Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Jaji Warioba amjibu Bulembo (CCM)

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,613
Reaction score
6,735
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wanasiasa wameacha kujadili rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume yake badala yake wamejikita katika kuijadili Tume yake na Wajumbe.

Kauli ya Jaji Warioba imekuja kufuatia tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdallah Bulembo mkoani Tanga zilizonukuliwa na ITV na baadhi ya magazeti leo.

Katika taarifa hizo, Bulembo anaelezwa kusema kuwa Tume ya Warioba imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya badala ya kukusanya maoni ya wananchi hao na kuongeza ikiwa Tume au Jaji Warioba anataka kufanya kazi hiyo, basi ajiuzulu kwanza katika Tume.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Warioba, ambaye ameshawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri Mkuu, amesema kauli hizo ni upotoshaji na kuwa Tume yake ina jukumu la msingi la kutoa elimu kwa umma.

“Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa elimu kwa umma, na ni kazi ya wakati wote,” anaelezwa kusema Jaji Warioba wakati akijibu swali la mwandishi mmoja kutoka Star TV aliyeongozana na baadhi ya waandishi wengine kutoka ITV, Channel Ten na Clouds FM.

Kwa mujibu wa Warioba, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao walikuwa ni wajumbe wa Mabaraza hayo walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na Wajumbe wa Tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

“Sasa anaona (Bw. Bulembo) kuwa kutoa elimu ni dhambi,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Bulembo kutoa kauli kama hizo.

“Nilimsikia Mbeya, Moshi na sasa Tanga akitoa matamshi hayo… kwa kawaida huwa sizungumzii mambo haya, huwa tunayaacha yapite,” alisema na kufafanua kuwa kauli kama hizo zimekuwa zikiwafanya wajumbe wa Tume kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Nilisema katika mkutano wangu na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita kuwa Tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za wanasiasa, zikiwemo zake (Bulembo),” alisema na kuongeza kuwa, pamoja na kauli hizo, Tume yake inafarijika na kauli za kutia moyo wanazozipata kutoka kwa wananchi wa kawaida.

“Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia rasimu,” anaelezwa kusema.

Jaji Warioba alisema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au Tume.

“Nadhani wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana, badala ya kuzungumzia Tume na watu,” amesema Jaji Warioba.

Kuhusu kujiuzulu, Jaji Warioba anaelezwa kusema kuwa haamini kuwa kauli zinazotolewa na Bulembo ni kauli za CCM kwa kuwa CCM haijawahi kuitaka Tume ijiuzulu.

“Sina hakika kama anazungumza kwa niaba ya CCM kwani CCM haijasema tujiuzulu,” anadaiwa kusema.

Imeandikwa na mwandishi wa JF
 
Tz sio ya warioba, wala yy hana mamlaka ya kuwasemea watz.
 
Kuna jamaa mmoja humu ameandika kwamba anatangaza kujiuzuru leo, kumbe UONGO! MODS mfuatilieni huyo jamaa. JF sio mtambo wa kuzalisha uongo.

Lakini mbona Judge Warioba hajasema kwamba Abdullah Bulembo (STD VII leaver) alifananisha uso wake na NGIRI!! Hawa watu wa Mara (Warioba na Bulembo) wanapenda sana VIMOLO vya Ngiri
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz
 
tume inavunjwa na Rais aliyoiteua, mwambieni Rais usiropoke hapa utafikiri hujui kanuni
 
watz wengi wanataka serikali 3 si 2 umeskia ww kubwa jinga yaambie na maccm menzio sawa.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

William,

Hii Tanzania si ya Malecela wala mgogo yoyote. Wewe ngoja chama cha baba yako kitakapoondolewa madarakani ndipo utakapojua ni kwa jinsi gani watu tunavyokutamani tukugawane huku nje! Hii Tanzania si ya mwaka 47! Watanzania wa leo tumeshawajua adui zetu ni akina nani.

Nyie mtabakia na sapoti ya hao hao wahamiaji haramu ambao wanawasapoti kwa kuwa wanajua ndio nguzo yao ya kuwafanya waendelee kuwepo nchini pasipo uhalali. Na nyie muendelee kuwaua ndugu zetu na biashara yenu ya Unga.
 
- Hatuwezi kuongelea Rasimu wakati tayari imeshakuwa muswaada, alichosema Bulembo ni sawa sawa kwamba Warioba hakuteuliwa kuwaamulia wananchi maoni ya katiba na wala hakuambiwa kuwaelemisha maana katiba, alichotakiwa ni kukusanya tu maoni yao, Warioba kama mwananchi wa Tanzania anayo haki ya kutoa maoni yake kuhusu katiba lakini hawezi kuyatoa akiwa ndani ya tume ni mpaka ajiuzulu kwanza, ndicho alichoambiwa na Bulembo na hakuna cha ajabu hapo wala utata.

- Narudia tena Warioba, ajiuzulu sasa kazi yake ya kamati ili awe Raia huru kama wengine wote ndio atoe maoni yake kuhusu KAtiba, hatuwezi kujadili Rasimu sasa maana tayari Rasimu ipo Bungeni inasubiri saini ya Rais twende kwa mbele.

Le Mutuz

weee na we si ukalime zabibu huko MVUMI
 
BVp-r8JCcAAsbk-.jpg
 
tume inavunjwa na Rais aliyoiteua, mwambieni Rais usiropoke hapa utafikiri hujui kanuni

- tunaishi kwa Sheria sio kanuni, Sheria ipo wazi Warioba hana mamalaka ya kuwaamulia wananchi Katiba, ila anayo mamalaka ya kukusanya maoni yao na kuyaandika chini, Warioba hana mamlaka yoyote kikattiba ya kuwaambia eti Viongozi wa Saisa wakae chini kujadili tena Rasimu, Rasimu imeshaenda Bungeni imepitishwa na Wabunge wa Chadema na CCM, sasa inasubiri saini ya Rais iwe Muswaada na kujadiliwa na Wabunge,

- Labda nikukumbushe historia kidogo, kule USA ni Republicans ndio walioamua kupunguza mafao ya Marais wao kwa sababu ya wingi wao bungeni, na ni wao ndio walioamua kupunguza malipo ya welfare ya wananchi wao bila kujali uchache wa Democrats bungeni kwa sababu Sheria inasema ni majority ndio wenye uamuzi wa mwisho wa marekebisho ya sheria, CCM ndio wenye mamlaka ya mwisho kisheria ya jamhuri kuamua katiba mpya iweje sio Warioba na Chadema.

Le Mutuz
 
ninaheshimu na kuikubali kazi nzuri Jaji Warioba anayofanya kwenye mchakato wakatiba....... nilisema kwa yule alietoa tetesi za Warioba kujiuzulu kwamba mimi ni, na, nitaendelea kuwa Tomaso hadi siku atapofanya kwel. Anapojitetea ccm haijamtaka ajiuzulu kwani huyo Bulembo ni nan? Au alitaka nan kutoka ccm atamke ndio aelewe? Kukwepa hizi dharau na kadhia anazopata mi naona heri achukue uamuz mgumu mapema kabla hawajamuaibisha.
 
Back
Top Bottom