"Kusikia kwa kenge mpaka damu imtoke masikioni.....
Na wewe nae umepost!kama unafikiria kwa kutumia ------ usiwe unatuletea upuuzi wa aina hii.
Kinachonishangaza ni kwa kwa mzee Warioba kuanza kutoa elimu kwa umma JUU ya rasimu yake sasa wakati alipewa pesa nyingi ili kuelimisha umma kwanini Tume yake ili andika rasimu kwa namna ile. Yote ingemsaidia Watu na wabunge kumuelewa. Alitumia muda mwingi kufafanua kwa nini anapendekeza kuuvunja muungano katika rasimu yake wakati akiiwasilisha bungeni ili kuhakikisha wananchi wa Pande mbili za muungano wanachukiana sana. Vitu vingine hata sisi wananchi tulikuwa hatuvijui . Sasa muda wake wa kuandika rasimu umekwisha kwa nini usitulie mzee Wangu upumzike baada ya kazi Ngumu? Kwanini unaona mawazo ya Tume yako pekee yanafaa ? Huoni wabunge wa bunge la katiba nao wanawawakilisha wananchi kwa mfano vijana, wanawake, wavuvi, wafugaji, wakulima, wafanyakazi, waajiri, wafanyabiashara, wanasiasa,NGO, wananchi kupitia wawakilishi majimboni. Je hayo makundi yote yaliyobaki bunge unaona mawazo yao waliyoyatumia kuboresha rasimu ya Tume hayana maslah kwa wananchi? Mi naomba mzee Wangu usitumike vibaya na kikundi kidogo cha wanasiasa na wafadhili wao ambao wana mipango yao ya 2015 wanajitahidi kuipigania kwa mgongo wako bila wewe kujua. Achana nao. Usipoteze nguvuzako waachie wanasiasa walumbane majukwaani na kwenye makongamano. Wananchi kwa mujibu wa sheria watapiga kura kufanya maamuzi. Hiyo ni katiba yao. Kazi yako umemaliza. Sitta kamaliza. Watanzania wataamua lini tumsubiri mwenye mamlaka aliyekuteua wewe na bunge la katiba atasema.
Warioba sasa atulie. Amebwata mno! Katiba tayari atake asitake
"Kusikia kwa kenge mpaka damu imtoke masikioni...! " Muache Sitta na genge lake wamalizie wizi wao huo wa pesa zetu halafu wakione cha mtemakuni...Hawa ni kama viwavi ndani ya shamba la mahindi. Tutalipiga shamba zima dawa tuone kama kuna kiwavi atakaesalimika.....
"Kusikia kwa kenge mpaka damu imtoke masikioni...! " Muache Sitta na genge lake wamalizie wizi wao huo wa pesa zetu halafu wakione cha mtemakuni...Hawa ni kama viwavi ndani ya shamba la mahindi. Tutalipiga shamba zima dawa tuone kama kuna kiwavi atakaesalimika.....
Sitta ameishaanza kuwalalamikia waandishi wa habari eti hawampendi ndio maana wanamuandika vibaya na kwamba siku hizi anatumiwa messages za kumtukana!! Sitta kwa wakati huu is the most hated person zaidi ya hao wanaoitwa mafisadi papa!! Sijui atajisafishaje kutokana na najisi aliojipaka huko kwenye bunge la katiba!