MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,268
Wakati akikabidhi Katiba Inayopendekezwa kwa Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Mhe. Andrew Chenge alieleza umakini mkubwa uliofanywa na Bunge hilo wakati wa kuandaa Katiba Inayopendekezwa.
Alisema, asilimia 81.8 ya mapendekezo ya Rasimu iliyowasilishwa bungeni na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba yamo katika Katiba Inayopendekezwa. Alisema Ibara 46 ambazo ni sawa na asilimia 10.7 zimefutwa na Ibara 54 sawa na asilimia 18.2 ni mpya.
Kwa mujibu wa Mhe. Chenge, ili kukidhi muundo mpya wa Serikali mbili ambao ulitofautiana na wa Tume iliyopendekeza wa Serikali Tatu, baadhi ya ibara ziliongezwa na nyingine kufutwa, kuboreshwa au kubadilishwa kukidhi muundo mpya wa Serikali Mbili.
Ibara zilizoathirika zaidi ni Ibara ya Kwanza na Ibara ya Sita ya Rasimu ya Tume ambazo zilihusu Muundo wa Serikali Tatu. Katiba Inayopendekezwa ambayo itapelekwa kwa wananchi kupigiwa Kura ya Maoni, itakuwa na Sura 19 zenye Ibara 296 tofauti na ile ya Tume ya Warioba iliyokuwa na Sura 17 na Ibara 271.
Katika kujibu hoja za Bunge Maalum, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa katika likizo ya wiki moja nyumbani kwake Bunda, Mkoa wa Mara, Jaji Warioba alialikwa na vijana wa mji huo kupitia Jukwaa lao la Uwazi na Fikra Yakinifu, wakiomba azungumze nao kuhusu masuala mbalimbali hasa mchakato wa Katiba Mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Harrieth, Jaji Warioba alinukuliwa akisema, "Kazi yetu kama Tume ya kuandaa Katiba ya Watanzania tuliimaliza. Bunge nalo limemaliza kazi yake japo ina upungufu. Sasa kazi imebaki kwenu wenye Katiba; kuisoma Katiba Inayopendekezwa kwa makini kabla ya kuipigia kura," alisema Warioba.
Jaji Warioba alieleza kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge la Katiba, Samuel Sitta siku ya kukabidhi Katiba Inayopendekezwa kwa Rais, kwamba Bunge hilo limeweka ndani ya katiba hiyo asilimia 81 ya maoni ya Tume, akisema huo ni uongo mkubwa.
"Ukweli ni kwamba wamechukua asilimia 20 tu na kutupa nje asilimia iliyobaki na kubandika yaliyomo katika Katiba ya sasa ambayo hayawezi kuleta mabadiliko yoyote," alisema Jaji Warioba.
Habari yenyewe inapatikana HAPA
Hivyo, Jaji Warioba aliwataka Watanzania kwa umoja wao bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini, rangi, kabila kuhakikisha kuwa wanapata Katiba Inayopendekezwa na kutumia muda mwingi kuisoma kabla ya kuipigia kura.
Fast forward mpaka tarehe 2 November 2014, kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, ambapo kulifanyika Kongamano liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).
Kabla ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza, mshehereshaji wa mdahalo huo Hamza Kassongo alimuomba atoe jibu kama ni kweli Katiba Inayopendekezwa imebeba asilimia 80 ya maudhui ya rasimu ya Pili ya Katiba.
Jaji Warioba katika jibu lake, alisema, ukihesabu Ibara baada ya Ibara utapata asilimia 81 ya ibara za Rasimu ya Tume zimewekwa kwenye Katiba Inayopendekezwa, hata hivyo, maudhui yake yakitazamwa kwa makini mambo mengi ya msingi yametupwa.
Kwa watu wenye fikra pevu lazima waanze kujiuliza, ukweli ni upi wa yale anayoyasema Jaji Warioba kwa sababu hoja zake zinakinzana. Kwa sasa anajikita kwenye maudhui badala ya idadi ya asilimia kama alivyosema wakati akiwa Bunda.
Kama Jaji Warioba anaweza akabadilisha majibu ndani ya muda wa mwezi mmoja, kitu gani zaidi ambacho mwananchi anaweza kuamini kuwa anachokisema leo hawezi kukikana kesho?.
Baadhi ya wananchi walimpatia the benefit of the doubt kuhusiana na kauli yake ya 26 Oct 2011 alipofanya Mahojiano na Gazeti la Raia Mwema pale aliposema Tusidanganyane, kutaka Serikali tatu ni kuvunja Muungano.
Mahojiano hayo yanapatikana HAPA
Jaji Warioba alinukuliwa akisema hivi,
Majibu aliyoyatoa Jaji Warioba hayatofautiani na majibu ambayo alishawahi kutoa kuhusu sababu zilizoifanya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuamua muundo wa Serikali tatu. Jaji Warioba alianza kwa kusisitiza na kusema, maamuzi ya kupendekeza Muundo wa Serikali tatu yamefikiwa baada ya ''wananchi wengi'' kupendekeza Muundo wa Serikali Tatu. Watanzania wengi katika maana ya Watanzania 17,280 waliopendekeza Muundo wa serikali tatu ambapo ni asilimia 37.2 ya Watanzania 47,280 walioongelea suala la Muungano.
Baada ya kugundua hoja zake hazina mashiko kwa watu wenye fikra pevu kwa sababu zimeangukia katika convenience sampling badala ya random sampling,ndiyo maana akageuka na kusema, umuhimu wa hoja ndiyo uliwafanya wachague Muundo wa Serikali tatu na siyo idadi wa waliochagua Muundo huo. Hii ilikuja baada ya watu wenye fikra pevu kuichana chana hoja yake kulingana na hali halisi ya takwimu na mazingira.
Kauli na hoja za Jaji Warioba zinanikumbusha usemi wa mwanasiasa, Mwingereza aitwaye, Joseph Chamberlain ambaye alinukuliwa akisema, ‘In politics, there is no use in looking beyond the next fortnight'. Hii ina maana kuwa, Kile anachokisema Jaji Warioba leo usitegemee ndicho atakachokisema wiki ijayo!
Hawa ndiyo wanasiasa na wazee wetu!
Mpaka kufika kwenye Kura ya Maoni, tutaona na kusikia mengi!

Shughuli za wananchi wa kawaida haziangalii orodha ya mambo ya Muungano, bali haki yao kama raia. Wanajiona ni raia katika shughuli zao za kibiashara au nyingine. Mwananchi wa kawaida anaona anayo haki ya kufanya biashara mahali popote. Wananchi wamezoea hivyo. Msiwafikishe mahali wakajiona kuwa kwenda Zanzibar au kuja Bara inabidi wafuate taratibu za kwenda Kenya au Uganda.
Sasa hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar. Hivi ukileta serikali tatu, ugomvi huu hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika yenyewe haitadai madaraka? Mwisho wataomba madaraka hadi Serikali ya Muungano isiwe na chochote.
Hivi Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na wimbo wake wa Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai ifanye biashara ya nje, unafikiri tutakuwa tumefika wapi?
Lakini tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande zote mbili. Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu wanajua nia yao ni kuvunja Muungano na huu ndio ukweli. Ukianzisha serikali tatu, maana yake unavunja Muungano