Jaji Warioba nakupenda kwa dhati

Jaji Warioba nakupenda kwa dhati

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
Jaji Warioba nakupenda kwa dhati sana wewe ni miongoni mwa watu ninaojivunia kuwa nao katika Taifa hili, umeonesha siyo mwoga kwa CCM na makada wake. Unasimamia haki na kile unacho amini hata kama watu wengi hasa waliyo kunywa maji ya CCM wanakubeza mimi kutoka ndani ya kilindi cha moyo wangu nakupenda siyo mimi tu natumaini maelfu yako nyuma yangu wanakupenda wewe ni adhina na mfano kwangu na Taifa hili LIVE LONG WARIOBA.
 
Ninasikia harufu ya ulibelari kwa mbaliiii
 
Kitu kikishakuwa najisi huendelea kuwa najisi. Rasimu ya warioba ilikuwa maridhawa na yenye manukato yaliyovutia taifa kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli hasa ya kumfanya mwananchi aweze kufaidi rasilimali za taifa. Ghafla wachafuzi na walafi wakaona haiwezekani fursa hii iwafikie hadi wananchi wa kawaida....wakaamua kuinajisi katiba na kupoteza harufu nzuri ya manukato yaliyovumishwa na upepo mzuuri wa wataalamu hawa wa akina jaji warioba. Kilichopo sasa walafi hawa wanalazimisha harufu mbaya iwe nzuri kitu ambacho hakiwezekani. Kutaka wajumbe wapige kura ughaibuni ni kulazimisha harufu mbaya iwe nzuri....kusema kuwa watapata 2/3 zanzibar ni kulazimisha harufu mbaya iwe nzuri. Kana kwamba wanahisi wanaanza kupata harufu nzuri linajitokeza suala lingine ambalo harufu yake ni kuu hasa kwa kuwa kuna watu wanaihisi ni nzuri na wengine wanahisi ni mbaya. Suala hili linaleta hofu kuu miongoni mwa walafi...wameanza kuweweseka watajinasua vipi mtegoni mwa kadhi (harufu kuu). Wajuvyi wa mambo walisema katiba ni maridhiano na ni dhahiri shairi walidharau maridhino awali wanayatunuku sasa hivi muda ukiwa umeyoyoma. Naomba kumalizia kwa kumnukuu Warioba kuwa "tutakutana mtaani".
 
Ninasikia harufu ya ulibelari kwa mbaliiii

Ndilo mnalowaza tuu hukoLumumba. Jana nimemsikia Komba analalamika kuwa Warioba "anawaingilia" sana, ajabu maccm wakaanza kupiga kelele "hatuingilii bwana! Anatufatafata tuu!" Wakiwa wamekwenda kwenye maana nyingine. Ndio mawazo yenu.
 
Duniani kuna watu na viatu,vyote vimo duniani kwa wakati mmoja,haiwezakani watu wakawepo na viatu visiwepo.Mtunzi wa wimbo huu alijua si kila binadamu anayevaa sketi\gauni,kaptula,suruali ni mtu vingine ni viatu.Mfumo wa serikali mbili kamwe hautamalizaimani ya wazanzibar kuamini kwamba Serikali ya Muungano imevaa kotila Muungano kama BOT na akaunti ya JMT itachanganywa na Tanzania Bara hata wabunge wote wa Zanzibar wawe makamu wa Rais wa JMK makamu 1,2......80.Tanzania Bara nao hata siku moja wanaona Serikali ya Mapinduzi imepora madaraka ya bara CHAO SI CHETU BALI CHETU NI CHETU.Dukuduku zote hizi hazitaisha kwa katiba ya Sitta na CCM yake hata zikipingwa kura toka sayari ya Mars.Muarobaini wa matatizo yote hayo ni serikali ya shirikisho.Acheni uongo hata Scotland na serikali ya Uingereza Labour n conservative wameaahidi kufanya mangeuzi makubwa likiwepo la kuanzisha serikali ya Shirikisho.Jaji Warioba aksnte kwa kazi nzuri na tume yako.Ufumbuzi wa Muungano wetu ni serikali tatu kama ulivyopetengeza lakini wenzako si watu unahangaishwa na viatu.KUNA WATU NA VIATU DUNIANI
 
Tumuombee Mungu, maana jamaa wa kung'oa kucha na meno wanaweza wakawa wanajipanga.
 
