Jaji Warioba ambana Jussa kuhusu Muungano wa mkataba

Pole sana mkuu. Mbwembwe nyiiingi lakini masuala yenyewe ni yale yale ya siku zote. Tena kwa kuonesha jinsi usivyo makini sijui niziite hoja au kitu gani (zako) nyingine zinajirudia rudia. Mambo mengine uliyoyaandika hayana mantiki kabisa.

Ina maana hapo kabla Zanzibar ilikuwa haina demokrasia, chaka la magaidi, chaka la madawa ya kulevya, haiheshimu haki za binadamu, hairuhusu uhuru wa kuabudu, nk., nk., nk.????!!!!
Nasema tena pole sana mkuu, kajipange upya.
 
Russia ilipata Uhuru twake toka Soviet union sasa watu wake wananeema kuliko mwanzo, why not for Tanganyika, Georgia ni Zanzibar Georgia ilikuwa inainyonya Russia uchumi wake lkn wote sasa ni nchi huru LIFE GOES ON! why Tanganyika au Zanzibar zisiwe huru? wacha ZNZ iende Tanganyika ni Russia
 
Mwezi uliopita niliwahi kutembelea kisiwa cha Unguja. Kitu kilichonishangaza kuanzia kwenye nyumba za watu/wageni hadi daladala kuna STICKERS za aina mbili tu. MOJA inasema MUUNGANO NI KAMA KOTI (Abeid Aman Karume). Sticker ya PILI inasema TUACHENI TUPUMUE. Hizi Stickers mbili zimetapakaa kila kona ya Unguja.

Lakini pia kila nilipokuwa ninatembelea VIJIWE VYA KAHAWA (my Observation) karibu kila MTU alikuwa anasema ZNZ wanataka MUUNGANO WA MKATABA. Tena wakijua mimi ni Mu-Bara ndiyo wanahanikiza kabisa SAUTI as if mimi ni Judges Warioba au Augustine Ramadhani. Kuna wakati nilijaribu kuhoji huo Muungano wa mkataba uko/utakuwaje? Lakini hakuna hata mtu aliyeweza kunielezea vizuri kitu kimoja nilichogundua ni kwamba ZNZ wanataka MORE AUTONOMY from Tangayika.

Huo MUUNGANO WA MKATABA wasije kuwa wanaaminsha kitu kile kile ila katika chupa nyingine, kwasababu hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitokana na MKATABA "ARTICLE OF UNION" Ninataka Mzanzibari anayefahamu vizuri huo muungano wa mkataba unaopigiwa sana upatu ZNZ uko/utakuwa je? Muundo wake?, uongozi wake? serikali zake, gharama za kuendesha MKATABA huo zitachangiwa vipi etc, Status ya Tangayika na ZNZ kwenyer huo mkataba, Amri Jeshi Mkuu? Mahusiano ya nje? Uraia? etc
 
Kumbe wewe umewaelewa jamaa zangu ni watu wa jazba wenye pupa na wasiokuwa na tabia ya kuona mbele wala kuweka kitu katika mizani. Kuhusu sticker na ya vijiweni ndio demokrasia hiyo ya mkataba tulionao hìvi sasa siyo huo tnaopigiwa chapuo.
 
Bobuk,

..ZNZ hawataki Tanganyika iwe na kauli kuhusu maamuzi yao.

..kwa mfano wanataka wawe na uwezo wa kuagiza bidhaa toka nje, kuziteremsha ZNZ, na baadaye kuzimwaga huku Tanganyika bila kulipa ushuru. huo ni mfano mmoja tu.

..suala lingine wanataka tuwasaidie kubeba baadhi ya majukumu ambayo hawawezi kuyabeba wenyewe. hapa kuna suala la URAIA na UHAMIAJI. Elewa kwamba 1/3 ya waZNZ wanaishi huku Tanganyika. ZNZ inapendelea raia hao waendelee kubaki huku Tanganyika.

..sioni faida yoyote ile tutakayoipata wa-Tanganyika ktk muungano wa mkataba.
 
