Jakaya Kikwete - Baba wa Katiba Mpya

Jakaya Kikwete - Baba wa Katiba Mpya

moma2k

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2010
Posts
1,109
Reaction score
1,423
Ni ukweli usiobishaniwa kuwa J.Kikwete ni baba wa katiba mpya hapa Tanzania.
Kama kweli katiba mpya itapatikana.
Kama kweli katiba mpya itapatikana kwa haki na amani.
Kama kweli katiba mpya itapatikana bila kuingiliwa na ushabiki na masilahi ya CCM.
Kama kweli katiba mpya haitakuwa na mapungufu yaleyale yaliyomo kwenye katiba ya sasa.
Kama kweli katiba mpya haitaingiza "udini" ndani ya katiba hiyo.
Kama kweli katiba mpya itapunguza madaraka ya kifalme ya raisi.
Kama kweli katiba mpya italiongezea nguvu BUNGE katika kuisimamia serikali.
Kama kweli katiba mpya itaiweka huru tume ya uchaguzi.
Kama kweli katiba mpa itapunguza viongozi wa kuteuliwa na raisi.
Kama kweli katiba mpya itampa madaraka makubwa zaidi ya kiuamuzi waziri mkuu.
Kama kweli katiba mpya itamuondoa raisi katika kuwateua majaji.
Kama kweli katiba mpya itamuondoa raisi katika kumteua katibu mkuu wa BUNGE.
Kama kweli katiba mpya itawafanya wakuu wa mikoa wachaguliwe na moja kwa moja na wananchi.
Kama kweli katiba mpya itapunguza baaraza la mawaziri ni kuweka idadi maalum.
Kama kweli katiba mpya itaondoa au kuweka kikomo cha ubunge kwa viti maalum.
Kama kweli katiba mpya itaweka bayana kikomo cha mtu kuwa mbunge.
Kama kweli katiba mpya itatoa mfumo sahihi wa Muungano wanaoupenda wananchi walio wengi, yaani serikali tatu.
Kama kweli katiba mpya itakuwa kweli ya imetoka kwa wananchi, na kwa masilahi mapana ya wananchi.
BASI KWELI: Jakaya Mrisho Kikwete atastahili kuitwa "BABA WA KATIBA MPYA" hapa Tanzania. Kama itakuwa hivyo, basi napendekeza ijengwe sanamu yake katika viunga vya BUNGE huko Dodoma akiwa ameshika kitabu cha KATIBA MPYA, ili iingie vizuri kwenye historia ya nchi hii vizazi kwa vizazi.
 
Usiwe na mashaka na katiba mpya. Iwe Isiwe Itapatikana. Katika hili hakuna ujanja.
 
Lakini hakuna wazo lake hata moja tutakalo liconstitute.
 
Kama hawatachakachua maoni yetu juu ya katiba tunayoitaka!
 
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.
 
Presha ndo imeleta haya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hongera vyama vya upinzan,taasisi za kijamii na haki za bnadamu kwa kuwapresha serikali ya sasa kuandaa katiba mpya bila nyie isingeandaliwa
 
Itakapokamilika huku imekidhi haja za watanzania bila undue influence, Anastahili kupewa pongezi zote, hakuna longolongo.
 
Stop being the captive of your own ignorance
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.
 
Hii katiba ya shirikisho bado inaacha maswali mengi na utata mwingi. Hao washirika hasa Tanganyika wanabaki katika hali gani? Naona safari ya katiba bado ndefu sana.
 
Kama ninavyokumbuka, wakatiwa kampeni za uchaguzi wa uraisi wa mwaka 2010, ni Dr, Slaa ambaye alitoa ahadi kuwa kama akichaguliwa kuwa raisi, ataanza mchakato wa kuandika katiba mpya ndani ya siku 100. Jambo hili lilipingwa sana na viongozi wa serkali ya ccm. Nilimwona kwa macho yangu, waziri wa sheria wa wakati huo, celina Kombani akipinga jambo hilo. mwingine aliyekuwa anapinga uandikwaji wa katiba mpya alikuwa ni mwanasheria mkuu Werema, kama sikosei. Ni baada tu ya kuona kwamba wananchi, CDM na vyombo vingine vya jamii vimepania kuwepo kwa katiba mpya, ndipo rais Kikwete, akatangaza kuwa pawepo na katiba mpya.

