Jaji Warioba: Siioni Katiba Mpya

Jaji Warioba: Siioni Katiba Mpya

nani kakudanganya kuwa wingi wa serikali ndio unaondoa kero za muungano? Pole sana. Alokwambia kuongeza mke wa pili ndio kuondoa kero kwenye ndoa alikudanganya.

Wingi wa serikali ni tamaa za wanasiasa kutaka vyeo yaani ni kama kukamata fursa kama wale wahubiri wa fursa pale mawingu wala haina mantiki kwenye maisha ya watu ya kila siku. Watu wanachotaka ni kuona mambo ya msingi na yanayohusu maisha ya watu ya kila siku yanajadiliwa.

Haki na maslahi ya wafugaji, wakulima, elimu,afya, maadili ya viongozi, tunu za taifa nk ndo vitu watu wanataka vijadiliwe na sio kupoteza muda kujadili maslahi ya wanasiasa au wale wafia dini wanaotaka mahakama za kadhi zikaingizwe kwenye katiba.

Wingi wa serikali sio kipaumbele cha watanzania bali ni kwa maslahi ya wanasiasa yenye lengo la kuisambaratisha nchi. Kama mmechoka amani hamieni congo somalia.

hebu ongea vizuri kama umeshatawaza we mkavilondo. Huyo mke aliyeolewa ni nani mburula weye?
 
Nani kakudanganya kuwa wingi wa serikali ndio unaondoa kero za muungano? Pole sana. Alokwambia kuongeza mke wa pili ndio kuondoa kero kwenye ndoa alikudanganya.

Wingi wa serikali ni tamaa za wanasiasa kutaka vyeo yaani ni kama kukamata fursa kama wale wahubiri wa fursa pale mawingu wala haina mantiki kwenye maisha ya watu ya kila siku. Watu wanachotaka ni kuona mambo ya msingi na yanayohusu maisha ya watu ya kila siku yanajadiliwa.

Haki na maslahi ya wafugaji, wakulima, elimu,afya, maadili ya viongozi, tunu za taifa nk ndo vitu watu wanataka vijadiliwe na sio kupoteza muda kujadili maslahi ya wanasiasa au wale wafia dini wanaotaka mahakama za kadhi zikaingizwe kwenye katiba.

Wingi wa serikali sio kipaumbele cha watanzania bali ni kwa maslahi ya wanasiasa yenye lengo la kuisambaratisha nchi. Kama mmechoka amani hamieni congo somalia.

wapenda ngono utawagundua tu ,mawazo yako yanahusiana na ngono.eti wanawake wawili.uhusiano wa mfano wako na serkali tatu uwapi?
 
we mzee nenda kalale sasa,umepewa kazi umeifanya,umeikabidhi,waache wanasiasa wahuni wa nchi wacheze michezo ya kuigiza,usijitumbukize kwenye huu usanii, jiulize swali moja tu, hivi huyu Mbowe anataka katiba mpya kweli au msanii? katiba ni demokrasia mpana,mbona kashindwa kwenye chama alichowekeza yeye na mkwewe Mtei? rasimu ya katiba yako imewafunga luku M,kiti na Katibu Mkuu wake,unadhani Mbowe analifurahia hili? waache hao wahuni wapambane wenyewe
 
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba, Jaji Joseph Warioba ametabiri kampeni za uchaguzi mkuu ujao kutawaliwa na ajenda ya Katiba mpya ambayo kwa mujibu wake, inaweza kugawa nchi. Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, ameeleza wasiwasi wa rasimu inayopendekezwa kwamba haitapigiwa kura mwaka 2016 badala yake, mchakato wa katiba utaanza upya.

Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Katika maadhimisho hayo yaliyokwenda pamoja na kukumbuka maisha ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Marehemu Dk Senkoro Mvungi na kuzindua kitabu chake, Jaji Warioba alisema haupo uhakika wa Katiba mpya kupatikana.

Wasiwasi juu ya upatikanaji wa Katiba mpya unatokana na kile alichosema kwamba haupo uwezekano wa rasimu inayopendekezwa kupigiwa kura mwaka 2016 kutokana na kutokuwepo maridhiano.

Alisema hata katika kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani, suala la Katiba Mpya litakuwa ni ajenda inayoweza kuigawa nchi ikizingatiwa msingi wa kukosekana maridhiano ni aina ya muundo wa Muungano.

"Hakuna maridhiano hasa kuhusu Muungano, rasimu hiyo itaanza kupingwa tangu siku ya kutolewa kwake na wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka kesho Katiba mpya itakuwa ni ajenda inayoweza kuigawa nchi," alisisitiza na kusema upo uwezekano mkubwa kwamba mwaka 2016 badala ya kupiga kura, mchakato wa kutengeneza katiba ukaanza upya.

Warioba alisema ataendelea kutetea maoni ya wananchi. Alisema wanaotumia vipaza sauti kumuona yeye ni shida, watakutana mtaani ambako kila mmoja akitetea hoja yake, ndipo itakapojulikana shida halisi iliko. Alisema tangu mwanzo matumaini yalikuwa ni nchi kupata Katiba mpya kwa maridhiano.

Alieleza kusikitishwa na mchakato kutekwa na vyama vya siasa kiasi cha maridhiano kutofanywa kipaumbele.

"Kipaumbele ni kupata kura…tangu mchakato huu ulipotekwa na vyama vya siasa, jitihada zilikuwa ni kupata katiba ya makundi, siyo katiba ya maridhiano ya wananchi," alisema Warioba .