Last edited by a moderator:
sio rahisi kama wanavyofikiria na dhambi hiyo hiyo itawaandama na wao watatengana na visiwa hivyo vitakuwa vichaka vya maharamia
 
[h=1]
jussa-564x272.jpg
[/h] Mh Ismail Jussa Muwakilishi wa Mjimkongwe Zanzibar(Stone Town)

Written by Stonetown (Kiongozi) // 05/12/2012 // Habari // 2 Comments

Na Ismail Jussa
Muungano wa Mkataba ni MASHIRIKIANO kati ya nchi mbili au zaidi ambazo kila moja huwa inabaki na mamlaka yake kamili ya KIDOLA kitaifa na kimataifa lakini vado zikawa zina mashirikiano katika maeneo maalum zitakazoamua kushirikiana, mahusiano ambayo huwa yanaongozwa na Mkataba.
Muungano wa Mkataba ni tofauti kabisa na Muungano wa Kikatiba ambao huwa unamaanisha kuwepo kwa Serikali ya Muungano inayosimamia mambo ya Muungano.
Katika Muungano wa Mkataba, kila nchi hubaki na Serikali yake kamili yenye kusimamia mambo yote. Yale maeneo ya USHIRIKIANO husimamiwa kupitia ama KAMISHENI YA PAMOJA au KAMATI YA PAMOJA kwa kadiri makubaliano yatakavyokuwa yamewekwa kwenye Mkataba.
Faida za Muungano wa Mkataba:
1. Hakuna khofu ya nchi moja kuimeza au kuitawalia nchi nyengine.
2. Kila nchi inabaki na uhuru na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kuamua mambo yake.
3. Kila nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katika jambo lolote ililoamua mwanzo kushirikiana pale inapoona hakuna maslahi au faida kuendelea nalo.
4. Huvutia nchi nyingi kuingia katika Muungano wa aina hiyo kwa sababu hakuna khofu ya kupoteza mamlaka au kupunguziwa madaraka au mambo yake kuamuliwa na nchi nyengine.
5. Mahusiano huwa ni ya kirafiki na ya ujirani mwema yanayopelekea kuaminiana na kuondoa kutiliana shaka kusikokwisha.
Zanzibar iwe na mamlaka yepi kitaifa na kimataifa katika Muungano wa Mkataba?
1. Iwe na Serikali kamili yenye Wizara zote ikiwemo Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani na Ulinzi.
2. Iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa na pia uanachama wa Jumuiya zote za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Nchi za Bahari ya Hindi.
3. Iwe na Benki Kuu yake na Sarafu yake.
4. Iwe na mamlaka yote ya kuamua será za fedha na uchumi, kodi na sarafu.
5. Iwe na Uraia wake.
6. Iwe na Paspoti yake na kusimamia Uhamiaji katika nchi yake.
7. Idhibiti Anga yake na Usafiri wa Anga yenyewe.
8. Isimamie Elimu ya Juu yenyewe na kuamua Mitihani gani itumie katika masomo.
9. Isimamie na inufaike na rasilimali zake zote za ardhini na baharini ikiwemo mafuta na gesi asilia.
10. Idhibiti yenyewe eneo la mipaka ya Bahari Kuu (EEZ) katika eneo lote inalopakana nalo.
11. Idhibiti mamlaka mengine yote yanayokuwa yanamilikiwa n anchi kamili.
Ni ipi Mifano ya Muungano wa Mkataba?
- Muungano wa Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.
- Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye wanachama 5 mpaka sasa.
- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS).
PAMOJA TUNAWEZA
 
Ismail Juha sorry Jussa tangu lini akaujua muungano wakati anachojua ni kubomoa? Nashauri akaulize maswali yake huko kwao u*********ni. Nchi yetu imekuwa kama haina mwenyewe. Hawa walioleta funza nao wanapewa nafasi ya kuongelea mambo yetu kwa jeuri na sababu zipi? Juha sorry Jussa ajifunze kwanza ndipo afundishe.
 
Russia ilipata Uhuru twake toka Soviet union sasa watu wake wananeema kuliko mwanzo, why not for Tanganyika, Georgia ni Zanzibar Georgia ilikuwa inainyonya Russia uchumi wake lkn wote sasa ni nchi huru LIFE GOES ON! why Tanganyika au Zanzibar zisiwe huru? wacha ZNZ iende Tanganyika ni Russia

Russia imekuwa Russia kw amiji miwili tuu, Moscow na St petersburg.HUko kwingine kama hakukuwa na nchi, sasa wapi tena Georgia ikainyonya Russia?Acheni uzembe nchi inapowatangulia msianza singizia kuw amlinyonywa ndio maana mkabaki nyuma.Kwanini usialame wakati ukinyonywa?
 
