Jakaya Kikwete - Baba wa Katiba Mpya



Nani anastahili heshima ya "Baba wa Katiba Mpya" Tanzania?

03/06/2013
2 Comments


7105249.png
Kilio cha Katiba Mpya ni wimbo ulioanza zama za miaka ya uanzishwaji wa vyama vingi. Pamoja na kuimbwa sana na miongo kadhaa kupita bila mafanikio, alhamudulillah walau sasa tunaweza kuanza kutandika majamvi tukiamini pilau la Katiba Mpya linakalibia kuliwa.

Nimejaribu kujihoji kwamba tutakapokuwa tumeipata hiyo Katiba Mpya, nani haswa atastahili kuvaa joho la kihistoria na kuenziwa kama Baba wa Katiba Mpya? Majibu yangu yote yananiacha katika mtanziko na hivyo basi sina budi kuwashirikisha wanajukwaa swali langu na matanziko wangu ili wanitanzue.

Ninaowawaza kustahili heshima hii ni wafuatao:

Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete: Huyu suala la Katiba Mpya halikuwemo kabisa katika agenda zake na wala katika Ilani ya chama chake. Lakini kwa kusoma matakwa ya Wananchi na kwa kuuelewa vema upendo wa kisiasa uliovumishwa mara tu baada ya matokeo ya 2010, alitumia vema hotuba yake ya kwanza katika ngwe ya pili kuichukua hoja hii ya Katiba Mpya. Dr. Jakaya alifanya hivyo kwa kukabiliana na upinzani mkali ndani ya chama na serikali yake. Pamoja na yote akasimama na kushinda kuhakikisha mchakato wa Katiba Mpya unapata ridhaa za kiitifaki ndani ya chama chake. Baada ya mchakato kuanza, kumekuwepo na msukumo wa wanasiasa wanaojiandaa na mchakato wa Urais 2015 kutaka CCM iingilie na kumiliki mchakato mzima wa Katiba Mpya. Hawa wanayafanya haya kwa maslahi yao binafsi na sijajiridhisha pahala popote kwamba JK anamtuma mtu au kuunga mkono najisi yoyote katika mchakato wa Katiba. Mengi ya yanayofanya kinyume yanafanyika kwa kuzungukana ndani ya chama. Labda kosa la JK ni ile tabia yake ya kukubali kushuhudia jambo au mambo yakinajisiwa pasipo kukalipia au kuchukua hatua. Nimejiridhisha mchakato wa upatikanaji wa Wajumbe wa Mabalaza ya Katiba Mpya ambao CCM ilifanya umafia kuingiza wajumbe wengi haukuwa na Baraka za JK. Hivyo kwa nilivyojiridhisha juu ya dhamira safi ya Rais JK kutoingilia mchakato wa Katiba Mpya na badala yake kuwa na kiu ya kweli kuona tunapata Katiba safi nimedhani anastahili kuwa Baba wa Katiba Mpya.


!


764419520.jpg
Jaji Sinde Warioba: Kama Mwenyekiti wa Tume atakapokuwa amefikisha jahazi alilopewa pwani kwa usalama, atakuwa ameshinda majaribu mengi na amekumbana na mikasa lukuki. Lazima atakuwa kwa vyovyote vile amewahudhi wakuu wake waliompa kazi na vile vile atakuwa amewakasirisha wanaharakati na wanasiasa waliotaka kumwendesha puta hasa wale wa kutoka Visiwani. Hadi sasa Jaji Warioba ameonyesha msimamo na hekima za hali ya juu katika kusuluhisha matatizo na kukabiliana na changamoto zilizoifika Tume yake. Haikuwa kazi ndogo kukusanya maoni na kisha kuyatathmini na kuandaa rasimu. Sura inayotoka ndani ya rasimu inadhihirisha jinsi Jaji Warioba alivyoweza kujiweka kati na huru katika kusimamia jukumu la Kupata Katiba Mpya; iliyo bora na inayotokana na matakwa ya Wananchi wa leo na kwa kipindi cha miongo michache ijayo. Nikiyajumuhisha haya yote sisiti kuliteua na kulipendekeza jina la Jaji Joseph Sinde Warioba miongoni mwa Watanzania wanaostahili kufikiriwa kupewa nafasi hii ya Baba wa Katiba Mpya.

Wako wengine waliojaribu kuibeba ajenda hii lakini wakakwama njiani. Si vibaya nao tukawatafutia njia sahihi ya kukumbuka michango yao. Miongoni mwao ni Mch. Mtikila. Sina kumbukumbu ya mtu mwingine aliyewahi kuhubiri Katiba mpya kwa nguvu na kwa muda mrefu zaidi ya Mtikila.

Wapo wengine wamekuwa wahubiri wa Katiba mpya kwa mtazamo wa vipengele vya kiimani, kiitikadi au kwa malengo binafsi. Hawa mtanisamehe kwa kutowatambua katika hoja ya nani anastahili kuwa Baba wa Katiba Mpya? Naamini Baba anapaswa kuwa mzazi/mtu asiye na ubaguzi!

