comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
Jina lake ni Jakaya Mrisho Kikwete,ni Mh Rais mstaafu wa awamu ya nne katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanajeshi mstaafu kwa cheo cha Luteni kanali, mwanadiplomasia mahiri mno mwenye macho ya kung'amua yatayotokea katika diplomasia mbalimbali kidunia.
Miongoni mwa Rais waliohudumu na kudumu mno katika Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa akiwa waziri wa wizara hiyo, hivyo kumuwezesha kusoma diplomasia za kimataifa zaidi na zaidi, ujanja wa diplomasia za uchumi na ulinzi duniani kwa umakini sana, aidha, ni moja ya viongozi walioiangalia jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makini mno akitumia uzoefu wake kijeshi na kidiplomasia kusoma nchi wanachama na janja zao katika diplomasia ya kiuchumi na kiulinzi.Hongera Jakaya Kikwete Mungu akupe nguvu zaidi.
Jakaya Kikwete ni Mtanzania pekee kiongozi mkuu aliejumuishwa katika mikakati ya Helsinki kuhusu utandawazi na demokrasia duniani, kwa kutambua umuhimu wa diplomasia na amani Jakaya Kikwete mnamo tarehe 26/5/2013 alieleza kwenye kikao cha umoja wa nchi za Afrika kwamba ili nchi ya Kongo iwe na amani ya kudumu ni vyema kabisa Rais wa Uganda, Rais wa Rwanda na Rais wa Kongo- Kinshasa wakae chini na vikosi vya waasi kama vile Allied for Democratic Force For Liberation of Uganda na Democratic Forces for Liberation of Rwanda kwa kifupi ADF wamalize tofauti zao kuhusu Kongo, ni msukumo wake wa diplomasia ya amani ambayo haikuwapendeza baadhi ya viongozi husika.
Mawazo yake yangefanyiwa kazi basi amani ya Kongo ingetengemaa kabisa, Aidha, kwa kutambua umuhimu wa amani Maziwa makuu Mh Jakaya Kikwete alifikiria na kuruhusu vikosi vyetu vya majeshi vikalinde amani nchini Kongo na kwa umahiri wa majeshi yetu kikundi cha M-23 kilifurumishwa na kusambaratishwa vibaya sana. Hongera Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mafanikio ya Mh Jakaya Kikwete katika anga la diplomasia ya kimataifa yalikua hivi:-
Mwaka 2007 alitunukiwa nishani ya amani ‘Most Excellent Order of the Pearl of Africa’ nchini Uganda.
Mwaka 2009 alitunukiwa nishani ya amani ‘Order of the Green Crescent of Comoros’ nchini Comoro
- Alishirikiana na rais wastaafu Mh Benjamin Mkapa na Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa wa wakati huo Mh Koffi Annan kunusuru malumbano makubwa ya serikali ya Kenya yalisababishwa na matokeo tata ya uchaguzi wa mwaka 2007 hivyo kufanikiwa kushawishi kuundwa kwa serikali ya pamoja kati ya Rais Mwai kibaki na Raila Odinga.