Jakaya Kikwete - Baba wa Katiba Mpya

Pongezi zangu za dhati kwa Dr Slaa, chadema, wanaharakati na watanzania wenye nia ya dhati juu ya mustakabali wa Tz yetu
 
The entire process was collaborative, why exalt one person? In this age?

For political reasons, Watanzania tumekuwa watu wa kushinikizwa kwamba kuna watu fulani ndio walio shape mambo nchini mwetu. Angalia historia ya uhuru wetu - kwa sehemu kubwa sana anatajwa mtu mmoja tuuu mpaka ina bore!

Hata hivyo ni vema tukubali michango ambayo ilikiuwa prominent kwenye issues mbalimbali including Katiba mpya.

Ha ha ha ha, siezi kusaliti hata Ziwa Nyasa likienda Malawi lote

Kwa sababu umenisaliti ukahamia kwenye mastress. Unataka kuwa diwani au mbunge wa viti maalum? Ntakufuata mjengoni, sipendi usaliti.
 
BADO. kikwete ana sitahili kupongezwa sababu kuanzia Raisi MWINYI, MKAPA hoja ya kuwepo na katiba mpya ili zungumzwa lakini wameshindwa kuchukua hatua hivyo Raisi JAKAYA KIKWETE name subutu na ameweza na anasonga mbele.ana sitahiri kupongezwa.
 
safi sana raisi wangu kikwete mimi ni mpinzani ila kwa hili nakuunga mkono

hongera sana muheshimiwa rais

Nilifikiri wapongezwe CHADEMA kwa kususia hotuba yake kutaka katiba mpya. Ni hawa CHADEMA waliokwenda kukaa na Rais Ikulu na kumtamkia kwamba hawatamtambua hadi hapo atakapokubalia kuandika katiba mpya. Inashangaza kwamba leo tunapongeza juhudi za Kikwete pasipo kuangalia juhudi za CHADEMA katika hili. Binafsi naweza kusema hata CHADEMA ikifa leo, kitakuwa ni chama pekee kilichoandika historia ya aina yake katika mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini. Chadema waliichukua hoja ya katiba kama agenda kuu katika ilani yao ya uchaguzi na walipokosa urais, wakamshinikiza Rais atelekeze ilani yao. Katika hili tuwapongeze CHADEMA hata kama tunawachukia.

cc. Ritz, ZeMarcopolo, bungeni, utaifakwanza, MAFILILI Nduka
 
Anastaili kupongezwa pindi itakapo toka imekamilika bila kuchakachuliwa, pia kama ni muungwa kwenye eneo la kinga na madaraka ya Rais yapunguzwe eneo hilo limeguswa lakini bado yapo mambo mengi ya kurekebisha
 
Hii hoja ya katiba mpya haikuwa kwenye mawazo ya chama kingine

Huu uongo wa kupitiliza, hata kilke kiwanda chenu hakiwezi kuzalisha uongo wa wa aina hii. Suala la katiba limekuwa hoja ya CUF kabla CDM haijapata pesa ya kukodi ofisi ya makao makuu pale Kinondoni.
 
For political reasons, Watanzania tumekuwa watu wa kushinikizwa kwamba kuna watu fulani ndio walio shape mambo nchini mwetu. Angalia historia ya uhuru wetu - kwa sehemu kubwa sana anatajwa mtu mmoja tuuu mpaka ina bore!

Hata hivyo ni vema tukubali michango ambayo ilikiuwa prominent kwenye issues mbalimbali including Katiba mpya.

Michango prominent is one thing, nitakuwa mtovu wa fadhila na maskini wa uungwana kama sitashukuru michango ya watu waliozunguka nchi nzima kukusanya maoni na kupigwa vumbi, hata kama wamelipwa.Kazi yenyewe ni ya lawama sana na kuna watu kibao wenye akili zao wasingeikubali (ingawa hatuna sana utamaduni wa kutokubali kazi zilizo visible kwa kukwepa lawama). Kwa hiyo kukubali kazi na kukubali kupigwa vumbi nchi nzima ni jambo la kushukuriwa.

Lakini hizi habari za "baba wa this" "baba wa that" zinatuondolea focus kwamba kinachojenga nchi si watu fulani, ni institutions.
 
