kiasi cha kutokumpa ubunge na baadaye ampe wizara, aliona mahali panapomfaa na akamtimizia.. Magufuli amempenda Nape Nnauye sasa tumeona matokeo yake!
7) Sitaki kuamini kuwa Kikwete hakuuona umuhimu wa mifuko ya jamii kuwekeza kwenye viwanda, alipiga hesabu akaona jinsi sekta ya viwanda inavyosuasua akaona kuwaingiza hawa na kuwalazimisha ni sawa na kuvaa bomu kwa kujitakia akaona kuwa mambo yao na fedha za wananchi wajuane wenyewe jinsi watakavyofanya.

Kwa kweli mwezi wa kumi na mbili nafunga safari kwenda Msoga nikaonane na Kikwete kumfikishia salamu pamoja na kuteta naye....!
Wapigaji utawajua tu, maana mebanwa kila kona sasa mnakuja na ngonjera za kukumbuka Jakaya Kikwete
 
Pia kumbuka wakati wa Kikwete uchumi ulikuwa unakua kwa zaidi ya asilimia saba. Huyu jamaa hata mwaka bado ajira zimekufa kila kona na uchumi umeporomoka kwa mwendo kasi, yeye bado anateua tu makada wakajifunzie mbele kwa mbele namna ya kuleta maendeleo. Tuliwaambia wakati wa uchaguzi kuwa hulka za huyu jamaa zinafahamika mkaleta ubishi wenu
 
JK ana roho ya utu, ni binadamu sana!
Zungu la roho, hana noma,wala nongwa na mtu.

Baada ya kumkata Lowasa, ona alivyompa uhuru, nafasi hata ulinzi wa kufanya mikutano yake ya kampeni bila kumsumbuasumbua.

Angekuwa kiongozi mwingine mwenye kupenda ubabeubabe Lowasa asingepewa uhuru ule wa kuzunguuka nchi nzima raha mustarehe ili kupiga kampeni ya kuing'oa CCM madarakani!
 
Kikwete mheshimiwa alikuwa amesomea uchumi na alikua na exposure nje ya nchi na vijijini ndani alikoanzia kazi. Aliongea kwa hekima,hakujishusha wala kujipandisha...japo kunavilivyoyumba lakini ndio ubinaadam,alilenga maisha bora kwa kilamtz,alijenga wafanyabiashara wakubwa na wakati,alijenga wasanii na wanamichezo,alijenga wasomi,demokrasia na wapinzani kiukweli alijitahidi asijenge "mashetani" eti watu waishi Kama mashetani!!! Hakuweka vinyongo hâta na waliomsakama,hâta mimi mtu wakawaida nlijenga nyumba,saivi sidhani Kama ntajenga hâta choo. Kwasasa sijajua wanajengwa kinanani labda tusubiri tutajaona japo nyota njema...
 
Kikwete mheshimiwa alikuwa amesomea uchumi na alikua na exposure nje ya nchi na vijijini ndani alikoanzia kazi. Alijenga wafanyabiashara wakubwa na wakati,alijenga wasanii na wanamichezo,alijenga wasomi,demokrasia na wapinzani kiukweli alijitahidi asijenge "mashetani" eti watu waishi Kama mashetani!!! Saivi sijajua wanajengwa kinanani labda tusubiri tutajaona japo nyota njema...
Kweli Kikwete ataishi daima.
 
Back
Top Bottom