Long live MZEE WARIOBA!waache wakutukane,kashifu n.k ila Watanzania twakupenda!
 
Jaji Warioba nakupenda kwa dhati sana wewe ni miongoni mwa watu ninaojivunia kuwa nao katika Taifa hili, umeonesha siyo mwoga kwa CCM na makada wake. Unasimamia haki na kile unacho amini hata kama watu wengi hasa waliyo kunywa maji ya CCM wanakubeza mimi kutoka ndani ya kilindi cha moyo wangu nakupenda siyo mimi tu natumaini maelfu yako nyuma yangu wanakupenda wewe ni adhina na mfano kwangu na Taifa hili LIVE LONG WARIOBA.
Mwambie akuchumbie ili ufadi zaidi upendo wake.
 
Ndilo mnalowaza tuu hukoLumumba. Jana nimemsikia Komba analalamika kuwa Warioba "anawaingilia" sana, ajabu maccm wakaanza kupiga kelele "hatuingilii bwana! Anatufatafata tuu!" Wakiwa wamekwenda kwenye maana nyingine. Ndio mawazo yenu.

Hahahah kwahiyo wametafsiri kuingiliwa kinyume sio



Hahahaha
 
Nimegundua vyombo vingi vya habari vinampiga vita mzee wetu. Akizungumza jambo huvisikii kumnukuu ila utavisikia vikiwanukuu hata wapiga debe wa chama chetu wanavomjibu kwa kejeli!
 
"Tutakutana mtaani......!!"

Waswahili pia tuna methali na misemo mingi.......baadhi husema "wengi wape,usipowapa watajichukulia...." na wajuzi wa mambo husema "huwezi shindana na nguvu ya wakati...." hawa manyangau tutakutana nao mtaani tu......
 
Mzee Warioba kwa kipindi kirefu sasa (awamu ya 4) hakuna mtu mzalendo wa kweli mwenye uchungu na watanzania aliewahi kujitokeza wewe ndio wa kwanza! Wewe ndio tegemezi la maelfu ya watanzania. Nili underestimate hili jambo ihadi nilipotambua kwamba kumbe wananchi wengi sana wanao msimamo thabiti wa kukuunga mkono. Kila sehemu niyopita makundi kwa makundi wote msimamo ni mmoja tuu! Hili nimenipa matumaini kwamba tutajikomboa tuu.
 
Katika aina ile ya viongoz aina ya kina nyerere,mandela na wengineo huyu ndio moja kati ya wazee wachache wenye uchungu na bara hili
Sijawahi kusikia wazee wetu wakubwa wakijitokeza huko mafichon walipo na kutoa nasaha zao kukemea uozo wa aina yoyote unaoendelea hapa home.
Ila wakati wa mikutano ya vyama vyao uonekana tena zaidi kwenye hafla mbali mbali
TANZANIA IMEKUWA KAMA MTOTO ASIYE NA MZAZI wakati wazazi mpo ila mmemezwa na watoto.jitokezeni mlipo onyeshen misimamo yenu.msikubali kumgeuka mwalimu na mlipotaka kulipeleka jahazi letu,hamuoni uelekeo liendako siko,Mungu amewahifadhi nyie wazee ili muwasaidie hawa vijana wanapokengeuka kama mnavyojitokezaga kule dodoma kwenye vikao vya chama jitokezeni basi kuongelea mambo ya msing ya taifa letu.WAZEE NI HAZINA YA TAIFA
Big up super Warioba songa mbele kwa kulijenga taifa
 
Back
Top Bottom