Huu uongo wa kupitiliza, hata kilke kiwanda chenu hakiwezi kuzalisha uongo wa wa aina hii. Suala la katiba limekuwa hoja ya CUF kabla CDM haijapata pesa ya kukodi ofisi ya makao makuu pale Kinondoni.
Haha, kwanza nikupongeza kwa kubadilisha avatar. Angalau huonekani kama jini tena. La pili nakubali kwamba ilikuwa kwenye hoja za CUF, but hawakuwahi kuwa serious nalo hadi CHADEMA walipoweka nguvu za ziada kuhakikisha suala la katiba linakatekelezwa.
 
Nilifikiri wapongezwe CHADEMA kwa kususia hotuba yake kutaka katiba mpya. Ni hawa CHADEMA waliokwenda kukaa na Rais Ikulu na kumtamkia kwamba hawatamtambua hadi hapo atakapokubalia kuandika katiba mpya. Inashangaza kwamba leo tunapongeza juhudi za Kikwete pasipo kuangalia juhudi za CHADEMA katika hili. Binafsi naweza kusema hata CHADEMA ikifa leo, kitakuwa ni chama pekee kilichoandika historia ya aina yake katika mageuzi ya kisiasa na kiuchumi nchini. Chadema waliichukua hoja ya katiba kama agenda kuu katika ilani yao ya uchaguzi na walipokosa urais, wakamshinikiza Rais atelekeze ilani yao. Katika hili tuwapongeze CHADEMA hata kama tunawachukia.

cc. Ritz, ZeMarcopolo, bungeni, utaifakwanza, MAFILILI Nduka
acha ushabiki wa kijuha. amka!!!!!!!!!!!!!!!!! umefunikwa ww!
 
Ni ukweli usiobishaniwa kuwa J.Kikwete ni baba wa katiba mpya hapa Tanzania.
Kama kweli katiba mpya itapatikana.
Kama kweli katiba mpya itapatikana kwa haki na amani.
Kama kweli katiba mpya itapatikana bila kuingiliwa na ushabiki na masilahi ya CCM.
Kama kweli katiba mpya haitakuwa na mapungufu yaleyale yaliyomo kwenye katiba ya sasa.
Kama kweli katiba mpya haitaingiza "udini" ndani ya katiba hiyo.
Kama kweli katiba mpya itapunguza madaraka ya kifalme ya raisi.
Kama kweli katiba mpya italiongezea nguvu BUNGE katika kuisimamia serikali.
Kama kweli katiba mpya itaiweka huru tume ya uchaguzi.
Kama kweli katiba mpa itapunguza viongozi wa kuteuliwa na raisi.
Kama kweli katiba mpya itampa madaraka makubwa zaidi ya kiuamuzi waziri mkuu.
Kama kweli katiba mpya itamuondoa raisi katika kuwateua majaji.
Kama kweli katiba mpya itamuondoa raisi katika kumteua katibu mkuu wa BUNGE.
Kama kweli katiba mpya itawafanya wakuu wa mikoa wachaguliwe na moja kwa moja na wananchi.
Kama kweli katiba mpya itapunguza baaraza la mawaziri ni kuweka idadi maalum.
Kama kweli katiba mpya itaondoa au kuweka kikomo cha ubunge kwa viti maalum.
Kama kweli katiba mpya itaweka bayana kikomo cha mtu kuwa mbunge.
Kama kweli katiba mpya itatoa mfumo sahihi wa Muungano wanaoupenda wananchi walio wengi, yaani serikali tatu.
Kama kweli katiba mpya itakuwa kweli ya imetoka kwa wananchi, na kwa masilahi mapana ya wananchi.
BASI KWELI: Jakaya Mrisho Kikwete atastahili kuitwa "BABA WA KATIBA MPYA" hapa Tanzania. Kama itakuwa hivyo, basi napendekeza ijengwe sanamu yake katika viunga vya BUNGE huko Dodoma akiwa ameshika kitabu cha KATIBA MPYA, ili iingie vizuri kwenye historia ya nchi hii vizazi kwa vizazi.

Wakupongeza ni CHADEMA kwani wao ndio walikuja na mchakato huu pamoja na kupingwa na magamba!!
 
Napenda kukuhakikishia ni unafiki mtupu kwa mwanaccm kusema anaipongeza tume kwa kuleta katiba mpya kwani wote walikuwa hawaoni sababu ya hii kitu akiwemo JK mwenyewe mpaka lilipotokea shinikizo. Walidhani watatawala milele ndiyo maana wakawa wamekataa katiba mpya...sasa kinachowawasha kusema JK ni baba wa katiba mpya ni nini?
 
Back
Top Bottom