Dr. W. Slaa: Akiwa mpeperusha bendera ya CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2010, Dr. Slaa aliinadi vema agenda ya Katiba Mpya ikiwa ni sehemu ya Ilani ya Chama chake. Dr. Slaa akiwakilisha CHADEMA aliahidi kuhakikisha mchakato wa Katiba mpya unaanza ndani ya siku 100 baada ya uchaguzi. Nisilolikumbuka vema ni kama alimaanisha kuwa ahadi hii ingetekelezwa hata bila kuingia Ikulu au lah! Lakini ninachojua na kinachoshuhudiwa na Watanzania wote sasa, ni kwamba Dr. Slaa hakuingia Ikulu bali mchakato wa Katiba Mpya ulianza katika kipindi kilichoahidiwa. Dr. Slaa na CHADEMA hawakuishia hapo. Wameendelea kuiumba Katiba Mpya kupitia mashinikizo mbalimbali na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ambayo karibu mara nyingi, hata kama hawakupata chote walichoshinikiza kupata, basi walipata bilauri iliyojaa zaidi ya nusu! Hata sura ya ujumla ya rasimu inayosomwa leo hivi sasa inaonyesha kwa kiwango kikubwa kuakisi matakwa ya Wananchi yaliyokuwa yakishinikizwa na viongozi wa CHADEMA kuwemo kwenye Katiba Mpya. Na hili sasa ni mtego kwa CHADEMA ambao walikwisha tangaza kususia mchakato! Hivyo ukiangalia kwa tathmini ya ndani na bila kiwewe utapata shida sana kushindwa kusema kuwa: Mchakato wa Katiba Mpya "UMECHAGIZWA" na CHADEMA wakimtumia Dr. Slaa. Tume ya Katiba Mpya ilipewa hadidu za rejea na Rais lakini imefanya kazi kwa kufuata matakwa ya Wananchi yalioshinikizwa kupitia CHADEMA. Ukweli huu unanishawishi kuikubali historia ya kuwa Katiba Mpya imechagizwa na CHADEMA na aliyefanya vema jukumu la kuchagiza ni Dr. Slaa na hivyo sioni ninsi gani nitamuengua kuwa Baba wa Katiba Mpya!

Prof.Lipumba:
Akiwa ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kati ya mwaka 205 hadi 2010, LIpumba na chama chake cha CUF alitetea sana hoja ya uwepo wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na daftari la kudumu la wapiga kura. Leo hii tunaona mchakato wa kupata katiba mpya ukiwa mezani ktk hatua za mwisho na uchaguzi ujao utafanyika chini ya katiba hiyo mpya..

Hongera watanzania kupata katiba mpya;

Karibuni kuchangia!



Source: Nani anastahili heshima ya "Baba wa Katiba Mpya" Tanzania? - wavuti.com



 
jk ndiyo mwenye hadhi hiyo wengine hawa ni wasaidizi ambao waliagizwa na jk wafanyie kazi maagizo yake pia jk alikuwa na nafasi ya kukataa bila yeye kuamua kuifanyia kazi isingekuwepo.
 
matokeo halisi ya kura za urais 2010 ndIyo chachu ya katiba mpya.
 
Nataka sehemu yoyote ambayo ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 iliandika kuhusu Katiba mpya - if NOT then wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CDM. so credit has to go to CDM and DR.Slaa kama mpiganaji numberi one.
 
Nakumbuka CHADEMA walivyokomaa wakati ule, nawapa HEKO iwapo Katiba mpya itapatikana kweli.
 
mboye uko wapi natimu yako yenye uweledi na si ya jk ambayo haina uweledi, mbona umeingia mitini, jk big up, mtu asiyetetereka na kalele zisizokuwa na maana, tutakukumbuka daima
 
Hii hongera kwa JK ni ya kinafiki. Yeye na watu wake hawakuwa radhi kuandika katiba mpya, lakini wananchi waliposhinikiza, ilibidi asalimu amri. Huyo ni mateka na wala sio shujaa. Hongera za dhati ya kuandika katiba inastahili kwenda kwa wananchi. Ni budi tuelekeze sifa kwa anaestahili sio sifa za kinafiki.

rais hafanyi kazi kwa kushinikizwa katika hilo umejidanganya tafakari upya hauko sahihi.
 
Hapa bila kuuma meno sifa zote ziwaendee cdm hili suala lilikuwa lao na walihubiri kila walipopanda jukwaani na hata JK aliposema kuwe na katiba mpya chama chake kilimjia juu kwa kucheza ngoma isiyo yao,swali la kujiuliza ni je katiba hii itatupa tume huru kama tutakavyo? kujaribu kujibu hilo swali ni kuwa hakuna baba wa katiba ila tutawapongeza kila mtu kwa sehemu yake.
 
penye ukweli uongo hujitenga ukiangalia kwa umakini sana jawabu unaweza kuwa nalo mtoa hoja(mpembuzi) amepembua vizuri sana na jawabu linapatkana hapo hapo
 
hongera vyama vya upinzan,taasisi za kijamii na haki za bnadamu kwa kuwapresha serikali ya sasa kuandaa katiba mpya bila nyie isingeandaliwa
Pongezi kwa Mkuu wa Nchi aliyekubali kusikia kilio cha watu wke, kwani angekataa mngefanya nn? hatakama kungekuwa na maafa lkn kakataa, lkn huyu anastahili pongezi nyingi sana kwa katiba nzuri ijayo.
 
Ushabiki ni ugonjwa mkubwa

Sasa umeshasoma ukajua kilichoandikwa? Au mradi kaandika tu?
 
Back
Top Bottom