Muungano ni mchongoma,wekeni fence ya umeme asipenye mtu
 
Zanzibar ilikuwa haikatiwi umeme hata siku moja, yaani mgao kwa Zanzibar ilikuwa kama history tu, mpaka mwa 2009 pole waziri wa nishati wa Znz mansuri yusufu himidi alipotukana Tanzania bara kuwa wanaiibia znz,ndio chanzo cha znz kupata mgao bila upendeleo kama mikoa ya bara
 
Zanzibar hawapo huru kifkra. Ndio maana viongozi kutoka zanzibar ni wa hovyo sana.Hawana challengei ktk kupita ktk dunia ya watu wasio jua huku wakiwa hawajui kuwa hawajui
 
Ismael Jussa said:
Ni ipi Mifano ya Muungano wa Mkataba?
- Muungano wa Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.
- Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye wanachama 5 mpaka sasa.
- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS).
PAMOJA TUNAWEZA
Kakke, GHIBUU, mpemba mbishi, Barubaru, Kibunango, Pakacha,

..haya Jussa anasema mfano wa muungano wa mkataba ni EAC!!

..sasa hebu ndugu zangu wa-ZNZ tuelezani ni mara ngapi mimi na Nguruvi3 tumewashauri tukajiunge EAC kuliko kupoteza muda kwenye mkataba baina ya Tanganyika na Zanzibar??
 
Joka kuu, huo mfano wa EAC unamaliza hoja zao. Kama wanataka muungano wa mkataba kama EAC(ambayo si muungano ni jumuiya kama ilivyo EU) kwanini wasivunje muungano uliopo halafu wakaomba kiti EAC kama walivyofanya Burundi na Rwanda.
Kwanini wanataka kitu cha pembeni kinachofanana na EAC na wala si kuingia EAC wazima wazima.

Hawa wanajificha, lakini Sheni kawaambia ukweli. Sheni alisema 350,000 wanafaidika na muungano kuanzia huduma za jamii, biashara, ajira na akasema Elimu ya juu ndio muhimu sana.

Kwa mantiki hiyo hutasikia hata mmoja akipanua mdomo na kusema vunja muungano. Wanauma uma maneno vyumbani .

Mkuu Joka kuu hawa hawana pa kutokea, wanaihitaji Tanganyika kuliko wanavyoizodoa.
Kundi la Waarabu limeanza kubainika na Wazanzibar hawataki kusikia upuuzi wa mkataba.

Ukiweka mkataba ina maana kila upande ufaidike, sasa Tanganyika itajiuliza tuweke mkataba wa kitu gani, kusaidiana au kubebana.

Tumewashika pabaya hawana ujanja. Ujanja wa kutishia vunja muungano sasa umekwama. Ni ima wakae kwa adabu na heshima au waondoke. Hatuwahitaji kwa lolote na wanajua hivyo.

Mkataba mwisho chumbe

LET ZANZ GO
 
Mwache Shein aseme analojisikia kwa vile ana mdomo hakatazwi kusema lakini kumbuka mwisho wa mchezo 'Ngoma' inaletwa kwa wananchi! Hata wakati wa referendum ya kuundwa GNU kuna watu walisimama hadharani na kupinga lakini ilipoletwa kwa wananchi ilipata baraka. Hadi muda huu zaidi ya 80% ya waliotoa maoni ni waumini wa MKATABA.
Nimekushangaa sana uliposema mumetushika pabaya na unasema Muungano wa Mkataba mwisho Chumbe!!!!! Kumbe nyinyi ndio munaotuhitaji na wala hamuwezi kutukosa! "Kuna watu wanatishana kila pale Zanzibar inapodai maslahi yake kwa kusema wanataka kumrejesha Sultani (Waarabu), Sultani (Waarabu) atoke wapi tena wakati ameshakufa zamani,, tusitishaneee" Amani Karume- Kizota. Lakini jambo la kushangaza zaidi nyinyi hua munawatishia Wazanzibari kuhusu Sultani (Waarabu) mbona hatujawahi kuwasikia munatishiana kwa Malkia wa Uingireza!!
 
Hivi anaewazuia kujiondoa kwenye muungano ni nani? Mna rais na baraza lenu la kutunga sheria, si mpitishe tu azimio la kujiondoa?
 
Back
Top Bottom