Akosoa rasimu inayopendekezwa Jaji Warioba alikosoa mambo kadhaa yaliyopendekezwa katika rasimu inayopendekezwa, mojawapo ikiwa ni suala la Rais wa Zanzibar kuwa kwenye Baraza la Mawaziri.

Alisema litakuwa jambo tata kwa kuwa yeye (Rais wa Zanzibar) haingiliwi kwa mambo ya Zanzibar.

Alisema lazima patahojiwa haki aliyo nayo kuamua mambo ya Tanzania Bara kwenye Baraza la Mawaziri wakati viongozi wake hawashiriki kuamua mambo ya Zanzibar.

Alisema yeye ni kiongozi wa taifa na atakuwa kwenye Baraza la Mawaziri, lakini hawezi kuwajibishwa wakati Rais, Makamu wa Kwanza na Waziri Mkuu wanaweza kuwajibishwa. Kuhusu madaraka ya wananchi alisema, kwa kuwa katiba inatungwa nao, maoni yao ilikuwa kwamba wawe na madaraka ya kumwondoa mbunge wao kama hawataridhika na uwakilishi wake.

Alisema wananchi pia hawakutaka wabunge kuwa mawaziri ili waweze kuwakilishwa vizuri na ukomo wa ubunge uwe wa vipindi vitatu. Hata hivyo, alikiri kwamba si jambo la kawaida kwa Mbunge kuondolewa madarakani katikati ya kipindi au kuwekewa ukomo, lakini alisisitiza kwamba kwa sababu ya rushwa katika uchaguzi, wananchi wanaona ni vyema watumie madaraka yao kuwawajibisha wawakilishi hao.

"Vyama vya siasa vina madaraka ya kuwaondoa wabunge wao katikati ya kipindi, wananchi nao wanataka watumie madaraka yao," alisema Warioba akisisitiza Bunge Maalumu liwaeleze wananchi sababu ya maoni yao kuondolewa. Kuhusu mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili alisema pendekezo la kumwondoa rais na mawaziri kutoka kwenye Bunge linakataliwa kwa sababu imezoeleka mfumo wa kibunge kama ilivyo kwa nchi nyingi za Jumuiya ya Madola.

"Siyo kweli kwamba mfumo wetu ni wa kibunge. Kwenye mfumo wa kibunge mkuu wa nchi hana madaraka ya utendaji, madaraka hayo yako mikononi mwa Waziri Mkuu ambaye ni mbunge," alisema na kutoa mfano wa Uingereza, India, Canada, Australia na hata New Zealand zinazofuata mfumo huo.

Alisema Tanzania ina mfumo wa urais ambao Rais ni Mkuu wa nchi, Mtendaji mkuu na Amiri Jeshi Mkuu.

Alisema Rais na Mawaziri wake kuwa sehemu ya Bunge ni kuchanganya mamlaka na kufanya serikali kuingilia mamlaka ya chombo hicho na pia chenyewe kuingilia mamlaka ya serikali.

Kuhusu tunu za taifa, Warioba alisema Bunge limeondoa uadilifu, uzalendo umoja, uwazi na uwajibikaji kutoka kwenye orodha ya tunu za taifa na kuziweka kwenye misingi ya utawala bora.

Alisema tunu za Taifa ndiyo msingi wa utamaduni na maadili ya taifa, mwelekeo wa taifa utategemea jinsi wananchi wanavyoenzi misingi mikuu na tunu.

Chanzo:Habari leo
 
Hawa jamaa wanaomtetea Warioba wanafiki sana.
Laiti ndo angekua kwenye chama chao cha chadema na anapishana na misimamo ya viongozi wake hawa hawa mashabiki mandazi wangembatiza jina la usaliti. Lakini kwakuwa yuko ccm anacheza ngoma ya ukawa wanaona poa tu na kumpa maujiko ya kijinga. Kwao hata nchi ikisambaratika hawana cha kupoteza kwasababu hata historia haiwatambui.

Kama mnaona Warioba anachokifanya ni sahihi basi mngetoa mfano kwa kuwapigania akina zitto wasifukuzwe ndani ya chama baada ya kuwa wanaipigania Katiba ya chama chenu iliyochakachuliwa ili kuweka kipengele cha ufalme(uongozi pasipo ukomo).

Wafukuzeni akina Mbowe na Slaa waliopindua katiba ya wananchi(wanachama) kisha kuweka mambo yao kinyemela kwan kwa kufanya hivyo hawana tofauti na CCM waliochakachua katiba ya wananchi kwa kuweka yao.

Hii yote ni shibe ya amani ndo inawalevya na kuona haina umuhim tena. Siku mtakapoanza kumwagana damu mtaikumbuka sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

dada arola ww unatetea genge la mafisadi kwa kisingizio cha kutambuliwa na historia,nina kati yako na warioba ambaye anatambuliwa na historia,serikali tatu zimekuwapo tangu muungano huu ulipoanza warioba kwa kutumia ujuzi ,uzoefu na elimu yake pamoja na jopo lake waliona jibu la kwanza la matatizo ya muungano ni kuwa na serikali 3. Rais wa muungano atakuwa amiri jeshi,siyo haya mazingaombweyaliyopo sasa JK2 akienda zanzibar ni mgeni anakuwa chini ya sheni,amiri jeshi mmoja ,uraia mmoja,fedha mmoja nchi itasambaratika vipi nyie B7 Acheni kuwatetea hawa wahalifu,wauza dawa,wakata magogo,mafisadi,sasa wanahangaika kuharibu rasmu,aibu yao na nyie mnaowatetea.
 
Back
Top Bottom