Mimi nashangaa kwa nini watu wengine wanachukulia wananchi kuwa ni mazezeta ambao hawana kumbukumbu wala hawajui ni kitu gani kinachoendelea? Ama ni mbinu ya kupindisha uongo ili uonekane kuwa ni ukweli? Hata hivyo, kwa hali ya kawaida, ukweli unajitokeza siku zote. Ni Dr. Slaa pamoja na CDM ndio waliotoa wazo la katiba mpya na ccm walikuwa wanalipinga.
 
ni aibu kubwa kwa mtu mzima kuwa muongo slaa alitoa ahadi moja tu kuwa atahakikisha nchi haitawaliki wala hausiki na katiba mpya yeye anachochea vurugu tu keshaisha ndo basi tena.
 
Mnakurupuka. Unataka watu waamini kuwa ameruhusu katiba iandikwe kwa hiari au kwa kupenda? Mnasahau kuwa amelazimishwa na nguvu ya wanaojua kuwa katiba iliyopo inawaonea. Asingeweza kuruhusu kwa utashi wake. Ni vema tuwakumbuke na kuwathamini waliotia pressure katika hili.
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.
 
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.

Hii hongera kwa JK ni ya kinafiki. Yeye na watu wake hawakuwa radhi kuandika katiba mpya, lakini wananchi waliposhinikiza, ilibidi asalimu amri. Huyo ni mateka na wala sio shujaa. Hongera za dhati ya kuandika katiba inastahili kwenda kwa wananchi. Ni budi tuelekeze sifa kwa anaestahili sio sifa za kinafiki.
 
Katika mchakato wa kuandika katba mpya RAIS JAKAYA KIKWETE ameandika historia mpya. kikwete ana sitahili kupongezwa na atakumbukwa daima.

Hili ni TUSI kwa watanzania kwani JK hajaamua kwa hiari yake kuandika katiba .Hili ni shinikizo lililotokana na kauli mbiu ya CHADEMA ya uchaguzi mkuu 2010 kuwa wakichukua nchi kitu cha kwanza ni kuandika katiba mpya. Inteligensia ya JK ilimwambia wingi wa kura alizopata Dr. Slaa na kumshusha JK hadi 61% zimetokana na hiyo slogan ya Kusudio la kuandika Katiba. WaTZ tusiifumbie historia macho kwa sababu ya ushabiki. hapa wa Kupongezwa ni CHADEMA na si JK kwani ametekeleza kauli mbiu ya CHADEMA na ikumbukwe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 CCM katika Ilani yake haikuwa na kitu kinachoitwa Katiba mpya. Mtoa mada acha unafiki!!!
 
Presha ndo imeleta haya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

presha ilikuwepo miaka yote hata kabla ya jk kuingia madarakani.alikuwa na uamuzi wa kuiacha hii iliyopo iendelee.me binafsi jana nilifurahia lakini sasa wakati wadau wameanza kuleta yaliyomo kwenye hiyo rasimu ya katiba humu jukwaani nimeanza kupata mashaka.
 
Lazima kumpa hongera my rais alikuwa na uwezo wa kukataa vyama vya upinzani vipo kwa ajili ya wananchi kukosoa sera za chama tawala sasa rais anapofanya jambo Zuri kwa manufaa ya umma anastahili pongezi
 
Acha turudi nyuma zaidi. Suala la Katiba mpya liliibuliwa huko nyuma na kupaziwa sauti sana na aliyekuwa Mwenyekiti wa DP Mhe Christopher Mtikila miaka ya 1990s. Akiwa mmoja wa Watanzania jasiri alilisemea sana kupitia kanda zake na alimlaumu sana marehemu J K Nyerere kwa kile alichokiita yeye utawala wa aian ya "AUTOCRACY" na kusisitiza kuwa mabadiliko ya msingi lazima yatokee kwenye Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom