Rais Dkt. Mwinyi ashiriki chakula cha usiku na GPE Ikulu Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika pamoja na Uongozi wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt.Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika chakula cha usiku alichowaandaliwa Ikulu Zanzibar tarehe 04 Disemba 2023.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE Laura Frigenti pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha Vikao vya GPE vitafanyika Zanzibar na kufunguliwa kesho tarehe 05 hadi 06 Disemba ikiwa ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika.

Vilevile Shirika hilo limeisaidia Zanzibar katika sekta ya elimu fedha za kigeni dola za kimarekani Milioni 11.7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya msingi ikiwemo miradi itakayoanza Januari 2024 kwa kujumuisha mafunzo ya walimu, utendaji, usimamizi wa elimu , masuala ya jinsia na mjumuisho.

Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na Zanzibar.

04 Disemba 2023

Ikulu, Zanzibar.
IMG-20231204-WA0008.jpg
IMG-20231204-WA0009.jpg
IMG-20231204-WA0010.jpg
IMG-20231204-WA0007.jpg
IMG-20231204-WA0014.jpg
IMG-20231204-WA0013.jpg
IMG-20231204-WA0011.jpg
IMG-20231204-WA0012.jpg
IMG-20231204-WA0015.jpg
 
shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na Zanzibar.
Hela yote hii lakini elimu yetu bado haieleweki mwanafunzi ana someshwa nzi ana mabawa mangapi😂
 
Back
Top Bottom